MAOMBI YA KUIFUNGUA NJIA YA KUFANIKIWA KWAKO.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe.

Karibu tujifunze Neno la MUNGU Kisha tuombe Maombi ya ushindi sana.


Isaya 48:17 " BWANA, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni BWANA, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, NIKUONGOZAYE KWA NJIA IKUPASAYO KUIFUATA."

[3/30, 11:48 AM] Peter Mabula: Neno Njia Lina maana mbili.


➡️Njia ni jinsi ya kufanya ili kupata kitu.


➡️Njia pia ni sehemu inagotumiwa ili kupita.


◼️Sasa Kila baraka au jambo fulani ili ulipate Lina njia zake.


◼️Ziko njia za kiroho za kupitishia vitu ambapo Leo tunaomba katika Jina la YESU KRISTO ili kufungua Njia hizo.


Mithali 16:9 "Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali BWANA huziongoza hatua zake."


 ➖Wako watu akiombea hitaji lake fulani Muhimu, baada ya siku chache baada ya Maombi huota ndoto akitembea katika njia ndefu sana na Kwa muda mrefu sana bila kufika au katika njia hiyo anakutana na maadui ambao ni wanyama wakali au vikwazo.


Hiyo yote ni taarifa ya rohoni kwamba njia yake ya kupata baraka hiyo Ina vikwazo hivyo inampasa ashughulikie Kiroho.


◼️Omba Bwana YESU KRISTO aifanye njia kamilifu mbele Yako.


Zaburi 18:32 " MUNGU ndiye anifungaye mshipi wa nguvu, Naye anaifanya kamilifu njia yangu.


◼️ Hakikisha tu pia katika Maisha Yako unatembea katika njia ya utakatifu katika KRISTO YESU.


Isaya 35:8 "Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo."


 Kwanini uombee njia Yako ya mafanikio?


1. Njia ya Mtu inaweza ikazibwa kiroho ili asione Kuvuka Wala kufanikiwa katika anachohitaji.


Ayubu 30:13 "Waiharibu njia yangu, Wauzidisha msiba wangu, Watu wasio na msaidizi."


2. Njia ya Mtu inaweza ikazibwa kiroho ili asipate anachohitaji.


Maombolezo 3:9 "Ameziziba njia zangu kwa mawe yaliyochongwa; Ameyapotosha mapito yangu."


3. Njia Yako inaweza ikawekewa mitego na mawakala wa shetani ili kukuchelewesha kupata baraka Yako.


Ayubu 18:10 "Amefichiwa tanzi chini, Na mtego amewekewa njiani."


4. Kuna njia za taabu, yaani Mtu Maisha yake ili kufanikiwa eneo lolote ni vita sana au atumie Nguvu sana za Maombi na Sadaka sana.


Ayubu 36:15 "Yeye humponya aliyetaabika kwa njia ya taabu yake, Na kuyafunua masikio yao kwa maonevu."


 Mambo Muhimu kujua.


1. MUNGU wa Mbinguni anaweza kuifanikisha Njia Yako, mtegemee tu daima.


Mwanzo 24:42 "Nami nikaja leo kisimani, nikasema, Ee BWANA, Mungu wa bwana wangu Ibrahimu, ukinifanikishia sasa njia yangu niendayo mimi,"


2. Kuna watu katika Maisha yao hawapitii njia ya Amani.


Warumi 3:17 "Wala njia ya amani hawakuijua."


◼️Omba ROHO MTAKATIFU akupe Wewe kupita njia ya Amani.


3. Ukipita njia ya MUNGU katika KRISTO YESU ujue adui hataiweza hiyo Njia.


Warumi 11:33 "Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani!"


4. Usipite katika njia aliyokukataza ROHO MTAKATIFU maana sio njia nzuri kwako.


Mithali 14:12 "Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti."


5. Katika njia zako zote mkiri MUNGU katika KRISTO YESU.


Mithali 3:6 "Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako."


 Mimi Peter Mabula sijui ni njia gani kwako Ina vikwazo vya shetani ndio maana hufanikiwi kwa wakati ila katika KRISTO YESU Kuna ushindi ukiomba.


➡️Je vikwazo kwako viko katika njia ya kupata kazi au katika kupata Ndoa?


➡️Je vikwazo kwako viko katika njia ya kufanikiwa katika biashara au katika huduma Yako?


◼️Katika Jina la YESU KRISTO Kuna ushindi Mkuu.


◼️Leo ifungue njia Yako kwa Maombi katika jina la YESU KRISTO utafanikiwa haraka sana.


◼️Kataa tu kuzifuata njia za Dhambi.


Ayubu 22:15 "Je! Utaiandama njia ya zamani Waliyoikanyaga watu waovu?"


◾ Nini ufanye kwenye Maombi?


1. Tubia dhambi zako zilizosababisha njia Yako kufungwa.


Marko 1:15 "akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa MUNGU umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili."


2. Omba MUNGU aikamilishe njia Yako ili ufanikiwe.


Zaburi 18:32 "MUNGU ndiye anifungaye mshipi wa nguvu, Naye anaifanya kamilifu njia yangu."


 3. Omba ROHO MTAKATIFU akufundishe njia ya kufanikiwa kwako.


Zaburi 32:8 "Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama."


4. Kama unapita njia isiyo sahihi omba ROHO MTAKATIFU akufunulie njia njema ya kupita.


Mathayo 2:12 "Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine."


5. Omba MUNGU akujulishe njia zake zitakazokufanya ufanikiwe.


Zaburi 25:4 "Ee BWANA, unijulishe njia zako, Unifundishe mapito yako,"


6. Omba Bwana YESU KRISTO akupe kutembea kwenye njia zake ili ufanikiwe.


2 Samweli 22:31 Mungu njia yake ni kamilifu; Ahadi ya Bwana imehakikishwa; Yeye ndiye ngao yao Wote wanaomkimbilia.


7. Mshukuru MUNGU Kwa kuwa ni mwema kwako.


Zaburi 118:28 "Ndiwe MUNGU wangu, nami nitakushukuru, Ndiwe MUNGU wangu, nami nitakutukuza."


Asante kwa kujifunza Neno la  siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.

MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

By Mwl Peter Mabula 

Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)

Ubarikiwe

Comments