![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Kuna watu wanateswa sana na nguvu za giza.
Mtu mmoja aliniandikia hivi
"Shalom Kaka Mabula,
mimi natokea kigamboni nilikuta mahubiri yako google, niliguswa sana maana kila siku mimi nikilala naota nafanya mapenzi na wanawake nisiowajua na kuna muda nikilala nakuta nimeamka na makovu ya kucha sijui tatizo nini, yaani ni mtu amenipalua kwa kucha na kunikata kwa kucha, nahitaji msaada wa maombi."
Ndugu inawezekana na wewe unateseka kama ndugu huyu au zaidi ya ndugu huyu.
◼️Mimi nakushauri amua Kuokoka ili uwe na Mamlaka ya kiroho kibali Cha kuomba ili kushinda Nguvu za giza zote.
➡️Labda tu kama Wewe ni Mtu wa Kanisani ila una Imani hapa, hicho ndio kikwazo ya matokeo ya Maombi Yako.
◼️Mimi nakushauri kwamba tafuta Kanisa la kiroho maeneo uliko na waeleze Watumishi waaminifu wa MUNGU watakuombea kwa jina la YESU KRISTO na utafunguliwa hakika.
Haiwezekani mawakala wa shetani wanaufanya mwili wako wanavyotaka na wewe unaangalia tu.
Mwambie MUNGU awaue hao manyoka(Mashetani) wanaokutesa.
Isaya 27:1 "Katika siku hiyo BWANA, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu lewiathani, nyoka yule mwepesi, na lewiathani, nyoka yule mwenye kuzonga-zonga; naye atamwua yule joka aliye baharini."
◼️Unaweza ukaitumia nafasi yako Leo ya maombi na hao wakuu wa Giza watajikuta wanalifuta jina lako kwenye ratiba ya kuonea, maana maombi yako yatapeleka uharibifu kwenye madhabahu zao za giza.
Mbona Neno la MUNGU liko wazi sana juu ya Wewe uliokoka ukajitanbua na ukawa unaomba lazima ushinde.
Maandiko haya yanakupa uhakika ambao hauwezi kupingwa na Nguvu za giza zozote.
Mathayo 21:22 "Na yo yote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea."
Isaya 54:14 "Utathibitika katika haki; utakuwa mbali na kuonewa, kwa maana hutaogopa; na mbali na hofu, kwa maana haitakukaribia."
Mathayo 17:20" YESU akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; WALA HALITAKUWAKO NENO LISILOWEZEKANA KWENU."
Isaya 43:11 "Mimi, naam, mimi, ni BWANA, zaidi yangu mimi hapana mwokozi."
◼️Ndugu Jifunze kuomba Tena omba kwa Imani utashinda dhidi ya Kila Nguvu za giza.
Asante kwa kujifunza Neno la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments