![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
Waebrania 3:14 "Kwa maana tumekuwa washirika wa KRISTO, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho;"
◼️Neno "Kushikamana" lina maana 2.
➡️Kushikamana ni kuambatana.
➡️ Kushikamana ni kuwa na msimamo na ushirikiano ili kutimiza Lengo.
Sasa kutoka Neno Kushikamana tuangalie Kushikamana na KRISTO Mwokozi.
◼️Kushikamana na YESU KRISTO ni kuambatana naye siku zote.
Kumbu 13:4 "Tembeeni kwa kumfuata BWANA, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye."
◼️Kushikamana na YESU KRISTO ni kuwa na msimamo na ushirikiano ili kutimiza kusudi la MUNGU la Wokovu.
Kumbu 30:20 "kumpenda BWANA, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako, na wingi wa siku zako; upate kukaa katika nchi BWANA aliyowaapia baba zako, Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kuwa atawapa."
◼️Kushikamana na YESU KRISTO ndio pia Kushikamana na MUNGU Mwenyezi.
➡️Ni jambo zuri sana na lenye Faida sana Kushikamana na MUNGU katika KRISTO YESU siku zote za Maisha Yako.
◼️Ambatana na KRISTO YESU siku zote za kuishi kwako.
◼️Shirikiana rohoni na ROHO MTAKATIFU siku zote.
➡️Baki na msimamo wa Wokovu wa KRISTO siku zote za Maisha Yako.
◾Kwanini nimesema Kushikamana na YESU KRISTO?
➡️Ni kwa sababu sehemu kubwa ya Wanadamu wameshikamana na shetani.
➡️Sehemu kubwa ya watu wameshikamana na uovu.
➡️Watu wengi hushikamana na watu walio kinyume na MUNGU, Ndugu usiwe Wewe.
➡️Mfano ni hawa watu walioshikamana na Kora kwenda kinyume na Mtumishi wa MUNGU Musa wakafa.
Hesabu 16:32 ''nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza, na watu wa nyumba zao na wote walioshikamana na Kora, na vyombo vyao vyote."
➡️Kuna watu wameshikamana na Dhambi za watangulizi wao, Ndugu usiwe Wewe.
➡️Mfano ni huyu kiongozi wa Nchi aliyefuata dhambi za mtangulizi wake.
2 Wafalme 3:3 "Pamoja na hayo alishikamana na dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo kwa hizo aliwakosesha Israeli; wala hakuziacha."
➡️Kuna watu wameshikamana na miungu ndio maana hawamtaki YESU KRISTO, Ndugu usiwe Wewe.
2 Nyakati 7:22 "Nao watajibu, Kwa sababu walimwacha BWANA, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka nchi ya Misri, wakashikamana na miungu mingine, wakaiabudu, na kuitumikia; kwa hiyo ameyaleta mabaya haya yote juu yao."
◼️Ndugu, nakuomba kwa Neno la MUNGU shikamana na MUNGU katika KRISTO YESU siku zote za Maisha Yako.
Kumbu 11:22 "Kwa kuwa kwamba mtayashika kwa bidii maagizo haya yote niwaagizayo, kuyafanya; kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kutembea katika njia zake zote, na kushikamana naye;"
◼️Ndugu, Hakikisha siku zote unatembea kwa kumfuata YESU KRISTO siku zote.
Kumbu 13:4" Tembeeni kwa kumfuata BWANA, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye."
◼️Ndugu, shikamana na Injili ya KRISTO YESU siku zote za Maisha Yako.
◼️Ndugu, shikamana na Neno la MUNGU siku zote za Maisha Yako.
◼️Ndugu, shikamana na mambo mema ya KRISTO utaitwa heri daima.
Asante kwa kujifunza Neno la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments