![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe Ndugu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
◼️Tunafahamu Waliookoka wote YESU KRISTO aliwaita kwa ajili ya uzima wa Milele.
Yohana 10:28 "Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu."
◼️Uzima Wa Milele ni mwito wa Kila aliyeitwa na YESU KRISTO Kwa ajili ya Wokovu.
➡️Ukiitwa na YESU Usikubali kitu chochote kikukwamishe kumpokea yeye YESU KRISTO aliyekuita.
Mathayo 8:22 "Lakini YESU akamwambia, Nifuate; waache wafu wazike wafu wao."
◼️Kabla ya kuishi katika mwito huu wa YESU inakupasa ujikane.
Mathayo 16:24 "Wakati huo YESU aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate."
◼️Lakini pamoja na uzima wa milele Kuna baadhi ya watu Bwana YESU amewaita kwa ajili ya mambo mengine zaidi.
1. Kuna watu wameitwa ili wawe Wahubiri wa Injili.
Mathayo 4:19 "Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu."
◼️Uliyeitwa katika wito huu ndani ya YESU inakupasa kutimiza wito wako.
2. Kuna watu wameitwa na YESU KRISTO Kwa ajili ya utumishi mbalimbali katika Kanisa na huduma na kazi za Injili.
Yohana 12:26 "Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, BABA atamheshimu."
3. Kuna watu wameitwa na YESU ili waurithi tu uzima wa milele kwa kutii kwao katika wakati wao wa Mwisho Duniani, watu hawa kama wakiamua kumfuata katika wakati wao wa Mwisho Duniani wanapata Neema yake kwa ajili ya uzima wa milele.
◼️Mfano hai ni mfungwa Msalabani, Bwana YESU angetaka angemponya na kumpa kutumika katika Injili lakini katika kumwokoa Bwana YESU alimhakikishia uzima wa milele masaa machache baadae na ikawa hivo, hivyo mfungwa yule muda wake Duniani ulikuwa umeisha.
Luka 23:42-43 " Kisha akasema, Ee YESU, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako. YESU akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi."
➡️Na Maombi ya mfungwa huyu hayakuwa kupona au kutoka katika kifungo ila Maombi yake yalikuwa kwenda uzima wa milele na ikawa hivyo.
◼️Kuna watu hupata Neema ya kumpokea YESU KRISTO katika wakati wao wa Mwisho Kisha wanaenda paradiso wakiwa tayari kwa uzima wa milele.
Yohana 8:12 "Basi YESU akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima."
➡️Kuna watu anaokoka na masaa machache au siku chache anafariki, huyu aliitwa tu kupata uzima wa milele ndio maana hajapewa muda wa kuhubiri Injili, kuongoza watu n.k
Hivyo katika Kanisa inapotokea hivyo tumwelewe MUNGU maana mwito namba Moja wa KRISTO kwa watu wote ni uzima wa Milele, Kuna Mtu anaweza akamkubali YESU na muda wake wa kuishi Duniani ukawa umeisha hivyo, huyo aliitwa akakubali kwa ajili ya uzima wa milele, ni jambo zuri sana.
◼️Wito huu ni wito wa MUNGU kwa ajili ya Watu wote lakini ni watu wachache ambao huupokea.
Tuliwahi siku Moja Mimi na Mke wangu na baadhi ya Waumini wenzetu Kanisani kutembelea Hospital ya Wagonjwa wa kansa kwa sababu kuna mwenzetu mmoja wa Kanisani kulikuwa na ndugu yake amelazwa hapo, katika wodi Moja tulikuta wagonjwa kama 5 au 6 au 7 sikumbuki vizuri idadi yao lakini nikawiwa moyoni mwangu kuwaambia kwa habari ya kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wao, ni mmoja tu aliyekubali, wengine walimhitaji YESU kwa ajili ya uponyaji tu ila hawakumhitaji YESU kwa ajili ya uzima wa milele.
Tuliwasihi kwa habari ya Kuokoka lakini hawakuhitaji ingawa walihitaji sana tuwaombee uponyaji, sisi tukawaombea Kisha tukaondoka, ndani ya siku 2 baada ya hapo yule mwenzetu akarudi kule hospital kwa sababu Ndugu yake yule alifariki kwa sababu ya kansa, katika kutembelea wodi akafika ile wodi tuliyokuwepo siku 2 kabla na kukuta wagonjwa wapya, akamuuliza muuguzi akaambiwa wote walifariki ndani ya siku 2 zile, yule Ndugu akanipigia simu kunieleza.
Niliogopa sana na kuwaza sana, kumbe Inawezekana sisi tulikuwa watu wa mwisho kwao kuitangaza Neema ya Wokovu kwao ila wengi kati yao hawakuipokea ingawa walikuwa dakika za mwisho za kuishi kwako.
Wangempokea YESU KRISTO ingekuwa heri kwao.
➡️Hapo ndipo tunakumbuka Kondoo wa MUNGU huisikia Sauti ya YESU na kumfuata.
Yohana 10:27 "Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata."
◼️Ndugu Kuna watu huitwa na YESU KRISTO Kwa ajili ya uzima wa milele, ndio maana Biblia siku zote inasema Mtu akiisikia Sauti yake asiufanye Moyo wake kuwa mgumu.
Waebrania 3:15 "hapo inenwapo, Leo, kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha."
5. Baada ya hapo wapo watu wameitwa ili wapate mara mia Sasa Kisha uzima wa milele.
Mathayo 19:29 "Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele."
◼️Wito huu wa kupata mara mia Sasa Kisha uzima wa milele ni wito wa wote ila wanaozingatia ni Kanuni za ki MUNGU za kupata mara mia Sasa ni wachache.
➡️Ndani ya wito huu wa kupata mara mia Sasa Kisha uzima wa milele unaweza ukapata mengi baadhi ni haya chini kama ukizingatia kanuni za ki MUNGU.
Marko 10:29-30 " YESU akasema, Amin, nawaambieni, Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili, ila atapewa mara mia sasa wakati huu, nyumba, na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele."
Hapa tunaona hiyo mara mia sasa ambayo Mtu anaweza kuipata kwa sababu amekubali kuokolewa na Bwana YESU KRISTO ni pamoja na
✔️✔️Kupata nyumba yake yaani kuwezeshwa na MUNGU kujenga nyumba ya kuishi au kuanzisha familia yake.
✔️✔️Kupata marafiki wapya wazuri wanaompenda MUNGU.
✔️✔️Kupata Ndoa.
✔️✔️Kupata uzao yaani kupewa Neema ya kuzaa Watoto wa kiume au wa kike hata kama alikuwa tasa.
✔️✔️Kupata Mali mfano Mashamba n.k
Ni Muhimu sana kwa kila Mtu kuupokea wito wa Kuokoka.
Asante kwa kujifunza Neno la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments