.
![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Tunafahamu kwa habari ya uumbaji?
◼️Ni kwamba Mwanzoni MUNGU aliumba Mbingu na Dunia.
Mwanzo 1:1 "Hapo mwanzo MUNGU aliziumba mbingu na nchi."
✓✓Mwanzo huu ni Mwanzo wa Ardhi tunayoiona na Anga tunayoiona, Anga tunayoiona ndio Mbingu.
✓✓Mwanzo huu hauhusishi Mbinguni makazi ya MUNGU Wala Mwanzo huu hauhusishi Mwanzo wa Malaika Wala viumbe walio Mbinguni, hao uumbaji wao MUNGU alishaufanya miaka Isiyojulikana Kabla.
Sasa uumbaji huu wa Mbingu na Nchi ulikuwa kwa ajili ya Mwanadamu na Wanyama na Samaki wa Baharini, Lengo kubwa la uumbaji huu ulikuwa kwa ajili ya Mwanadamu.
◼️MUNGU ndiye aliyeumba viumbe vyote kwa ustadi Mkubwa.
Mwanzo 1:21" MUNGU akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; MUNGU akaona ya kuwa ni vyema."
◼️Kwa sababu Lengo kuu la uumbaji linamhusu Mwanadamu MUNGU alimwandalia Mwanadamu makazi ndio maana akaumba Mbingu na Ardhi.
◼️Ili Mwanadamu ajue majira na Nyakati MUNGU akaumba Usiku na Mchana.
Mwanzo 1:4-5" MUNGU akaiona nuru, ya kuwa ni njema; MUNGU akatenga nuru na giza. MUNGU akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja."
◼️Baadae MUNGU akamuumba Mwanadamu Mwanaume na Mwanamke.
Mwanzo 1:27" MUNGU akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa MUNGU alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba."
◼️Baada ya Mwanadamu kuumbwa akapewa majukumu.
Mwanzo 1:28 "MUNGU akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi."
Malengo makuu ya MUNGU alipowaumba Wanadamu.
A. Ili Mwanadamu awe mtawala wa Viumbe wengine.
Mwanzo 1:26" MUNGU akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi."
B. Mwanadamu kuzaa, kuongezeka na kutiisha.
Mwanzo 1:28 "MUNGU akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi."
✓✓ Kutiisha maana yake kumiliki na kujaza nchi na kuenea maeneo yote ya Dunia.
✓✓Katika kuzaa MUNGU alikusudia Ndoa ya Mume mmoja kwa Mke mmoja ndio maana aliumba hivyo.
Mwanzo 2:18" Bwana MUNGU akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye."
C. Kila Mwanaume awe na Mke wake na Kila Mwanamke awe na Mume wake.
Mwanzo 2:24 "Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja."
Nini tunajifunza katika somo la Leo?
1. Kila aliyeumbwa na MUNGU amepewa jukumu na MUNGU.
✓✓Kama unaishi tambua unalo jukumu jema uliloumbwa nalo na MUNGU Baba wa Mbinguni.
✓✓Yapo majukumu mengi lakini jukumu la kwanza ni kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na kuishi maisha matakatifu katika Wokovu.
1 Petro 1:15 ''bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;"
Ndio maana MUNGU alimleta Bwana YESU KRISTO ili Wanadamu wote tuhusike na jukumu la kumpokea kama Mwokozi kama tunauhitaji uzima wa milele.
Yohana 3:16 "Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."
◼️Ndugu usilikwepe kamwe jukumu hili la kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako maana ni jukumu la kila Mwanadamu mwenye akili nzuri.
2. Ni mpango wa MUNGU uwe katika Ndoa Yako takatifu.
✓✓kama huna Ndoa na unatamani kuingia katika Ndoa idai hiyo Ndoa kwa Maombi Kisha fuata utaratibu mtakatifu ili uipate Ndoa Yako maana ipo na iliumbwa na MUNGU katika utakatifu.
Yeremia 29:6 "oeni wake, mkazae wana na binti; kawaozeni wake wana wenu, mkawaoze waume binti zenu, wazae wana na binti; mkaongezeke huko wala msipungue."
3. Ndoa ya Ki MUNGU ni Mume mmoja kwa Mke mmoja, si zaidi ya hapo.
Mwanzo 2:24 "Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja."
4. Kama umekosa uzao katika Ndoa Yako Ahadi ya MUNGU kwako ni kuzaa na kuongezeka.
Mwanzo 1:28 "MUNGU akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi."
◼️Hivyo iombe Ahadi hiyo ya kuzaa katika Ndoa yako na itakuja Kwako kwa Jina la YESU KRISTO Mwokozi.
Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments