KUNA MAMBO YANAKUSUBIRI UONE KWANZA NDIPO USHINDI WAKO UANZE KUTOKEA.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU 

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.

Karibu Tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.


◼️Kuna mambo yanakusubiri Uone kwanza ndipo yaanze kutendeka.


➡️Mfano ni Musa alipoona kwanza ndipo utumishi wake mkubwa ukaanzia hapo.


Kutoka 3:4 "BWANA alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, MUNGU akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema, Musa! Musa! Akasema, Mimi hapa."


◼️Musa alipoona ndipo Sauti ya MUNGU ilimwita na huo ndio ukawa mwanzo wa utumishi wake mkubwa Sana.


◼️Musa alipoona ndipo ikawa mwanzo wa huduma yake kubwa na ushindi wa ki MUNGU uliotikisa falme na Mamlaka.


◼️Ni Kusudi la MUNGU Uone.


Isaya 42:18 "Sikilizeni, enyi viziwi; tazameni, enyi vipofu, mpate kuona."


➡️Ndugu, Kuna Nguvu ya ushindi na mabadiliko kwenye kuona.


1 Samweli 17:51 "Ndipo Daudi akapiga mbio, akasimama juu ya Mfilisti, akautwaa upanga wake, akaufuta alani mwake, akamwua, akamkata kichwa kwa upanga huo. NAO WAFILISTI WALIPOONA YA KUWA SHUJAA WAO AMEKUFA, WAKAKIMBIA."


◼️Wafilisti walipoona Goliath amepigwa walikimbia wote na huo ndio ukawa ushindi kwa Daudi na Israeli.


◼️Hata adui yako unaweza ukamuombea aone Nguvu za MUNGU kupitia Wewe, akiona atakukimbia na kukuogopa.


✔️✔️Kuna Nguvu kubwa katika kuona ndio maana Kuna mambo yabasubiri Uone kwanza ndipo yaanze kutendeka kwako.


◼️Hata katika kuhubiri kwetu inatakiwa tuombe ili watu waone Matendo YESU KRISTO ili wamfuate maana Kuna Nguvu kubwa katika kuona.


Luka 18:43 "Mara hiyo akapata kuona, akamfuata, huku akimtukuza MUNGU. Na watu wote walipoona hayo walimsifu MUNGU."


◾Kwanini Uone kwanza?


1. Ukiona utatiwa Moyo na utainua njia ya ushindi wako hivyo hata vikija vikwazo hutaogopa.


2 Wafalme 6:17 "Elisha akaomba, akasema, Ee BWANA, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. BWANA akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote."


◼️Huyu alikuwa anaogopa ila alipoona ulinzi wa MUNGU juu yao alitiwa Moyo na hakuwaogopa maadui zao.


2. Ukiona utachukua hatua za kimaombi au hatua za matengenezo ili utembee kwenye kusudi la MUNGU.


➡️Mfano Kuna watu wako katika vifungo vya giza na magereza ya kiroho   na hawajui kwa sababu hawajaona.


Isaya 42:7 "kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa."


◼️Ukifanikiwa kuona ukaomba katika Jina la YESU KRISTO unatoka kwenye kifungo hicho.


Isaya 35:5 "Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa, na masikio ya viziwi yatazibuliwa."



3. Ukiona utapanga uamue Nini.


Mwanzo 48:17-19 " Yusufu alipoona kwamba babaye anaweka mkono wake wa kuume juu ya kichwa cha Efraimu, ikawa vibaya machoni pake. Akauinua mkono wa babaye auondoe katika kichwa cha Efraimu, ili auweke juu ya kichwa cha Manase. Yusufu akamwambia babaye, Sivyo, babangu, maana huyu ni mzaliwa wa kwanza; weka mkono wako wa kuume kichwani pake. Babaye akakataa, akasema, Najua, mwanangu najua, yeye naye atakuwa taifa, yeye naye atakuwa mkuu; lakini ndugu yake mdogo atakuwa mkubwa kuliko yeye, na uzao wake watakuwa wingi wa mataifa."


◼️Yakobo baada ya kuona kwenye ulimwengu wa roho aliamua vyema katika ulimwengu wa Mwili kama kusudi la MUNGU Kwa Watoto wa Yusufu lilivyo.


4. Ukiona utalijua kusudi la MUNGU.


Luka 8:34 "Wachungaji walipoona lililotokea walikimbia, wakaieneza habari mjini na mashambani."


◼️Wachungaji walipoona walienda kuhubiri Injili yaani habari njema za YESU KRISTO.



Nini ufanye?


1. Tubia dhambi, maovu na makosa Yako.


Isaya 59:1-2 " Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na MUNGU wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia."


2. Ukifanikiwa kuona ushindi wako katika ulimwengu wa roho mtukuze MUNGU.


Matendo  27:23-25 " Kwa maana usiku huu wa leo malaika wa MUNGU yule ambaye mimi ni wake, naye ndiye nimwabuduye, alisimama karibu nami, akaniambia, Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena, tazama, MUNGU amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe. Basi, wanaume, changamkeni; kwa sababu namwamini MUNGU, ya kwamba yatakuwa vile vile kama nilivyoambiwa.



3. Omba MUNGU akupe kuona baraka zako ili uziendee kiroho hadi uzipate.



Luka 18:42-43 " YESU akamwambia, Upewe kuona; imani yako imekuponya. Mara hiyo akapata kuona, akamfuata, huku akimtukuza MUNGU. Na watu wote walipoona hayo walimsifu MUNGU."



4. Kataa kuona yasiyo ya MUNGU.

 

2 Wakorintho 2:11 ''Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake."


5. Omba ROHO MTAKATIFU akuongoze kwenye ushindi baada ya kuona.


Yohana 16:13 "Lakini yeye atakapokuja, huyo ROHO wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake."

Asante kwa kujifunza Neno la  siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.

MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

By Mwl Peter Mabula 

Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)

Ubarikiwe

Comments