MAOMBI YA LEO YA UFUNUO.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 


Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki yangu.

◼️Siku Moja Nilipata ufunuo kutokea Isaya 40:28- 31 na nikaomba muda mrefu sana na nilimuona MUNGU wa Miujiza.

Maandiko hayo yanasema  hivi 
"Isaya 40:28-31 " Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye MUNGU wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.  Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo.
 Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka; bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia."

◼️Nakuletea ufunuo huo huo ili na wewe uombe katika jina la YESU KRISTO na utashinda.

➡️Kabla ya kuomba hakikisha unatafakari maandiko hayo katika ROHO na utapata nguvu mpya za kuomba, kwangu ilitokea hivyo.

Leo omba hivi;

1. Mwambie MUNGU kwamba unamngoja;

➡️Unamngoja katika uponyaji.

 ➡️Unamngoja katika uzao.

 ➡️Unamngoja katika baraka.

➡️ Unamngoja katika ndoa n.k kulingana na hitaji lako.

2. Futa kila kitu cha kipepo kilichokaa ndani ya nafsi yako, futa kumbukumbu mbaya rohoni mwako na futa kifungo cha uovu kwako.

3. Tumia damu ya YESU KRISTO ikapeleleze kwenye ardhi ulikofungwa, kwenye anga la kipepo ulikofungwa, kwenye bahari na popote ulikoshikiliwa kipepo, ili maagano ya Giza yafutike na ubaki huru ukingoja baraka za MUNGU.

4. Futa roho za vitisho, na mwambie Bwana YESU unamngoja kwa hatua nyingine ya ushindi wako.

◼️Nilipofunuliwa niliandika na Leo nimepata msukumo rohoni kukujulisha hivyo kama ni muombaji fanyia kazi na utamuona MUNGU aliyeziumba mbingu na dunia.

✔️✔️Ng'ang'ania Isaya 40:31 ukimwambia MUNGU kwamba unamngoja ili akutendee muujiza, mtajie kila hitaji lako ambalo unamngoja JEHOVAH aliye hai ili akutendee, na yamkini mwakani au hata mwaka huu huu ukaona ushindi mkuu katika hitaji lako.

✔️✔️Unaweza ukapata kazi kiajabu sana ukiomba na Kisha ukatafuta kazi.

✔️✔️Unaweza ukapata mchumba sahihi kiajabu sana.

✔️✔️Unaweza ukashinda kesi kiajabu sana.

✔️✔️Unaweza ukapona kila ugonjwa kiajabu sana.

◼️Muhimu tu Mwamini MUNGU kwamba anaweza yote(Yeremia 10:6)

◼️Mwamini Bwana YESU maana ni katika yeye tu ndio unaweza kushinda(Luka 10:19)

◼️Mwamini ROHO MTAKATIFU maana ndiye pekee mwalimu wa kweli akilitumia Neno la MUNGU kukusaidia(Yohana 16:13)

◼️Muhimu tu hakikisha YESU KRISTO ni Mwokozi wako na Hakikisha unaishi maisha matakatifu ya haki katika yeye( 1 Petro 1:15)
MUNGU wangu akubariki sana na kukutendea mema.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU Mwenyezi.
+255714252292.
Ubarikiwe sana na nasubiri.
 Ushuhuda za waliokusudiwa na mbingu, najua na wewe ni mmoja wao.
Amen Amen kwa YESU KRISTO Mwokozi wa milele.

Comments