KAMA UNA MPANGO WA UZIMA WA MILELE HUJAOA AU KUOLEWA USIKUBALI KUINGIA KATIKA NDOA NA MPINGA KRISTO.
![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
◼️Ujumbe wa Leo ni kwamba kama hujaingia katika Ndoa na unautaka uzima wa milele basi utakapoingia katika Ndoa Usikubali kuingia katika Ndoa na mpinga KRISTO.
◾Mpinga KRISTO ni nani?
➡️Mpinga KRISTO ni Mtu yeyote anayemkataa YESU KRISTO kuwa Mwokozi wake kwa ajili ya uzima wa milele.
1 Yohana 2:18 "Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho."
◼️Mpinga KRISTO ni mpagani mbele za MUNGU.
◼️Mpinga KRISTO huabudu shetani au Sanamu au miungu iwe kwa kujua au kwa kutokujua.
◾Utamjuaje kama ni mpinga KRISTO?
➡️Utamjua tu pale anapokataa kuokolewa na YESU KRISTO.
◼️Tangu Zamani MUNGU Mwenyewe alikataza Wateule wake kuoana na waabudu miungu.
Kumbu 7:3-4 " binti yako usimpe mwanawe mume, wala usimtwalie mwanao mume binti yake. Kwa kuwa atamkengeusha mwanao mume asinifuate, ili wapate kuabudu miungu mingine; ndipo itakapowaka hasira ya BWANA juu yenu, naye atakuangamiza upesi."
◼️Sababu kuu kwanini MUNGU anakataza Wateule wake kuoana na wapinga KRISTO ni kwa sababu Wapinga KRISTO watawakengeusha watu wa MUNGU wamwache YESU mwenye uzima wao wa milele.
Kumbu 7:4 "Kwa kuwa atamkengeusha mwanao mume asinifuate, ili wapate kuabudu miungu mingine; ndipo itakapowaka hasira ya BWANA juu yenu, naye atakuangamiza upesi."
◼️Ndugu, kama kweli una nia ya kwenda uzima wa milele na hujaingia katika Ndoa Usikubali kamwe kuingia katika Ndoa na Mtu asiye na Wokovu wa KRISTO, usiingie katika Ndoa na Mtu asiye na YESU KRISTO.
➡️Leo Kuna watu wanadanganywa kwamba waoane tu ila Kila Mtu abaki na Dini yake, Ndugu huo ni uongo na ni mtego wa shetani maana hata akikuachia YESU Wewe Kisha Watoto mtakaozaa wanamfuata shetani bado umepata hasara kuu, Usikubali uongo wa shetani.
Biblia inaonyesha kwamba shetani daima ni Baba wa uongo.
Yohana 8:44" Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo."
◼️Kwa watu ambayo tayari anapojifunza Neno hili Yuko katika Ndoa tayari Nina ushauri tu juu yao, ila ambavyo hujaingia katika Ndoa kamwe Usikubali kuingia katika Ndoa na Mtu mpinga KRISTO.
◼️Wewe ambaye uko katika Ndoa ila mwenza wako ni mpinga KRISTO ushauri wangu kwako ni huu.
1. Jichunge sana Usikubali kufuata miungu ya mwenzi wako.
Kumbu 6:14 "Msifuate miungu mingine katika miungu ya mataifa wawazungukao;"
2. Ishi Maisha ya tahadhari sana ili usiende kinyume na Maisha Matakatifu ya Wokovu wa KRISTO YESU.
1 Petro 4:2 "Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya MUNGU, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani."
3. Kama mwenzi wako anafanya juhudi akutoe kwa YESU KRISTO Usikubali kamwe, akizidi sana ni heri hata kutengana naye kuliko yeye akutenge na YESU KRISTO Mwokozi.
Mithali 1:10 "Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, Wewe usikubali."
4. Muombee ili MUNGU ampe Neema ya kuifikia kweli ya MUNGU ambayo ni KRISTO.
Yuda 1:23 "na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu, mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili."
◼️Kwa yule ambaye hujaingia katika Ndoa Narudia tena Usikubali kamwe kuingia katika Ndoa na mpinga KRISTO hata Wewe moyo wako unamuona ni Mtu Mzuri kiasi gani.
➡️Kijana Usikubali kamwe kuoa mpinga KRISTO.
➡️Binti Usikubali kamwe kuolewa na mpinga KRISTO.
Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments