KUHUSU ADUI ANAYETAKA KUKUSUKUMA.

 

Na Mwl Peter Mabula,  Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai milele 

Zaburi 118:13 " Ulinisukuma sana ili nianguke; Lakini BWANA akanisaidia."


✓Inawezekana yuko adui yako alikusukuma sana kwenye ulimwengu wa roho akitaka akuangushe, alitaka ndoa yako ivunjike, alitaka uchumba wako ufe.


✓Inawezekana yuko adui alitamani sana uanguke lakini MUNGU akakusaidia.


✓Inawezekana wako wakuu wa giza walitaka ufe lakini YESU KRISTO akasema uishi ndio maana sasa unaishi hata kama kwenye ulimwengu wa roho wakuu wa giza walishakuzika.


✓Sio watu wote ni wema kwako, wengine ni mawakala wa shetani wakikuwinda kupitia kuwa na ukaribu na wewe.


✓Sio kila mtu anayekuchekea  ana mpango mzuri na wewe, wengine ni wapambe wa shetani.


✓✓Ndugu, Leo omba ukimshukuru MUNGU kwa kukulinda  dhidi ya maadui waliotaka kukuangusha ili udhurike au usiwepo duniani.


✓✓Leo omba pia ukimwambia MUNGU Baba akulinde dhidi ya kila adui anayekutafuta ili akuangushe, aangushe biashara yako, aangushe kipato chako, akufukuzishe kazi n.k


✓✓Hakikisha unamtukuza MUNGU aliyekushindia wakati mawakala wa shetani wameinuka maishani mwako.


✓✓Inawezekana kwenye ndoa yako sasa mna amani na furaha lakini yuko mtu kila siku anatamani asikie mmeachana, inawezekana anapita hata jirani na kwako akidhani angalau atasikia mnazozana lakini MUNGU wa milele amewalinda.


✓✓Inawezekana yuko aliyekuendea kwa mganga ili tu uanguke.


✓✓Inawezekana yuko aliyetambika au aliyetoa sadaka kwa mashetani ili kukufunga lakini YESU KRISTO Mwokozi amekulinda.


✓✓Inawezekana wapo wanaokuwinda kila siku lakini kwa sababu wewe umeokoka basi MUNGU amekuagizia Malaika zake ili wakulinde usiku na mchana.


Zaburi 91:11 "Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote."


Wakuu wa giza, wachawi na majini wamejaribu kila mbinu kukuwinda lakini JEHOVAH aliye hai amekulinda.


Ndugu Mshukuru MUNGU aliyekulinda mbele za maadui zako.


Mtukuze yeye na ishi maisha matakatifu ya Wokovu wa KRISTO huku ukimpendeza MUNGU siku zote na kumtukuza.


Ni kweli walitaka kukuangusha ila MUNGU akakusaidia, ni kweli walitaka ufe kwa magonjwa ya kurogwa lakini jina la YESU KRISTO likawa msaada kwako. Ni kweli walifanya kila mipango kuua ndoa, uzao, uchumi na kila baraka yako lakini MUNGU akakulinda.


Ndugu, mtukuze MUNGU aliyekulinda dhidi ya maadui zako.

MUNGU akubariki sana.

By Peter Mabula.

Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292

Ubarikiwe

Comments