KUOTA UKO SHULENI NA ULISHAMALIZA SHULE.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 

Ndoto za kuota uko shuleni na ulishamaliza kusoma zina maana hizi chini haijalishi uliona unafanya matukio tofauti hapo shuleni 


Kuota uko shule ina maana zifuatazo kulingana na ulivyoona.


1. Kuota ndoto uko Shule hata kama ulishamaliza shule tafsiri yake ni uhitaji wa maarifa fulani ambayo yanatakiwa yakutoe sehemu moja na kukupeleka sehemu nyingine bora zaidi.

Yaani kuna maarifa ya Neno la MUNGU unahitaji ili uvuke hatua uliyopo.

Mithali 12:1 " Kila apendaye mafundisho hupenda maarifa; Bali yeye achukiaye kulaumiwa ni kama mnyama. mtu mwema atapata upendeleo kwa BWANA."


2. Kuota ndoto uko darasa ambalo umeshavuka kwa jinsi ya mwili maana yake kufikiri kwako kuko chini ya kiwango MUNGU anachotegemea. mfano hai ni mtu umeshamaliza chuo kikuu lakini kila mara unaota uko shule ya msingi.

Maana yake kiwango chako cha kufikiri vyema ni cha chini sana.

Waebrania 5:12 " Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya MUNGU; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu."

Kwa maana nyingine unapoota uko darasa ambalo ulishalipitia siku nyingi maana yake umekwama kufikiri, wewe ni mchanga kiroho,hufikiri vyema yaani inavyotakiwa, unahitaji sana kujifunza Neno la MUNGU.

Au fikra zako zimekamatwa na shetani.


3. Kuota umeyarudia maisha ya utotoni au shule ya msingi au sekondari wakati ulihitimu huko zamani maana yake unafuatiliwa na roho ya kuanguka, pia hii ni dalili ya kufungwa na roho za mizimu au roho za kurithi za mababu.


4. Kuota uko shuleni maana yake nyingine ni hii. Kuna eneo umekwama katika maisha yako.


5. Kuota uko shule maana yake katika hatua Fulani ya ki maisha unayoiendea unahitaji maandalizi ya kutosha


6. Kuota upo darasani au mazingira ya shule ambayo ulishavuka, maana yake katika maisha yako, kuna eneo bado hujaivuka kimaisha. Mahali ulipo sipo unapotakiwa uwepo, kinachohitajika ni kujifunza sana Neno la MUNGU na kumsikiliza ROHO MTAKATIFU


7. Kuota uko shule maana yako uko chini kiviwango vya kiroho.

Ndugu hakikisha unajifunza Biblia na Neno la MUNGU litakusaidia kujua maana ya ndoto yako.

Ishi maisha matakatifu ya Wokovu wa YESU KRISTO na hakikisha sana unaenda katika ROHO MTAKATIFU.

MUNGU akubariki.

By Peter Mabula.

Mtenda kazi katika shamba la MUNGU.

Comments