![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
Mwanzo 11:1 "Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja."
✓✓Biblia inasema Nchi yote ilikuwa na usemi mmoja yaani Dunia yote ilikuwa na lugha Moja, watu wote Duniani waliongea lugha Moja.
Sijui ilikuwa lugha gani lakini ilikuwa lugha Moja kwa watu wote.
Sidhani kama lugha hiyo inatokana na lugha yeyote ya Leo, ingekuwa hivyo isingewezekana Wanadamu wote kutawanywa kwa lugha Maana lugha Mama wote wangeisikia.
Mwanzo 11:8 "Basi BWANA akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji."
✓✓Lugha hii Moja ilikoma baada ya Wanadamu kwa kutenganishwa kwa lugha, baada ya lugha Moja kuwafanya wafanye mambo yasiyo kusudi la MUNGU wa Mbinguni.
Nini nataka kusema Leo?
1. Umoja mbaya unaweza kuvunjwa na MUNGU kama huo umoja unaharibu kusudi lake.
Mwanzo 11:7 "Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao."
◼️Hivyo unavyoona umoja umevunjwa na MUNGU kubaliana Wala usilalamike.
2. Umoja uliovunjika kwa sababu ya makosa ya Wanadamu MUNGU katika KRISTO YESU ameurudisha umoja huo katika ROHO MTAKATIFU.
Waefeso 4:3 "na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa ROHO katika kifungo cha amani."
◼️ Ndugu amua tu kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako ili ROHO MTAKATIFU ahusike na Wewe.
3. Lugha zilizopo Duniani ni mpango wa MUNGU hivyo usidharau lugha Yako au lugha yeyote ya kabila lolote au lugha ya nchi yeyote, lugha hiyo Haina makosa yeyote maana ililetwa na MUNGU ili Wanadamu waenee Duniani na sio kukaa eneo Moja.
Mwanzo 11:8 "Basi BWANA akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji."
4. YESU KRISTO yuko tayari kuwaokoa watu kutoka kabila lolote na wanaozungumza lugha yeyote.
Ufunuo 5:9-10" Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia MUNGU kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa, ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa MUNGU wetu; nao wanamiliki juu ya nchi."
◼️Hivyo usitengwe na kabila au lugha katika kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako maana yeye alikuja kwa ajili ya watu wa lugha zote na makabila yote.
◾Ingawa Leo katika baadhi ya maeneo watu wanabaguana kwa lugha na kabila, anayekubagua au anayebagua watu kwa lugha au kabila mwambie Mwanzoni watu wote Duniani walikuwa lugha Moja hivyo asijivunie lugha Bali ajisifu tu kama ana MUNGU wa kweli ambaye amejifunua katika KRISTO YESU.
Yeremia 9:24 "bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni BWANA, nitendaye wema, na hukumu, na haki, katika nchi; maana mimi napendezwa na mambo hayo, asema BWANA,"
Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments