MAHUBIRI 7 YENYE MATOKEO MAKUBWA ZAIDI KWENYE UFALME WA MUNGU.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.

Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.


◼️Yapo Mahubiri ya yamna mbalimbali lakini yapo pia Mahubiri yenye matokeo makubwa zaidi ingawa baadhi ya Wahubiri hawajui.


◼️Mhubiri endelea kuhubiri Injili ya KRISTO Kwa ujasiri.

Baki kwenye nafasi Yako ya utumishi Kila siku kama walivyofanya Watumishi wa MUNGU wa zamani.


Matendo  5:42 ''Na kila siku, ndani ya hekalu na nyumbani mwao, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema za YESU kwamba ni KRISTO."


◼️Mhubiri endelea kuhubiri Injili ya KRISTO Kwa ujasiri lakini na haya yafahamu pia.


◾Mahubiri Saba yenye matokeo makubwa kwenye Ufalme wa MUNGU.


1. Mahubiri ya kuwafanya watu mioyoni mwao waseme "Tutendeje? Au nifanye Nini nipate Kuokoka?"


Matendo  16:30-31 "kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? Wakamwambia, Mwamini Bwana YESU, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako."


◼️Ukihubiri Kisha Mahubiri Yako yasimfanye Mtu mpagani Kuokoka unakuwa umefanya vyema kuhubiri lakini hukupata matokeo mazuri wakati huo.


◼️Mahubiri yanayoweza kumfanya Mtu ajiulize ndani yake "heri nimpokee YESU", "Sasa niamueje?  ni heri niokoke" 

hayo ni Mahubiri yenye matokeo makubwa zaidi katika Ufalme wa MUNGU.


◼️Mahubiri yanayowafanya watu kuamua mioyoni mwao Kuokoka ni Mahubiri yenye matokeo makubwa zaidi katika Ufalme wa MUNGU.


 ◼️Mahubiri yanayomfanya Mtu amuulize Mhubiri "Sasa nifanyeje?" Au anawauliza watu wake wa Karibu waliookoka "Au Mimi niamue kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wangu? " hayo ni Mahubiri yenye matokeo makubwa zaidi katika Ufalme wa MUNGU.


◼️Mahubiri kama hayo yalihubiriwa na Watumishi wa MUNGU tangu zamani.


Luka 3:10 "Makutano wakamwuliza, Tufanye nini basi?"


◼️Hata Leo Mahubiri kama hayo yapo hivyo na Wewe Mhubiri unayeanza Hakikisha unayahubiri maana ndio Mahubiri yenye matokeo makubwa zaidi katika Ufalme wa MUNGU.


Luka 3:14 "Askari nao wakamwuliza, wakisema, Sisi nasi tufanye nini? Akawaambia, Msidhulumu mtu, wala msishitaki kwa uongo; tena mtoshewe na mshahara wenu."


2. Ni Mahubiri yanawafanya Watu wachomwe mioyoni ili wafanye maamuzi sahihi.


Matendo  2:37 -38 "Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake YESU KRISTO, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha ROHO MTAKATIFU."


➡️Pata picha umetoka kuwahubiri mashoga na ulipomaliza tu kuhubiri wakaenda kufanya ushoga, unawahubiri Wachawi ukimaliza tu wanapanda ungo wa kichawi kwenda kuroga, unamhubiri mzinzi au mwasherati na wakati unahubiri anamwandikia meseji mzinzi mwenzake akisema " Nikitoka tu hapa njoo gheto kwangu chap maana nimekumisi" kwa namna yeyote Mahubiri hayo hayajawafanya watenda dhambi kuchoma mioyo yao ili wafanye maamuzi sahihi ya kubadilika kuacha dhambi zao.

Kwani huna Mahubiri yanayowafanya watu wachomwe mioyoni yao, sababu ni kwamba unahubiri siasa, unahubiri Mafanikio tu, hukemei Dhambi, huonyi watu, Mafundisho Yako ni Mafundisho laini tu yasiyohusika na utakatifu kwa unaowahubiri.


◼️Mahubiri yenye matokeo makubwa zaidi katika Ufalme wa MUNGU ni yake ambayo wakati yanahubiriwa yanawafanya Watu wenye dhambi kuchoma mioyo yao Kisha wanaamua kuanzia muda huo kuacha dhambi.

Siku Moja nilifundisha Kanisani Kawe, nilipomaliza Kuna Mtu mmoja akaniambia ni kweli anatenda dhambi na alikusudia baada ya Ibada aende kutenda dhambi ila ameamua rasmi hataenda kutenda dhambi na kuanzia siku hiyo atabadilika, Mimi nikamshukuru MUNGU na kumuombea.


◼️Kuna watu walikuwa safarini lakini walipopita Karibu na mkutano wa Injili wakasikia Neno la MUNGU safari za kwenda kutenda dhambi zikafa na tangu siku hiyo wakaacha dhambi, hayo ndio Mahubiri yenye matokeo makubwa zaidi katika Ufalme wa MUNGU 


3. Ni Mahubiri ambayo yanamfanya Mtu aamue moyoni mwake kumfuata YESU KRISTO.


Luka 9:56-57 " Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine. Nao walipokuwa wakienda njiani, mtu mmoja alimwambia, Nitakufuata ko kote utakakokwenda."


◼️Ukihubiri na baada ya Mahubiri Yako wakajitokeza watu au Mtu hata mmoja ambaye akasema ameamua kumfuata YESU KRISTO tangu muda huo, hapo umefanya Mahubiri yenye matokeo makubwa zaidi katika Ufalme wa MUNGU.


➡️Omba MUNGU akupe Neema ya kuhubiri Mahubiri yenye matokeo makubwa zaidi katika Ufalme wa MUNGU ambapo unaowahubiria wanaamua wenyewe kumfuata YESU KRISTO kama Mwokozi wao.

Sio yale Mahubiri ambayo Mtu anatoka kama alivyokuja, yaani kama alikuja Kanisa akiwa na dhambi ya uongo anatoka Ibada akiendelea na dhambi yake ya uongo.


4. Ni Mahubiri yanayoleta Nguvu za ROHO MTAKATIFU.


1 Wakorintho 2:4 "Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za ROHO na za nguvu,"


◼️Ukiona Mahubiri ambayo yanamleta ROHO MTAKATIFU katika Ibada ujue hayo ni Mahubiri yenye matokeo makubwa zaidi katika Ufalme wa MUNGU.


◼️Ukiona unahubiri na katika Ibada hiyo Nguvu za ROHO MTAKATIFU zinashuka ujue hayo ni Mahubiri yenye matokeo makubwa zaidi katika Ufalme wa MUNGU.


5. Ni Mahubiri yanayowafanya watu kuwa watakatifu.


 Walawi 11:45 "Kwa kuwa mimi ni BWANA niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili kwamba niwe MUNGU wenu; basi mtakuwa watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu."


◼️Mahubiri yote ni mbegu inayopandwa katika mioyoni ya watu, ukiona mbegu ya Mahubiri Yako imezaa utakatifu kwa watu ujue hapo unahubiri Mahubiri yenye matokeo makubwa zaidi katika Ufalme wa MUNGU.


◼️Kipaombele Cha MUNGU Cha kwanza kwa kila Mtu ni kumpokea YESU KRISTO Mwanae kama Mwokozi wake.


Yohana 3:16 "Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."


◼️Kipaombele Cha pili Cha MUNGU kwa kila Mtu aliyeokoka ni kuishi maisha matakatifu.


1 Petro 1:14-15 " Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;"


➡️Ukiona Mchungaji unaowahubiria hawabadiliki kwa kuacha dhambi na wakaanza kuishi maisha matakatifu Cha kwanza Anza kuchunguza Mahubiri Yako na msisitizo wako katika Mahubiri ni Nini?


◼️Sisitiza zaidi watu Kuishi maisha matakatifu ya Wokovu wa KRISTO YESU Mwokozi.


6. Ni Mahubiri yanayomfanya Mtu kugeuka na kuacha mabaya.


2 Wafalme 17:13 "Pamoja na hayo BWANA aliwashuhudia Israeli, na Yuda, kwa kinywa cha kila nabii, na cha kila mwonaji, akisema, Geukeni, na kuziacha njia zenu mbaya, mkazishike amri zangu na hukumu zangu, sawasawa na ile sheria yote niliyowaamuru baba zenu, nikawapelekea kwa kinywa cha manabii watumishi wangu."


◼️Tangu Zamani MUNGU anataka watu wake wanaotenda mabaya wageuke na kuyaacha hayo mabaya.


◼️Injili ya kweli ni ile inayawafanya watu wabaya kuacha mabaya, hilo ndio kusudi la MUNGU wa Mbinguni.


Mithali 1:23 "Geukeni kwa ajili ya maonyo yangu; Tazama, nitawamwagia roho yangu, Na kuwajulisheni maneno yangu."


◼️Ukihubiri watu wakaacha dhambi na mabaya hapo umehubiri Mahubiri yenye matokeo makubwa zaidi katika Ufalme wa MUNGU.


7. Ni Mahubiri ya Wokovu wa KRISTO yanayoambatana na watu kufunguliwa vifungo, kuponywa na kuwekwa huru mbali na nguvu za giza.


Mathayo 10:7-8 " Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia. Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure."


◼️Hakikisha unahubiri Injili ya Wokovu wa KRISTO YESU, Injili ya namna hiyo huambatana na watu kufunguliwa na kuponywa, na ukifanya hivyo utakuwa umehubiri Mahubiri yenye matokeo makubwa zaidi katika Ufalme wa MUNGU.


➡️Changamoto Leo watu wengi hutaka Miujiza tu bila Injili ya Wokovu hivyo wapo Watumishi ambao Wana Miujiza ya uongo na wengine ni mawakala wa shetani hivyo Miujiza wanayo kweli ila ni ya shetani.

Hivyo mpime Mtumishi anayefanya Miujiza kama anaihubiri Injili ya Wokovu wa KRISTO YESU, Ukiona ana Miujiza bila Injili ya Wokovu wa KRISTO YESU achana na Mhubiri huyo ila Ukiona anayo Injili ya Wokovu wa Bwana YESU KRISTO na Miujiza anayo huo Ambatana naye.


Asante kwa kujifunza Neno la  siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.

MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

By Mwl Peter Mabula 

Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)

Ubarikiwe

Comments