MUNGU AKUPE NDOA WEWE MWANAMKE UNAYEHITAJI NDOA.

 


Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU 


Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu yangu.
Siku ya  tarehe 31 December 2024 nikiwa safarini kurejea Dar es salaam nilijulishwa na Mbingu kitu Cha ajabu sana. Niliambiwa niwajulishe rafiki zangu Wanawake Mtandaoni na Kanisani ambao hawajafunga Ndoa na wanatamani hivyo.
Kwamba "Waombe Kuonekana" Nami niwaombeee "Kila Mtu apate atakayempenda kwa ajili ya Ndoa"

Ngoja nifafanue kidogo.

Wewe Binti au Mwanamke unayehitaji Ndoa omba MUNGU akupe Kuonekana kwa huyu atakayekupenda na kukuchumbia Kisha mfunge Ndoa takatifu, Mwaka huu wingu hilo limefunguka nami kwa Maombi yangu yanayotokana na Ufunuo huu wanawake 200 wanaenda kufunga Ndoa.

Inawezekana Maombi Yako kila mara umekuwa ukiomba MUNGU akufunulie Mume wako, wakati huu  badilisha Maombi, omba Kuonekana kwa huyo aliyekusudiwa kwa ajili Yako kwa ajili ya Ndoa.
Ngoja nikupe mifano hai.

✓✓Rebeka alionekana kisimani ikawa Chanzo Cha kuolewa na Isaka 

Mwanzo 24:13-14 " Tazama! Nimesimama karibu na kisima cha maji, na binti za watu wa mjini wanatoka kuteka maji, basi na iwe hivi; yule msichana nitakayemwambia, Tua mtungi wako, nakuomba, ninywe; naye akasema, Unywe, nami nitawanywesha na ngamia zako pia; basi huyu na awe ndiye uliyemchagulia mtumishi wako Isaka; na kwa hayo nitajua ya kuwa umemfadhili bwana wangu. Ikawa, kabla hajaisha kunena, tazama, Rebeka anatokea, binti wa Bethueli mwana wa Milka, mkewe Nahori, ndugu wa Ibrahimu, naye ana mtungi begani pake."

Rebeka alikuwa anaenda Kisimani pale kila mara tena alikuwa Mwenyeji ila hakuonekana hadi siku ya Kuonekana iliyomfanya aolewe na Isaka, Binti yangu Mwaka huu omba Kuonekana na utaonekana na kupata mwenzi wa Ndoa.

✓✓Watu wote walio kwenye Ndoa walianza na kuonana na huko kuonana kukatengeneza "Kuonekana" Wewe katika Jina la YESU KRISTO omba Kuonekana kwa huyo utakayefunga naye Ndoa takatifu.

✓✓Si unafahamu habari za Esta?

Huyu Binti alionekana kwa Mfalme Ahusuero ndipo akaolewa naye.

Esta 2:17 "Mfalme akampenda Esta kuliko wanawake wote, naye akapata neema na kibali machoni pake kuliko mabikira wote; basi akamtia taji ya kifalme kichwani pake, akamfanya awe malkia badala ya Vashti."

Mbele ya macho ya Ahusuero walipita mabinti wengi sana na warembo sana ila wote hawakuonekana, Esta tu ndio alionekana hivyo akaolewa.
Bwana YESU KRISTO akupe huu mwaka uwe wa Kuonekana kwako.

✓✓Hata Eva alionekana kwenye macho ya Adamu ndio Maana Adamu akamuoa na kumkubali kama Mkewe.

Mwanzo 2:22-24 " na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA MUNGU akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu. Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume. Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja."

Adamu alimkubali Eva baada ya Eva Kuonekana. Binti yangu omba uonekane kwa huyo utakayefunga naye Ndoa takatifu kwa kusudi la MUNGU.

Omba Maombi haya ni nijulishe Inbox majina Yako nami nitakuombea MUNGU akupe Mwanaume atakayekupenda kwa ajili ya Ndoa takatifu, mwaka huu utafunga Ndoa kwa Jina la YESU KRISTO.
Maombi yangu juu Yako utakayenijulisha majina Yako ni haya.

Mwanzo 29:18 "YAKOBO AKAMPENDA RAHELI akasema, Nitakutumikia miaka saba kwa kumpata Raheli, binti yako mdogo."

Kama Raheli alipendwa na Yakobo, na Wewe mwaka huu anaenda kutokea Mwanaume atakayekupenda kwa Upendo sahihi wa Ndoa.
MUNGU akuletee Mwanaume sahihi atakayekupenda. Mimi Peter Mabula nitakuombea Wewe rafiki yangu kwa ajili ya hilo 

Mwanzo 34:3 "Moyo wake ukaambatana na Dina binti Yakobo, akampenda huyu msichana, akasema na huyu msichana kwa maneno mazuri."

Dina alipendwa, na MUNGU akupe Mtu sahihi atakayekupenda kwa ajili ya Ndoa takatifu, nitakuombea juu ya hilo.

Ndugu usikate tamaa, usichoke maana Mwaka huu ni tofauti na Miaka iliyopita 
Biblia Iko wazi kwamba  hakuna Mtu atakayekosa mwenzake.

Isaya 34:16" Tafuteni katika kitabu cha BWANA mkasome; hapana katika hao wote atakayekosa kuwapo, hapana mmoja atakayemkosa mwenzake; kwa maana kinywa changu kimeamuru, na roho yake imewakusanya."
Binti yangu ishi Maisha matakatifu ya Wokovu wa Bwana YESU KRISTO maana hutakosa Mtu kwa ajili ya Ndoa, Bali utapata.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
Hakikisha umeokoka na unaishi Maisha matakatifu ya Wokovu wa Bwana YESU KRISTO.
By Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai milele.
+255714252292.
Ubarikiwe 

Comments