KUNA WATU WAMEWEKWA KUWA WAKUU.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 


Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki yangu.

Karibu sana Tujifunze Neno la MUNGU.


◼️Kuna Watu wamewekwa na MUNGU kuwa Wakuu.


Mfano ni huu


1  Nyakati 2:10 "Na Ramu akamzaa Aminadabu; na Aminadabu akamzaa Nashoni, mkuu wa wana wa Yuda;"


➡️Nashoni alikuwa Mkuu wa Wana wa Yuda.

Katika Kabila la Yuda kulikuwa na maelfu ya Watu ila Nashoni ndio alikuwa Mkuu wao, ilitokeaje?

Huwa haitokei tu Bali Kuna watu MUNGU amewaweka wawe wakuu


◾Mtu Mkuu ni Mtu gani?


◼️Mtu Mkuu ni Mtu mwenye Madaraka juu ya wengine katika Eneo alilowekwa.


◼️Mtu Mkuu ni Mtu ambaye ni Kiongozi mwenye Mamlaka juu ya watu, jamii au vitu.


◼️Kuna Watu wamewekwa na MUNGU kuwa Wakuu hata katika kazi ya MUNGU.


1 Wakorintho 3:10 "Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake."


◼️Kuna Watu wamewekwa na MUNGU kuwa Wakuu.


Mfano Mwingine ni huu ambapo ni MUNGU Mwenyewe anasema.


Ezekieli 34:24 ''Na mimi, BWANA, nitakuwa MUNGU wao, na mtumishi wangu, Daudi, atakuwa mkuu kati yao; mimi, BWANA, nimesema haya."


➡️Mtu kuwa Mtu Mkuu Haina maana tu ya cheo katika Serikali au kuwa mfanyabiashara mkubwa, Kuna watu ni Wakuu sana Wala sio Wafanyabiashara wakubwa na Wala sio Wafanyakazi wa Serikali Wenye cheo kikubwa, MUNGU anaweza akamweka Mtu kuwa Mtu Mkuu.


◼️Mfano hai ni Ayubu ambaye alikuwa Mtu Mkuu sana.


Ayubu 1:3 "Mali yake nayo yalikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng'ombe mia tano, na punda wake mia tano, na watu wa nyumbani wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki."


➡️Ndugu, Inawezekana MUNGU amekuweka kuwa mkuu katika familia yenu au katika jamii yenu au katika eneo ulilopo.

Ndugu mtii sana MUNGU katika KRISTO YESU aliyekuumba kuwa Mtu Mkuu.


Hesabu 2:5 "Na hao watakaopanga karibu naye ni kabila ya Isakari; na mkuu wa wana wa Isakari atakuwa Nethaneli mwana wa Suari;"


➡️Kama utagundua uliumbwa na MUNGU ili uwe Mtu Mkuu  omba mambo haya chini  yaambatane na Wewe.


Nini  ufanye?


1. Uchumi mkubwa huambatana na watu waliowekwa na MUNGU kuwa Wakuu.


◼️Mfano ni huu wa Isaka.


Mwanzo 24:35 "na BWANA amembarikia sana bwana wangu, amekuwa mtu mkuu; amempa kondoo, na ng'ombe, na fedha, na dhahabu, na watumwa, na wajakazi, na ngamia, na punda."


◼️Watu wakuu huambatana na Mali na utajiri.


Ruthu 2:1 "Basi huyo Naomi alikuwa na ndugu ya mumewe, mtu mkuu mwenye mali, wa jamaa yake Elimeleki, na jina lake aliitwa Boazi."



◼️Omba uchumi mkubwa uambatane na Wewe.


Zaburi 2:8 "Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, Na miisho ya dunia kuwa milki yako."


2. Omba Utisho wa a ki MUNGU uambatane na Wewe maana watu Wakuu waliowekwa na MUNGU watu hao huambatana na Utisho wa ki MUNGU.


➡️Mfano hai ni huu ambapo watu wa mji wanambembeleza Isaka na kumsifia kwa sababu Yuko na MUNGU na ana Utisho wa MUNGU.


Mwanzo 23:6 "Utusikie, Ee bwana, ndiwe mtu mkuu sana kwetu, uzike maiti wako katika kaburi lile utakalochagua katika makaburi yetu. Hapana mtu kwetu atakayekuzuilia kaburi lake, usizike maiti wako."



◼️Omba Utisho wa MUNGU uambatane na Wewe .


Kutoka 23:27 "Nitatuma utisho wangu utangulie mbele yako, nami nitawafadhaisha watu wote utakaowafikilia, nami nitawafanya hao adui zako wote wakuonyeshe maungo yao."


3. Omba MUNGU akupe kustawi huku ukinyenyekea sana kwake maana watu Wakuu waliowekwa na MUNGU ustawi wa ki MUNGU huambatana nao.


Mwanzo 26:13 "Na mtu huyu akawa mkuu, akazidi kusitawi, hata akawa mkuu sana."


4. Jiambatanishe na Watumishi waaminifu wa Bwana YESU KRISTO ili wakubariki na utazidi kuwa Mkuu.


Mwanzo 48:18-20 " Yusufu akamwambia babaye, Sivyo, babangu, maana huyu ni mzaliwa wa kwanza; weka mkono wako wa kuume kichwani pake. Babaye akakataa, akasema, Najua, mwanangu najua, yeye naye atakuwa taifa, yeye naye atakuwa mkuu; lakini ndugu yake mdogo atakuwa mkubwa kuliko yeye, na uzao wake watakuwa wingi wa mataifa. Akawabariki siku ile akasema, Katika ninyi Waisraeli watabariki, wakisema, MUNGU na akufanye kama Efraimu na Manase. Akamweka Efraimu mbele ya Manase."


◼️Yakobo aliwabariki Vijana Ephraim na Manase na baraka ikiambatana nao.


5. Watu wakuu waliowekwa na MUNGU huambatana na Mamlaka ya kiroho .


◼️Omba ROHO MTAKATIFU awe pamoja na Wewe ili Mamlaka ya KRISTO iende na Wewe.


Kutoka 11:3 "BWANA akawapa watu hao kibali machoni pa Wamisri. Zaidi ya hayo, huyo Musa alikuwa ni mkuu sana katika nchi ya Misri, machoni pa watumishi wa Farao, na machoni pa watu wake."


6. Omba usipungukiwe akili njema ya ki MUNGU 


Mithali 28:16 "Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu sana; Bali achukiaye kutamani ataongeza siku zake.'


➡️Ni hatari sana umekuwa Mtu Mkuu lakini huna akili njema ya ki MUNGU ndani Yako.


◼️Mfano wa Mtu Mkuu aliyepungikiwa na akili ni Nabali.


1 Samweli 25:2 "Na huko Maoni kulikuwa na mtu mmoja, ambaye alikuwa na mali yake katika Karmeli; naye yule mtu alikuwa mkuu sana, mwenye kondoo elfu tatu na mbuzi elfu; naye alikuwa akiwakata manyoya kondoo zake huko Karmeli."


➡️Kwa kupungukiwa kwake akili akamdharau hadi Mkuu wa Nchi ambaye alikuwa ameshapakwa mafuta ya ki MUNGU tayari bado kuapishwa tu katika mwili, akamdharau.


1 Samweli 25:10 ''Naye Nabali akawajibu wale watumishi wa Daudi, akasema, Huyu Daudi ni nani? Na mwana wa Yese ni nani? Siku hizi kuna watumwa wengi wanaomtoroka kila mtu bwana wake!"


➡️Nabali Mtu Mkuu asiye na akili njema aliponywa na Mkewe mwenye hekima na akili.


1 Samweli 25:32-3" Naye Daudi akamwambia Abigaili, Na ahimidiwe BWANA, Mungu wa Israeli, ambaye amekuleta hivi leo kunilaki; na ibarikiwe busara yako, na ubarikiwe wewe, uliyenizuia hivi leo nisimwage damu, wala kujilipiza kisasi kwa mkono wangu mwenyewe."


◼️Ukiwa Mtu Mkuu au ukijijua MUNGU amekuweka kuwa Mtu mkuu omba sana hekima ya MUNGU na akili njema iambatane na Wewe.


◼️Ishi Maisha Matakatifu katika KRISTO YESU ili kumruhusu ROHO MTAKATIFU kuwa kwako na kukupa akili na hekima njema


7. Omba MUNGU akufanye kuwa Mtu Mkuu kama umewahi kufunuliwa katika ulimwengu wa roho au ni watu wengine walifunuliwa kwamba Wewe umebeba ukuu ndani Yako au utakuwa Mtu Mkuu.


1 Samweli 9:16," Kesho, wakati kama huu, nitakuletea mtu kutoka nchi ya Benyamini, nawe mtie mafuta ili awe mkuu juu ya watu wangu Israeli, naye atawaokoa watu wangu na mikono ya Wafilisti; maana nimewaangalia watu wangu, kwa sababu kilio chao kimenifikilia."⁰


Asante kwa kujifunza Neno la  siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.

MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

By Mwl Peter Mabula 

Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)

Ubarikiwe

Comments