Na Mwl Peter Mabula

Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze ujumbe wa  Neno la MUNGU.

2 Nyakati 16:12-13 '' Akashikwa Asa na ugonjwa wa miguu katika mwaka wa thelathini na kenda wa kumiliki kwake; ugonjwa wake ukazidi sana; lakini hakumtafuta Bwana katika ugonjwa wake, bali waganga. Asa akalala na babaze, akafa katika mwaka wa arobaini na mmoja wa kumiliki kwake. ''

Asa alikuwa mfalme wa Israeli.

✓✓Asa alikuwa mwanadamu  kama walivyo wanadamu wengine wowote.

✓✓Katika maisha ya Asa ikafika kipindi akaugua. 

✓✓Baada ya kuugua Asa akaenda kwa waganga ili kutafuta tiba. 
✓✓Alitarajia waganga wamponye lakini  kwenda kwake kwa waganga ndiko kukawa mwanzo wa kifo chake.

✓✓Kwa waganga hakukuwa na msaada wote  kwa Asa ndio maana akafa.

◼️Biblia hapo inaonyesha kwamba, kama Asa angemtafuta MUNGU na sio waganga angepona na kuendelea kuishi, ila kwa kosa lake la kutegemea waganga Asa alikufa.

Ndugu, usiwe kama Asa ambaye alitumainia waganga akafa wala hakupona ugonjwa wake, wala hakupata hitaji lake.

Neema ya MUNGU tu ndio huwafanya hai wanadamu wote hata waenda kwa waganga  lakini ukweli ni kwamba MUNGU hawezi kumponya mtu alieenda kwa waganga kwasababu mtu huyo akipata nafuu kidogo tu atamtukuza mganga na sio MUNGU aliyemponya.

✓✓Hata Leo akina Asa ni wengi sana.
Watu wengi sana wamekufa kwa sababu tu ya kutegemea misaada ya waganga.

Watu kama hao wangeenda kwenye maombezi au Kanisani  hakika wangepona na kuendelea na maisha.

Misaada ya waganga ni misaada feki na ambayo haitakiwi kufuatwa na mcha MUNGU yeyote yule.

Ndugu, usiwe kama Asa ambaye alitumainia waganga akafa wala hakupona ugonjwa wake, wala hakupata hitaji lake.

◼️Kama yuko yeyote anayeponya basi na yeye mwenyewe anatakiwa awe hawezi kuumwa wala kufa, lakini waganga wote huumwa na hufa wakati wanajitangaza kwamba wanazo dawa za kuponya, mbona wao hawaponi?.

Hivyo ndugu zangu naomba mtambue kwamba hakuna msaada hata mmoja kwa mganga wa kienyeji.
Ndugu, usiwe kama Asa ambaye alitumainia waganga akafa wala hakupona ugonjwa wake, wala hakupata hitaji lake.

Waganga wa kienyeji ni watumishi wa ulimwengu wa roho wa Giza, na kazi yako ni kueneza Giza la shetani.

Isaya 5:20 ''Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza; watiao uchungu badala ya utamu, na utamu badala ya uchungu!''

Kama waganga wangekuwa wanatoa baraka basi  na wao pia wangekuwa matajiri na wasingemtaka  mteja kwenda na pesa au mali maana kwao hivyo vyote vingekuwepo tu maana wanao uwezo wa kuvileta, lakini wanaoongoza kwa umasikini  ni pamoja na waganga. 
Kwa waganga hata viti wakati mwingine unaweza ukakuta hakuna.

Ndugu, usiwe kama Asa ambaye alitumainia waganga akafa wala hakupona ugonjwa wake, wala hakupata hitaji lake.

Kwenda kwa Waganga wa kienyeji ni sawa na kuchukua mimba ya makapi ili uje uzae majani makavu.
Isaya 33:11 '' Ninyi mtachukua mimba ya makapi, mtazaa majani makavu; pumzi yenu ni moto utakaowateketeza wenyewe. ''

Jirani yetu mmoja kule kijijini nilikokulia  alikuwa mganga wa kienyeji maarufu sana, na mara kadhaa tulikuwa tunapika kwake maana ni jirani  na kwetu na njia yetu ilipitia nyumbani kwake, na watoto wake kila siku tuko nao iwe shuleni au kwenye uchungaji wa mifugo maana tulikuwa wafugaji na yeye pia alikuwa mfugaji. 
Nilikuwa naona watu wengi tu wakienda kwake ili kupatiwa tiba mbalimbali lakini sikuwahi kumuona mteja hata mmoja akishukuru kwamba amepata msaada, zaidi sana ni kulaumu tu. 
Kuku za wateja na mbuzi zao zilikuwa zinaliwa sana katika familia ile lakini msaada haukuwepo, na hata ukiwepo basi ulikuwa ni msaada wa kiini macho yaani unatoka leo unashangilia lakini kesho utaendelea na kulia kama kawaida.

Nilichojifunza kwa waganga ni  kwamba wanajua sana kucheza na akili za watu.
waganga ni  wanasaikolojia wazuri sana maana mikakati yao humtisha mteja na mteja huyo kujikuta akipelekeshwa kama mbuzi ndani ya gunia.

Hebu jiulize kwamba unakwenda kwa mganga na anakuambia hakikisha unakuja kesho yake ukiwa na kuku mweupe jogoo mkubwa, tena anakutahadhalisha kwamba usije ukathubutu kuja na kuku mwekundu ama mweusi.
 Kwa haraka haraka unaweza ukaona kama kwamba mganga yule hana uhitaji sana wa kuku ndio maana amesema usilete kuku nje na rangi ya kuku aliyekuambia, lakini ukweli ni kwamba hiyo ni janja tu ya kukufanya utafute kuku mweupe kwa makini sana na umpeleke ukijua kwamba shida zitaisha kumbe unapeleka kitoweo kizuri na wewe unaenda kuvuna laana na maagano ya kishetani.

Ndugu, usiwe kama Asa ambaye alitumainia waganga akafa wala hakupona ugonjwa wake, wala hakupata hitaji lake. 
Waganga hawawezi kukuletea utajiri ila wanachoweza kukuletea ni laana, vifungo vya giza, mikataba ya kishetani  na kukuibia tu.

Kuna watu wanaishi maisha ya mashaka sana kwa sababu tu ya masharti waliyopewa na waganga.
Kuna watu hawaruhusiwi jua lichomoze wakiwa nyumbani, wamedanganywa na waganga na wanauishi uongo huo.

Kuna watu katika kupishana njiani na watu lazima yeye akae kushoto maana akikaa kulia atapata shida, huo ni uongo wa waganga.

Kuna watu wamepewa masharti na waganga ya kuhakikisha wanatembea bila kuvaa nguo ya ndani.

Kuna watu hata wamepata laana kubwa kwa kuambiwa ni lazima walale na wazazi wao au watoto wao ndipo watafanikiwa, hiyo ni sayansi ya shetani ya kuwapata wanadamu wasiompenda KRISTO.

Ndugu, usiwe kama Asa ambaye alitumainia waganga akafa wala hakupona ugonjwa wake, wala hakupata hitaji lake.

Mtu anayewategemea Waganga wa kienyeji, huyo mtu amelaaaniwa Maana anategemea Wanadamu.
Yeremia 17:5 '' BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA. ''

 Amelaaniwa mwanadamu anayewategemea wanadamu na amewafanya kuwa kinga yake.

Amelaaniwa mtu yule ayakwenda kwa waganga ili wamsaidie mambo yake.

Amelaaniwa mtu yule  anayeishi kwa kutegemea uganga na waganga.

Hakuna msaada hata mmoja kwa waganga ila msaada ni kwa MUNGU tu.
Msaada ni katika KRISTO YESU pekee.
Amelaaniwa mtu yule anayetegemea hirizi na tunguli.

Amelaaniwa mtu yule anayetafuta mtoto kwa waganga, kwanza mtoto wa kwa waganga huyo ni mtoto wa dawa na siku zote mtoto wa dawa ni tatizo.

Amelaaniwa mtu yule anayewafuata wateja kwa mganga wa biashara yake .

Ndugu, usiwe kama Asa ambaye alitumainia waganga akafa wala hakupona ugonjwa wake, wala hakupata hitaji lake.

Je, unategemea uganga wewe?
Neno la MUNGU linasema juu yako kwamba ''Utalaaniwa uingiapo, utalaaniwa na utokapo, BWANA atakuletea laana na mashaka, na kukemewa, katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya, hata uangamie na kupotea kwa upesi; kwa ule uovu wa matendo yako, uliyoniacha kwayo.-Kumb 28:19-20 '' 

Kuwategemea waganga ni kuifanya ghadhabu ya MUNGU iwe juu yako.

Ndugu, usiwe kama Asa ambaye alitumainia waganga akafa wala hakupona ugonjwa wake, wala hakupata hitaji lake.

Kama umezoea kuweka bajeti za kwa waganga wa kienyeji nakuomba kuanzia leo acha  na badala yake  panga bajeti za kwenda Kanisani au kwenye mikutano ya injili au panga bajeti ya kuwezesha kazi ya MUNGU.

Kama umezoea kuwaona waganga ndio kila kitu katika maisha yako nakuomba  kupitia ujumbe huu ufahamu wako mzuri ukurudie leo, na uanze kuona kwamba YESU KRISTO ndiye kila kitu kwako.

Kama umezoea kila kabla ya kulala  unashika  hirizi au mzizi uliopewa na mganga  nakuomba acha na tupa vyote hivyo na anza kumwabudu MUNGU BABA katika ROHO na kweli.

Anza kumwabudu MUNGU wa mbinguni na sio waganga.
Zaburi 55:16 ''Nami nitamwita MUNGU, Na BWANA ataniokoa;''
Asante kama umelielewa  Neno la MUNGUndugu yangu ila nina Neno la mwisho leo Kwa ajili yako.
Bwana YESU KRISTO Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By  Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai.
+255714252292.
Ubarikiwe sana kwa Kusoma somo hili.

Comments