![]() |
Na Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu zangu wote.
Kwenye ndoto Mtu anaweza kuota Yuko uchi, amesimama uchi au anatembea uchi.
Ni ndoto ya kukujulisha vitu ambavyo unatakiwa ufanyie kazi haraka katika MUNGU ili uwe salama.
Maana ya kuota uko uchi au kumuona Mtu ndotoni Yuko uchi ni hizi.
1. Kuna Siri unayo ambayo Kuna Mtu au watu unadhani hawajui lakini taarifa ya rohoni ni kwamba hao watu unaodhani hawajui Siri hiyo wanajua na ndio maana wanakudharau.
Maombolezo 1:8 "Yerusalemu AMEFANYA DHAMBI SANA; Kwa hiyo amekuwa kama kitu kichafu; Wote WALIOMHESHIMU WANAMDHARAU, KWA SABABU WAMEUONA UCHI WAKE; Naam, yeye anaugua, Na kujigeuza aende nyuma."
2. Ni taarifa ya rohoni kwamba kwa wakati huu hauna Wokovu wa KRISTO, hivyo ni hatari sana kwako.
Ufunuo 16:15 (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)
✓✓Wokovu wa KRISTO ni vazi ambalo unatakiwa kulivaa siku zote.
Isaya 61:10 ✓✓Nitafurahi sana katika BWANA, nafsi yangu itashangilia katika MUNGU wangu; maana AMENIVIKA MAVAZI YA WOKOVU, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.✓✓
Ukiona uko uchi maana yake umelivua vazi la Wokovu hivyo ni heri sana kurudi kwa Bwana YESU KRISTO ili vazi la Wokovu lirudi kwako.
3. Nguvu za giza zina Nguvu dhidi Yako hivyo hivyo ukikaa vibaya zitakuabisha.
Matendo 19:16 "Na yule mtu ALIYEPAGAWA NA PEPO MCHAFU akawarukia wawili, AKAWAWEZA, AKAWASHINDA, HATA WAKATOKA MBIO KATIKA NYUMBA ile hali WA UCHI na kujeruhiwa."
◾Ukikaa mbali na YESU KRISTO uwe na uhakika mawakala wa shetani watakuabisha.
✓✓Amua kukaa Karibu na YESU KRISTO siku zote ili Nguvu za giza wasipate nafasi ya kukuabisha.
4. Roho ya kuabishwa, yaani Kuna mipango ya kukuletea aibu kubwa Wewe.
Ezekieli 23:29 "nao WATAKUTENDA MAMBO KWA CHUKI, watakuondolea kazi zako zote, WATAKUACHA UCHI, HUNA NGUO NA AIBU YA MAMBO YAKO ya kikahaba ITAFUNULIWA, uasherati wako na uzinzi wako."
◾Kuna mambo mbele Yako yanapangwa ulimwengu wa roho wa giza ili upate aibu kubwa.
◾Kuna mipango ya kichawi au kiganga dhidi Yako ili uabike.
✓✓Kaa vizuri na YESU KRISTO Kisha omba kwa Jina lake kukataa "roho ya kuabishwa na Mawakala wa Shetani"
Zaburi 119:6 "NDIPO MIMI SITAABIKA, NIKIYAANGALIA MAAGIZO YAKO YOTE."
✓✓Ndugu fuata maagizo yote ya MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi.
5. Ni taarifa kuwa umefanya kosa kubwa mbele za MUNGU hivyo geuka MUNGU asije akakuabisha yeye mwenyewe.
Nahumu 3:5 "Tazama, mimi ni juu yako, asema BWANA wa majeshi; nami nitafunua marinda yako mbele ya uso wako; NAMI NITAWAONYESHA MATAIFA UCHI WAKO, na falme aibu yako."
✓✓Ndugu ukiendelea na mabaya MUNGU mwenyewe atakuabisha hivyo Acha mabaya, watu wa namna hii MUNGU anawapa nafasi nyingine ili wageuke kuacha mabaya, MUNGU anawapenda ndio maana anataka waache njia zao mbaya.
Ili ukishupaza shingo MUNGU mwenyewe atakuabisha.
Nahumu 3:6 "Nami nitatupa uchafu uchukizao juu yako, kukufanya uwe mchafu, NAMI NITAKUFANYA KUWA KITU CHA KUTAZAMWA KWA DHAR AU."
✓✓Hivyo tubu haraka kwa MUNGU katika KRISTO YESU na rejea kwenye utakatifu.
6. Kuwa uchi kiroho ni kupungukiwa na utukufu wa MUNGU.
Ezekieli 16:7 "Nalikufanya kuwa maelfu-elfu, kama mimea ya mashamba, ukaongezeka, na kuzidi kuwa mkubwa, ukapata kuwa na uzuri mno; matiti yako yakaumbwa, nywele zako zikawa zimeota; lakini ulikuwa uchi, huna nguo."
Kupungukiwa Utukufu wa MUNGU ni nini?
✓✓Ni kupungukiwa na uwepo wa Nguvu za MUNGU.
✓✓Ni kupungukiwa na Utakatifu.
✓✓Ni kuondokewa na uwepo wa ROHO MTAKATIFU kwenye Maisha Yako.
◼️Zingatia sana kumsikiliza na kumtii ROHO MTAKATIFU ili ubaki katika kusudi la MUNGU daima.
7. Kaa vizuri na MUNGU maana yeye mwenyewe atakuabisha kwa sababu ya makosa au Dhambi Fulani mbele zake.
Ezekieli 16:36" Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu uchafu wako umemwagwa, NA UCHI WAKO UMEFUNULIWA, kwa njia ya uzinzi wako pamoja na wapenzi wako; na kwa sababu ya vinyago vyote vya machukizo yako; na kwa sababu ya damu ya watoto wako, uliyowapa;"
✓✓Ni taarifa ufanye haraka kutengeneza na Bwana YESU KRISTO ili MUNGU asikuabishe.
✓✓Ukiendelea na uasi MUNGU atakuabisha na matendo Yako maovu yatajulikana kwa watu wote.
Isaya 47:3 "Uchi wako utafunuliwa, Naam, aibu yako itaonekana. Nitalipa kisasi; simkubali mtu ye yote."
Zingatia mteule wa KRISTO na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.

Comments