JIFUNZE KUJIWEKEA AKIBA.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 


Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu yangu.

Karibu tujifunze Neno la MUNGU.


Ukisoma Zaburi 144:13 Biblia inasema "Ghala zetu na zijae Zenye akiba za jinsi zote. Kondoo zetu na wazae Elfu na makumi elfu mashambani mwetu."


Ghala zetu na zijae Zenye akiba ya jinsi zote.


◼️Akiba ni nini?


➡️Akiba ni kitu kinachotunzwa kwa ajili ya matumizi ya Baadae.


Mithali 10:14 "Watu wenye akili huweka akiba ya maarifa; Bali kinywa cha mpumbavu ni uangamivu ulio karibu."


◼️Watu wenye Akili huweka Akiba.

MUNGU atusaidie tuwe wenye Akili ya kuweka Akiba.


✔️✔️Yusufu kwa Ufunuo wa ROHO wa MUNGU aliwaambia Taifa Zima watu wote wakati wa Mavuno mengi watunze Akiba.


Mwanzo 41:35 "Na wakusanye chakula chote cha miaka hii myema ijayo, wakaweke akiba ya nafaka mkononi mwa Farao wakakilinde kuwa chakula katika miji."


◼️Hapa tunajifunza kwamba Jambo la kuweka Akiba ni la Kibiblia kabisa ndio maana akina Yusufu kwa uongozi wa ROHO MTAKATIFU walifundisha kuweka Akiba na wakaweka Akjba na kuponya Nchi na kuponya Ndugu zake.


✓✓Hata Wewe Ndugu unaweza ukajiwekea kanuni hii wakati wa kupata vitu vingi Kumbuka kujiwekea Akiba.


✓✓Wakati umefanikiwa jiwekee Akiba.


✓✓Inawezekana umelima na kupata mazao mengi, jiwekee Akiba baadhi ya mazao.


✓✓Inawezekana biashara Yako wakati huu imepata mafanikio makubwa, Kumbuka kujiwekea Akiba.


✓✓Inawezekana umelipwa pesa nyingi au umelipwa madeni ya muda mrefu Kumbuka kuweka Akiba baadhi ya pesa.

Mimi Peter Mabula Kwa miaka 17 tangu nimeanza utumishi kwa KRISTO mwaka 2009 sikuwahi kufundisha somo kuhusu Akiba zaidi ya somo la Matendo mema  ni Akiba lakini kwa Neema ya MUNGU katika masomo ya kufundisha mwaka huu 2026 ROHO MTAKATIFU amenipa na somo hili.

Ndugu, Niko hapa kukuambia kwamba Jifunze kuweka Akiba.

Kama huwa unaweka Akiba Nakusihi endelea kuwa unaweka Akiba.


◼️Kumbuka Akiba itakufaa wakati wa Baadae.


Walawi 26:10 "Nanyi mtakula akiba ya zamani mliyoiweka siku nyingi, tena hayo ya zamani mtayatoa, ili myaweke yaliyo mapya."


◼️Unaweza ukaweka Akiba ya pesa au Akiba ya vitu kwa ajili ya matumizi ya Baadae.


1 Nyakati 22:3 "Daudi akaweka akiba tele ya chuma kwa misumari ya tarabe za malango, na kwa mafungo; na ya shaba akiba tele isiyo na uzani;"


◼️Ndugu, Jifunze hata kuweka Akiba kwa ajili ya kazi ya MUNGU, walio wa MUNGU baadhi hufanya hivyo.


1 Nyakati 29:16 "Ee BWANA, Mungu wetu, akiba hii yote tuliyoiweka, ili tukujengee nyumba kwa ajili ya jina lako takatifu, yatoka yote mkononi mwako, na yote ni yako wewe."


◼️Ndugu, Hakikisha unakuwa Mtu mwenye Akili maana Mtu mwenye Akili huweka Akiba.


Mithali 6:8 "Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno."


◼️◼️Lakini pia Usisahau kutenda mema na kuishi maisha matakatifu katika KRISTO YESU maana utakatifu huo ni Akiba Yako kwa ajili ya uzima wa milele.


1 Timotheo 6:18-19 " Watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo;

 huku wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao, ili wapate uzima ulio kweli kweli."


Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.

MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

By Mwl Peter Mabula 

Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, sadaka ya kuipeleka Injili,  Whatsapp n.k)

Ubarikiwe

Comments