NA ZAKA YOTE NIMEWAPA WALAWI.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu zangu wote.

Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.


Hesabu 18:21 "Na wana wa Lawi, nimewapa zaka yote katika Israeli kuwa urithi wao, badala ya huo utumishi wautumikao, maana, ni huo utumishi wa hema ya kukutania."


◼️Agizo hili la Zaka ni la MUNGU kwamba Walawi kwa sababu ya Utumishi wao wa Madhabahuni basi wapewe.


➡️Walawi hao ndio Wachungaji leo ambao Wanamtumikia  MUNGU kwa uaminifu katika KRISTO YESU.


Waebrania 7:5-6 " Na katika wana wa Lawi nao, wale waupatao ukuhani, wana amri kutwaa sehemu ya kumi kwa watu wao, yaani, ndugu zao, kwa agizo la sheria, ijapokuwa wametoka katika viuno vya Ibrahimu. Bali yeye, ambaye uzazi wake haukuhesabiwa kuwa umetoka kwa hao, alitwaa sehemu ya kumi kwa Ibrahimu, akambariki yeye aliye na ile ahadi."


➡️Najua jambo hili huwaumiza sana baadhi ya watu lakini ukweli wa Neno la MUNGU hubaki pale pale daima.


◼️Na kwa habari ya Zaka Mwanzo MUNGU alisema ni ya kwake hivyo anaposema amewapa makuhani naomba ieleweke kwamba sio watu wamewapa ila ni MUNGU.


Walawi 27:30 "Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya BWANA; ni takatifu kwa BWANA."


➡️Hivyo usitoe Zaka ukisema "Nampa Mtumishi " Bali toa ukimpa MUNGU ingawa anayepokea ni Mtumishi na anayeitumia ni huyo Mtumishi ila baraka zinazotokana na utoaji huo anakubariki MUNGU maana umemtolea yeye.


➡️Watu wengi hudhani baraka za MUNGU baada ya kutoa ni kupata tu pesa nyingi, baraka za MUNGU zipo za aina nyingi.


◼️Kuna Mtu anamtolea MUNGU Zaka na kwa kipindi kirefu sana hatatumia pesa yake kujitibu maana MUNGU atamlinda dhidi ya magonjwa.


➡️Lakini Yuko Mtu anazuia Zaka kwa Siri  mfano alitakiwa atoe elfu 70 hataki kutoa lakini ndani miezi 4 anatumia laki 6 kujitibu au kutibu familia yake, kumbe alichokosa ni baraka ya MUNGU ya utoaji Zaka.


◾Yuko Mtu alisikia moyoni mwake kutoa Zaka lakini akadhani atawafaidisha Watumishi kilichofuata duka lake likaibiwa ghafla maana ulinzi wa MUNGU uliondoka kwenye kazi ya Mikono yake kwa sababu hakuwa mwaminifu kwa MUNGU kwenye fungu la kumi.


◼️MUNGU katika Neno lake ametoa maelekezo ya utoaji wa Zaka na Sadaka.


◼️Maelekezo mengine yanawahusu Watoaji na maelekezo mengine yanawahusu wapokeaji.


➡️Kwa wapokeaji yaani Wachungaji ukisoma Kumbu 14:28-29  katika Tafasiri ya BHN Unaona Zaka ni kwa ajili ya Walawi lakini mbele yake Biblia inasema Yatima, Wajane na wageni nao wanatakiwa kushiba hivyo Mpokeaji wa Zaka ambaye ni Mchungaji Kumbuka kuwagawia Yatima na Wajane na wahitaji.


Kumbu 14:28-29 "Na kila mwisho wa mwaka wa tatu toeni zaka ya mazao yenu yote na kuyaweka akiba katika miji yenu.

Hiyo itakuwa kwa ajili ya Walawi, kwa kuwa hawana fungu wala urithi wao kati yenu, nao wageni, yatima na wajane ambao wanaishi katika miji yenu, watakuja kula na kushiba. Fanyeni hivi naye Mwenyezi-MUNGU, MUNGU wenu, awabariki katika kazi zenu zote mfanyazo kwa mikono yenu."


➡️Changamoto Leo watoaji ni Wachache sana na hutoa kidogo sana hivyo hata huyo kuhani haiwezi hata familia yake kupata Chakula hata Cha wiki moja tu.


➡️Mchungaji unapopewa Zaka nyingi usijikimbikizie Mali za Zaka Bali wakumbuke sana Yatima na Wajane maana ndio mapenzi ya MUNGU.


➡️Leo kwa aji ya chuki za Waumini kwa Wachungaji wao hutoa Zaka kwa Yatima na Wajane na Zaka hiyo hugeuka Msaada na sio Zaka, na MUNGU habariki Msada Bali Zaka, Sadaka na dhabihu.


Ni vizuri sana tukafuata Neno la MUNGU linataka Nini?


◼️MUNGU hawezi kusema Zaka yote nimewapa Walawi Kisha Wewe Zaka upelekee Yatima, Yatima wapelekee Sadaka na utakuwa umefanya vyema sana na MUNGU atakubariki, lakini kwa habari ya Zaka au kwa Jina lingine fungu la kumi mpe Mchungaji wako anayekulisha Neno la MUNGU Kila siku, au mpe Mtumishi mwaminifu wa KRISTO ambaye ROHO MTAKATIFU atakuelekeza.


Neno la MUNGU linataka Nini?


◼️Hata kwa baadhi ya Sadaka sio Sadaka zote anapewa Mchungaji.


➡️Ukisoma Biblia vizuri unagundua kwa habari ya sadaka ni baadhi tu ya Sadaka wameruhusiwa kupewa Wachungaji ila sio Sadaka zote.


Hesabu 18:19 "Sadaka zote za kuinuliwa za vitu vitakatifu, wana wa Israeli wavisongezavyo kwa BWANA, nimekupa wewe na wanao na binti zako pamoja nawe, ni haki yenu ya milele; ni agano la chumvi la milele mbele za Bwana kwa ajili yako, na kizazi chako pamoja nawe."


◼️Ndugu, jilinde usije ukamwacha Mlawi yaani Mchungaji wako anayekufundisha Neno la MUNGU Kila siku na kukuombea.


Kumbu  12:19 "Jilinde nafsi yako usimwache Mlawi siku zote uishizo katika nchi yako."


➡️Mtu mmoja aliniandikia hivi "Mtumishi Mabula Mimi sitatoa Fungu la kumi kwa Mtumishi yeyote ila nitatoa kwa Yatima" 


Nikamwambia nionyeshe andiko linaloonyesha Mtu hata mmoja alitoa Zaka kwa Yatima nami nitakuonyesha maandiko mengi  Zaka akipewa kuhani.


Alitafuta akakosa.


◼️Ndugu, njia mojawapo ya Wewe kumwacha MUNGU nj kufanya dhambi na kuacha kumtolea MUNGU.


➡️Na njia mojawapo ya kumwacha Mchungaji wako na kujitenga naye ni kuacha kumuombea na kuacha kutoa Zaka, huwa Kuna ushirika kutoka kwenye utoaji, hata MUNGU anaweza akazungumza kwa sababu ya utoaji huu.


➡️nakupa Siri hii ambayo Mimi nimejifunza na kuthibitisha.

Ukitaka hata Mchungaji wako asipate Ufunuo wa ki MUNGU kuhusu Wewe basi Acha kumtolea MUNGU Zaka na Sadaka anayokuelekeza ROHO MTAKATIFU.


◼️Tangu Zamani utaratibu wa kutoa Zaka kwa Watumishi wa MUNGU ulikuwepo.


Nehemia 12:44 "Na siku hiyo watu wakaagizwa juu ya vyumba vya hazina, kwa sadaka za kuinuliwa, na kwa malimbuko, na kwa zaka, ili kuzikusanya, kwa kadiri ya mashamba ya miji, sehemu zilizoamriwa katika torati za makuhani, na Walawi; kwa maana Yuda waliwafurahia makuhani na Walawi waliotumika."


◼️Ni Muhimu sana kuwa mwaminifu katika kutoa Zaka kwa MUNGU kupitia kwa Watumishi wake waaminifu katika KRISTO YESU Mwokozi.


➡️Kazi ya utumishi wa kweli  ni ngumu sana hivyo usiwaonee wivu wanapopokea Zaka za MUNGU, ni MUNGU wa Mbinguni aliwapa hiyo Zaka.


Nehemia 10:37-38 " tena tuyalete malimbuko ya unga wetu, na sadaka zetu za kuinuliwa, na matunda ya miti ya namna zote, mvinyo, na mafuta, kwa makuhani, hapo vyumbani kwa nyumba ya MUNGU wetu; na zaka za ardhi yetu kwa Walawi; kwa kuwa hao Walawi wazitwaa zaka mijini mwote mwa kulima kwetu. Naye kuhani, mwana wa Haruni, atakuwako pamoja na Walawi, watwaapo zaka Walawi; nao Walawi wataipandisha zaka ya hizo zaka nyumbani kwa MUNGU wetu, vyumbani, katika nyumba ya hazina."


◼️Usiache kutoa Zaka na zingatia sehemu sahihi ya kutoa.

Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.

MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

By Mwl Peter Mabula 

Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)

Ubarikiwe

Comments