SEHEMU SAHIHI YA KUTOA FUNGU LA KUMI.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu zangu wote.

Karibu tujifunze Neno la MUNGU.


Siku moja katika mtandao wa Facebook niliona Mtumishi mmoja wa MUNGU kapost ujumbe akisema ''Wale ambao hawana pa kupeleka fungu la kumi yaani zaka watume kwangu''

Nilishangaa sana kwa ujumbe huo maana nilijua kila mtu anapo Kanisani anakoabudu au anao watumishi ambao humsaidia kiroho hivyo anaweza kupeleka zaka yake huko, lakini mpaka naandika ujumbe huu nimewahi kuwasiliana na watu kadhaa ambao mwanzo sikuwaelewa kabisa waliposema niwafundishe ni wapi watoe fungu lao la kumi, ila baadae nikawaelewa.


Kumbu 12:13-14 " Ujihadhari usitoe sadaka zako za kuteketezwa katika kila mahali upaonapo; bali katika mahali atakapopachagua BWANA katika kabila zako mojawapo, ndipo utakapotoa sadaka zako za kuteketezwa, ndipo utakapotenda yote nikuamuruyo.


◼️Kumbe ni Muhimu kutoa Zaka, Sadaka, nadhiri kule alikokuchagua MUNGU, alikokuchagua MUNGU ni kule ROHO MTAKATIFU anakupa msukumo ndani Yako utoe.


➡️Mama mmoja siku moja aliniambia kwamba Kanisani kwao hawana utaratibu wa kutoa fungu la kumi ila yeye anataka kutoa fungu la kumi na haujui atatoa wapi. Moyoni mwangu nilitamani hata kumwambia nitumie mimi Peter Mabula haraka sana hiyo zaka maana nilishangaa sana kuona mtu amekosa pa kutoa fungu la kumi lakini Biblia inamtaka Mtumishi wa MUNGU kwenda kiroho na sio kimwili hivyo sikumwambia anitumie mimi.

Nilimwelekeza sehemu ya kupeleka kwenye makanisa ya karibu na aliko na akapeleka na kuniambia kwamba sasa ana amani moyoni.


➡️Ndugu mmoja siku moja aliniambia kwamba yuko nchi za mbali na huko hakuna utaratibu wa kutoa zaka, sasa ametunza zaka yake muda na anataka nimwelekeze sehemu ambapo atatoa, nilimshangaa sana maana nilidhani ananitania tu lakini nikampa ushauri wa sehemu ya kutoa katika kazi ya MUNGU kule ambako MUNGU atampa amani kutoa, na alipotoa akawa na amani moyoni.


◼️Nimewahi kuwasiliana na watu kadhaa wakisema kwamba niwaelekeze sehemu sahihi ambapo watakuwa wanatoa zaka zao na kuwa na amani.


Mwanzoni nilishangaa sana juu ya hilo maana kwangu niliona ni ajabu sana Mtu kukosa pa kutoa fungu la kumi lakini nimesemwa rohoni mwangu kuandika ujumbe huu  ili kumsaidia mtu atakayesoma ambaye hana pa kutoa fungu lake la kumi na rohoni mwake anapata msukumo wa kutoa.

◼️Kumbuka walio wa MUNGU huwezi kuwatenga na kumtolea MUNGU Zaka, sadaka na dhabihu.


✓✓Dhabihu ni Sadaka ya hiari ambayo Mtu ansiongeza kwenye fungu lake la kumi.


➡️Inawezekana uko nchi ambapo makanisa ya kweli hakuna mfano Uarabuni.


➡️Inawezekana Kanisani kwenu hakuna utaratibu wa kutoa fungu la kumi.


➡️Inawezekana kuna mahali ulikuwa unatoa na huna amani maana Mtumishi wa hapo sio mtumyishi mwaminifu wa MUNGU katika KRISTO YESU.


➡️Inawezekana unaabudu kwa nabii wa uongo au kwa wakala wa shetani, hama na usitoe Zaka huko.


➡️Inawezekana wewe sio Mkristo lakini unapata msukumo rohoni kutoa fungu la kumi katika kazi ya MUNGU katika KRISTO YESU.


Nilipokutana na watu ambao wanatafuta pa kutoa fungu la kumi mwanzo nilidhani wananipima ili kuona kama naweza kuwaambia wanitumie mimi, lakini nilikuja kugundua ni kweli wako watu ambao wanatamani kutoa fungu la kumi ila hawana pa kupeleka kutokana na mazingira yao.


◼️Kwanza Biblia inasema kwamba ''Ujihadhari usitoe sadaka zako za kuteketezwa katika kila mahali upaonapo;-Kumb 12:13''


◼️Hivyo sio kila mahali upaonapo panastahili wewe utoe hapo zaka, sadaka, dhabihu au nadhiri.


◼️Sio kwa kila madhabahu unaweza kutoa zaka, sio kwa kila mtumishi umuonae unaweza kumtumia fungu lako la kumi.


✔️Biblia inatoa majibu juu ya wapi upeleke zaka yako, sadaka yako ya hiari, dhabihu yako au nadhiri yako.

Biblia inasema  " Lakini mahali atakapochagua BWANA, Mungu wenu, katika kabila zenu zote, apaweke jina lake, maana, ni makao yake, elekezeni nyuso zenu hapo, nawe wende huko; pelekeni huko sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu, na sadaka zenu za hiari, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ng'ombe na ya kondoo;" -Kumb 12:5-6


 ➡️Upeleke wapi zaka zako na sadaka kulingana na Biblia?


Ni huku peleka matoleo yako.


1. Panapostahili kutoa Zaka Yako ni kule MUNGU alikolikarisha Jina lake yaani ni Kanisani kwenu unakolishwa kiroho Neno la MUNGU.

Kanisani kwenu anakoabudiwa MUNGU katika Roho na kweli toa fungu la kumi,  hutatoa tu huko kama ROHO MTAKATIFU atakukataza kutoa huko kwa sababu atakazokupa.


2. Panapostahili wewe upeleke zaka zako au sadaka zako ni mahali alipopachagua MUNGU  yaani kule ambako unasikia msukumo rohoni kupeleka matoleo yako ambako YESU KRISTO Yuko, huku utatoa Zaka Yako kama tu utagundua madhabahuni kwenu hakuko sawa kwa Sasa hivyo ulikosa amani kutoa huko, labda Mchungaji ameanguka n.k


3. Unaweza kupeleka Zaka Yako kwa Mtumishi wa kweli wa YESU KRISTO kama ROHO MTAKATIFU atakuelekeza huko labda Kanisani kwenu hawana utaratibu wa kutoa Zaka, uko kikazi sehemu ambayo hakuna Kanisa safi, uko nchi au mji ambako hakuna makanisa ya kiroho mfano Uarabuni na baadhi ya mataifa ya Asia au Mtumishi huyo anakufundisha Neno la MUNGU Kila siku na linakusaidia.


◼️Muhimu tu  jilidhishe kwanza kama huyo unayempa zaka zako ni Mtumishi mwaminifu wa Bwana YESU KRISTO.


◼️Kama mazingira yako hayakuruhusu kutoa huko uliko unaweza hata kuwatumia watumishi waaminifu wa MUNGU katika KRISTO YESU ila ni wale tu ambao ROHO MTAKATIFU atakupa amani kwao.


✔️Mtumishi husika awe ameokoka na ana ushuhuda mzuri wa maisha yake kiroho, pia utoaji mzuri ni vyema ukaampatana na kibali cha ROHO MTAKATIFU rohoni mwa mtoaji na rohoni mwa mtumishi anayepokea.


Sitasahau siku moja dada mmoja alinipigia siku akisema kwamba anataka anitumie Sadaka yake ili nimuombee apone Kansa, rohoni mwangu niliingiwa na uoga ajabu nikamwambia kwamba maombi sio mpaka utoe Sadaka lakini akasema kwamba anajua hayo yote ila yeye ameamua kutoa Sadaka ili iambatane na Maombi yangu. Nilitamani kumwambia muda ule ule kwamba usitume maana usipopona utanilaumu lakini akaniambia kwamba atanitumia jioni. Baada ya maongezi hayo nilijikuta naomba muda mrefu sana nikisema ''Eee Bwana YESU KRISTO kama huna mpango wa kumponya huyu naomba asitume Sadaka yake, au unijulishe mapema maana naweza kudhalilika kama atatuma na asipone pia kazi yako inaweza kudhalilika kama hatapona''

Niliomba maombi hayo na rohoni mwangu nikawa na na uoga mkubwa sana, jioni yule ndugu alituma na nikamuombea huku rohoni nina maswali yasiyo na majibu. Namshukuru MUNGU maana alimponya Dada huyo na hadi akanitumia ushuhuda wake nilioupost mtandaoni, ila kabla ya uponyaji nilikuwa na maswali mengi yasiyo na majibu.


◼️Sasa hata Mtumishi wa MUNGU unayepokea matoleo ya mtu inakupasa utafute kibali cha MUNGU rohoni na uwe na juhudi za kumuombea mara kwa mara huyo anayetoa kwa MUNGU kupitia Wewe.


◼️Kutoa fungu la kumi ni jambo la lazima kwa watu wa MUNGU wanajielewa hivyo kama dhehebu linakataza kutoa zaka mtu mwelewa anaweza hata akatafuta sehemu nyingine ya kutoa zaka yake ili awe na amani.


◼️Naamimi umejifunza kitu ndugu wewe usiye na sehemu ya kutoa zaka, sadaka, nadhiri, ahadi na dhabihu.


➡️Hakikisha unakuwa mtoaji na MUNGU akubariki sana.


◼️Utoaji wako jitahidi sana uambatane na utakatifu katika KRISTO ili usiishie kuwa mtoaji tu lakini huhusiki na uzima wa milele.

Hakikisha unaacha dhambi zote na mtii Bwana YESU na Neno lake.

Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.

MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

By Mwl Peter Mabula 

Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)

Ubarikiwe

Comments