NENO LOLOTE ATAKALOKUAMBIA MUNGU LIFANYE BILA KULIONGEZA WALA KULIPUNGUZA.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki yangu.

Karibu tujifunze Neno la MUNGU.


◼️Neno lolote atakalokuambia MUNGU wa Mbinguni lifanye bila kuliongeza Wala kulipunguza.


Kumbu 12:32 "Neno niwaagizalo lo lote liangalieni kulifanya; usiliongeze, wala usilipunguze."


◼️Neno lolote atakalokuambia MUNGU wa Mbinguni lifanye bila kuliongeza Wala kulipunguza.


◾Kwanini Biblia inasema hivyo?


◼️Watu wengi hujikuta kwenye madhara, adhabu, kukataliwa,na kupigwa na MUNGU Kwa sababu ya kuongeza alilowaambia MUNGU au kupunguza alilowaambia MUNGU.


Mifano hai ni hii


➡️Sauli alipunguza kile alichoambiwa na MUNGU, aliwaambiwa awaue Waamaleki na vitu vyao asichukue chochote.


1 Samweli 15:2-3 " BWANA wa majeshi asema hivi, Nimeyatia moyoni mwangu mambo hayo Amaleki waliyowatenda Israeli, jinsi walivyowapinga njiani, hapo walipopanda kutoka Misri. Basi sasa enda ukawapige Amaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyo navyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, mtoto naye anyonyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda."


◾Kwanini aliambiwa awaue Waamaleki?


➡️Biblia imesema sababu ni  kwamba kilikuwa ni kisasi Cha MUNGU kwa sababu Amaleki waliwapinga Israeli wakati wakitoka Misri, maana yake Amaleki walimpinga MUNGU aliyekuwa anawatoa Waisraeli Misri, kisasi kikawa kinawahusu wakati huu wa Sauli ila Sauli akashindwa kufanya kusudi la MUNGU Kwa tamaa.


➡️Sababu nyingine ya kufanya hivyo ni ili kuufuta ukumbusho wa Amaleki kama MUNGU alivyomwambia Musa.


Kutoka 17:14" BWANA akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu."


➡️Sababu nyingine Waamaleki walipigana na Israel wakati wakitoka Misri.


➡️Sababu nyingine Waamaleki walikuwa watu wa dhambi na Wauaji hivyo MUNGU alitaka kuwaondoa wote ili dhambi yao isiendelee.


1 Samweli 15:32-33 " Ndipo Samweli akasema, Nileteeni hapa Agagi, mfalme wa Waamaleki. Basi Agagi akamwendea kwa utepetevu. Naye Agagi akasema, Bila shaka uchungu wa mauti umeondoka.

 Lakini Samweli akamjibu, Kama upanga wako ulivyofanya wanawake kufiwa na watoto wao, vivyo hivyo mama yako atafiwa miongoni mwa wanawake. Basi Samweli akamkata Agagi vipande mbele za BWANA huko Gilgali."


◼️Sauli akapunguza alichoambiwa, hakufanya kama alivyoambiwa.


1 Samweli 15:11 "Najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe mfalme; maana amerudi nyuma, asinifuate, wala hakufanya nilivyomwamuru. Samweli akasikitika, akamlilia BWANA usiku kucha."


◼️Kwa kosa hilo Sauli akafanya machukizo kwa MUNGU.


1 Samweli 15:18-19 " Kisha BWANA akakutuma safarini, akasema, Enenda ukawaangamize kabisa wale Waamaleki wenye dhambi, upigane nao hata watakapoangamia. Mbona, basi, hukuitii sauti ya BWANA, bali ukazirukia nyara ukafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana?"


➡️Sauli alitii Sauti ya Wanadamu na sio ya MUNGU aliyesema naye Mwanzo.


1 Samweli 15:24 "Ndipo Sauli akamwambia Samweli, Nimefanya dhambi; maana nimeihalifu amri ya BWANA, pia na maneno yako; kwa sababu naliwaogopa wale watu, nikaitii sauti yao."


◼️Adhabu aliyoipata Sauli  kwa kupunguza maelekezo ya MUNGU ni kuondolewa kwenye Ufalme.


1 Samweli 15:26 "Samweli akasema, Sitarudi pamoja nawe; kwa sababu umelikataa neno la BWANA, BWANA naye amekukataa wewe, usiwe mfalme wa Israeli."


➡️Ufalme akapewa Daudi kwa makosa ya Sauli.


1 Samweli 15:28 "Basi Samweli akamwambia, Leo BWANA amekurarulia ufalme wa Israeli, naye amempa jirani yako, aliye mwema kuliko wewe."


◼️Huyu Sauli kosa lake alipunguza maelekezo aliyoambiwa na MUNGU.


✔️✔️Ndugu usipunguze maelekezo ya ROHO MTAKATIFU kwenye Maisha Yako maana hayo ni maelekezo ya MUNGU wa Mbinguni.


Mfano wa pili.


Nabii Kijana aliambiwa na MUNGU asiye Chakula Cha watu fulani Wala kunywa maji yao Wala kurudi kwa njia ile aliyotumia kwenda baada ya kusema ujumbe wa MUNGU.


1 Wafalme 13:8-9 " Mtu wa MUNGU akamwambia mfalme, Ujaponipa nusu ya nyumba yako, sitaingia pamoja nawe, wala sitakula chakula, wala sitakunywa maji mahali hapa; maana ndivyo nilivyoagizwa kwa neno la BWANA, kusema, Usile chakula cho chote wala usinywe maji, wala usirudi kwa njia ile uliyoijia."


➡️Nabii huyu baada ya MUNGU kumpa Maelekezo yeye akakubali kudanganywa na Nabii mzee.


➡️Nabii Kijana akajikuta ametoka  nje na yale aliyoambiwa na MUNGU.


1 Wafalme 13:18 "Akamwambia, Mimi nami ni nabii kama wewe, na malaika akaniambia kwa neno la BWANA, kusema, Mrudishe pamoja nawe nyumbani kwako, ale chakula, akanywe maji. Lakini alisema uongo."


◼️Huyu Nabii Kijana hakumwamini MUNGU aliyesema naye, yeye akawaamini Wanadamu ikapelekea kifo chake.


◼️Aliongeza nje ya yale aliyoambiwa  na MUNGU.


➡️Mimi sijui MUNGU kupitia ROHO MTAKATIFU amekuambia Nini, Alikuambia Nini.

Ndugu Fanya tu kile alichokuambia MUNGU maana MUNGU sio Mwanadamu hata aseme uongo.


Hesabu 23:19" MUNGU si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?"


◼️Ndugu, ni maelekezo gani Bwana YESU KRISTO amewahi kukupa?

Nakuomba Fanya kama alivyokuambia usipunguze Wala kuongeza.


➡️Inawezekana taratibu za dhehebu lenu zinakataa baadhi ya maandiko, Ndugu usifuate dhehebu kama liko kinyume na MUNGU wa Mbinguni.


➡️Leo Kuna watu wanamkataa hadi  ROHO MTAKATIFU ndio maana hafanyi kazi kwao.


◼️Ndugu, usiliongeze Wala kulipunguza Neno la MUNGU aliye hai.


◼️Ndugu, usiliongeze Neno la MUNGU ili liseme kinyume na MUNGU maana haiwezekani na utachukua hatia mbaya.


Ufunuo 22:18 "Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki."


◼️ROHO MTAKATIFU alikupa kuonya Hakikisha unaonya.


◼️ROHO MTAKATIFU akikupa kukemea Hakikisha unakemea, usiongeze Wala kupunguza.


Asante kwa kujifunza Neno la  siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.

MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

By Mwl Peter Mabula 

Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)

Ubarikiwe

Comments