KUNA PUNDA ALIPATA HESHIMA.

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 




Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe.

Karibu tujifunze ujumbe huu mfupi.

Unamkumbuka yule Punda aliyembeba Bwana YESU KRISTO?.

◼️Punda yule alipita  hadi sehemu  asiyotakiwa kwa sababu tu  alikuwa amembeba  Bwana YESU.


◼️Punda alipita kwenye barabara ambayo imetandikwa nguo nzuri za thamani kwa sababu tu punda alikuwa amembeba   Bwana YESU KRISTO.


Mathayo 21:6-9 " Wale wanafunzi wakaenda zao, wakafanya kama YESU alivyowaamuru, wakamleta yule punda na mwana-punda, wakaweka nguo zao juu yao, naye akaketi juu yake. Watu wengi katika ule mkutano wakatandaza nguo zao njiani; na wengine wakakata matawi ya miti, wakayatandaza njiani. Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la BWANA; Hosana juu mbinguni.


◼️Punda alipata heshima ya kupita juu ya nguo nzuri kwa sababu tu alikuwa amembeba Bwana YESU KRISTO Mwokozi.


➡️Nini nataka kusema?


◼️Wewe ukimbeba Bwana YESU moyoni Mwako unaweza ukapita hata kwenye ngome  za wachawi lakini  hawatakufanya lolote kwa sababu umembeba YESU KRISTO  asiyeshindwa.


◼️Ndugu kama  ukimbeba YESU KRISTO moyoni mwako  unaweza kuishi hata sehemu  ambazo wengine wanasema  Mwanadamu  Fulani  hawezi kuishi eneo hilo kwa  sababu  eneo hilo  ni  makao  ya  nguvu za giza.


 ◼️Ndugu, mbebe  Bwana YESU KRISTO katika Maisha Yako  utapita kila sehemu na nguvu za giza hazitakugusa.


➡️Unambebaje Bwana YESU?


◼️Unambeba Bwana YESU KRISTO Kwa kumpokea kama Mwokozi wako Kisha ukafuata maelekezo yake.


Yohana 1:12-13 " Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU."


Tena ukimpokea Bwana YESU KRISTO yeye na Baba yake watakuja kwako na kufanya makazi hivyo utapata heshima kama aliyoipata yule Punda na zaidi.


Yohana 14:23 "YESU akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na BABA yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake."


Ndugu, ni wakati wako wa kupata heshima na kuogopekwa kwa mawakala wa shetani kwa sababu una Bwana YESU KRISTO kama Mwokozi wako.

Nakuomba Mpokee Bwana YESU KRISTO kama Mwokozi wako na ataanza kuwa kwako hivyo utashinda na zaidi na kushinda na utapata heshima maana uko na yeye Mwokozi mwenye Nguvu na heshima.

MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

By Mwl Peter Mabula 

Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU Mwenyezi.

Amen.

Comments