![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU Kisha tuombe Maombi ya ushindi.
◼️Katika somo hili nimetumia neno "Limitations" kwa sababu ni Neno lililobeba maana nyingi kulingana na Ufunuo niliopewa.
Siku Moja mwaka huu huu nilikuwa katika Maombi yangu binafsi ya Kufunga siku 4 nikiwa nimeweka kambi Kanisani kwa siku hizo.
Katika Maombi hayo nilikuwa naombea mahitaji mbali mbali na nikiombea pia watu mbalimbali, wakati namtaja Mtu mmoja katika Maombi yangu nilisikia Sauti ikisema "Kuvuka limitations alizowekewa na watu, Wakala wa shetani na nguvu za giza"
➡️Ufunuo huo ni somo hili la Leo la Maombi, Kuna watu wengi wanaenda kuvukwa kwa Jina la YESU KRISTO Mwokozi.
Yohana 16:24 "Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu."
Nimetumia neno la kiingeleza kama nilivyosikia rohoni.
◼️Limitations ni Nini?
➡️Limitations ni Vikwazo, vizuizi, upungufu, mipaka ya kuendelea, Ukomo n.k
Ningeyaweka maneno haya yote katika kichwa Cha somo kisingeeleweka vizuri ndio maana nikatumia neno lile Moja "Limitations"
◼️Katika Maisha ya Mwanadamu Kuna limitations zilizowekwa na MUNGU Kwa sababu ya makosa fulani ya Wanadamu.
➡️Mfano hai ni Musa aliambiwa hataingia Kaanani na hakuingia kwa Neno la MUNGU, hivyo Musa aliwekewa mpaka/ limitation.
Kumbu 34:4-5 " BWANA akamwambia, Hii ndiyo nchi niliyowaapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, nikisema, Nitawapa wazao wako. Basi nimekuonyesha kwa macho yako, lakini hutavuka huko.
Basi Musa, mtumishi wa BWANA, akafa huko, katika nchi ya Moabu, kwa neno la BWANA."
➡️Mfano wa pili ni kwamba siku za kuishi Duniani Kwa Mwanadamu yeyote Zina limitations yaani Ukomo.
Ayubu 14:1-2 " Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe."
◼️Hata Mwanadamu angefanyaje lakini lakini siku Moja itakuwa ya Ukomo Kuishi Duniani, hiyo ni limitation iliyowekwa na MUNGU.
Mwanadamu hata afanyeje Kuna muda wa kupukutika kama nyasi au Majani
Isaya 40:6-7 " Sikiliza, ni sauti ya mtu asemaye, Lia! Nikasema, Nilie nini? Wote wenye mwili ni majani, Na wema wake wote ni kama ua la kondeni; Majani yakauka, ua lanyauka; Kwa sababu pumzi ya BWANA yapita juu yake. Yakini watu hawa ni majani."
➡️Adamu aliwekewa limitation/ kizuizi Cha kula kwa jasho, yaani bila kutumia Nguvu za mwili na akili asingeweza kupata vyakula na mahitaji ya kiuchumi na kimwili, lazima afanye kazi.
Mwanzo 3:19 "kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi."
✔️✔️Ndugu, Kuna limitations za MUNGU hizi hazina maswali na Wanadamu wote hukubaliana nazo kwa sababu aliyeziweka ni MUNGU.
◼️Sasa limitations Pekee ambazo hazikuhusu Mwanadamu ni zile zilizowekwa na Watu au Nguvu za giza, limitations hizo Leo kwa Jina la YESU KRISTO ziondoe kwa Maombi.
◼️Usikubali kuishi huku mganga wa kienyeji au mchawi amekuwekewa mipaka katika ulimwengu wa roho ili usifanikiwe katika eneo Fulani.
◼️Usikubali kuishi huku mizimu au mapepo au majini wamekuwekea vizuizi katika ulimwengu wa roho ndio maana hufanikiwi, Leo kwa Maombi katika jina la YESU KRISTO unayo nafasi ya ajabu ya kuomba na kushinda.
Ngoja nikupe mfano wa vizuizi ya adui.
➡️ Paulo alizuiliwa na shetani mara mbili kwenda kuhubiri Injili sehemu fulani.
1 Wathesalonike 2:18 "Kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo, mara ya kwanza, na mara ya pili, na Shetani akatuzuia."
◼️Paulo alikuwa Mtumishi wa MUNGU mwenye Nguvu za MUNGU sana lakini bado Kuna muda akakumbana na limitations za shetani, hiyo ikufundishe usipoomba hata Wewe unaweza kuzuilika Kufunga Ndoa, kuzaa, kuajiriwa, kupona, kusafiri, kuanzisha biashara n.k
Leo katika Jina la YESU KRISTO vuka limitations zote za giza.
➡️Mfano Mwingine ni huu.
Mfalme wa Misri aliweka kipepo limit ya Waisraeli kuongezeka.
Kutoka 1:8-10 " Basi akainuka mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu. Akawaambia watu wake, Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi. Haya! Na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, ikitokea vita, wao nao wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii."
◼️Huyu mfalme ni Mfano wa Wanadamu wanaotumika kipepo ili kuzuia wengine kuzaa.
➖Leo ni watu wangapi ambao Kila akibeba mimba inatoka?
➖Leo ni watu wangapi Kila akipanga jambo jema halitokei?
Leo kwa Mamlaka ya Jina la YESU KRISTO omba kuharibu limitations zote kwenye Maisha Yako.
Huo ndio ushauri wangu Mimi Peter Mabula kwako rafiki yangu, nakuomba rafiki yangu unayesoma somo langu hii omba Kuvuka limitations zote ulizowekewa na Wachawi, majini, mizimu na Wanadamu wabaya.
◼️Kataa kuzuiliwa na nguvu za giza katika jambo lolote la mafanikio Yako.
◼️Leo kwa Jina la YESU KRISTO kataa Wachawi na Waganga kukutenda kwa akili ili wakuwekee Ukomo wa kufika hatua fulani ya Maisha au huduma au kazi.
◼️Kataa adui anayekuzuia kuingia katika Ndoa.
◼️Mpinge Leo adui anayekuzuia Kuvuka kwenda hatua njema ya huduma Yako, kazi Yako, Maisha Yako, biashara Yako n.k pambana naye kwa Jina la YESU KRISTO utashinda.
◼️Bwana YESU KRISTO hakukubali kuzuiliwa na Wanadamu, akapita katikati yao.
Luka 4:28-40 " Wakajaa ghadhabu wote waliokuwa katika sinagogi walipoyasikia hayo. Wakaondoka wakamtoa nje ya mji, wakampeleka mpaka ukingo wa kilima ambacho mji wao umejengwa juu yake, wapate kumtupa chini; lakini yeye alipita katikati yao, akaenda zake."
◼️Wanadamu wanaweza hadi kumzuia Mtu asioe au kuolewa.
1 Timotheo 4:3 "wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli."
◼️Leo kwa Maombi Usikubali Mtu yeyote akuzuie kuingia katika Ndoa.
-Inawezekana unataabika sana kuhusu baraka fulani kumbe kwenye ulimwengu wa roho Kuna limitations za vivywa vya watu wabaya kwako, kumbe Kuna limitations za Wachawi na Waganga au Kuna limitations za mizimu na nguvu za giza zote.
✔️✔️Leo vuka kwa Maombi katika jina la YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai milele.
Nini ufanye katika Maombi?
1. Tubia dhambi zako zote ili uwe safi kwa MUNGU na ili uwe na kibali Cha kuomba na kufanikiwa.
Mathayo 3:2 "Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia."
2. Omba MUNGU akupe kuona ulipowekewa limitations ili uombe na kushinda
Yeremia 33:3 "Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua."
3. Ng'oa limitations zote ulizowekewa na Mawakala wa shetani katika Maisha Yako.
Mathayo 17:20 "YESU akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali MTAUAMBIA MLIMA HUU, ONDOKA HAPA UENDE KULE; NAO UTAONDOKA; WALA HALITAKUWAKO NENO LISILOWEZEKANA KWENU."
4. Achilia mapigo kwa madhabahu za giza zinazotumiwa na adui zako.
2 Samweli 22:38 "Nimewafuatia adui zangu, na kuwaangamiza; Wala sikurudi nyuma hata walipokomeshwa."
5. Omba MUNGU akupe kuishi maisha aliyokuumbia nayo kabla hujazaliwa.
Waefeso 2:10 "Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika KRISTO YESU, tutende matendo mema, ambayo tokea awali MUNGU aliyatengeneza ili tuenende nayo."
6. Pigana kiroho na waweka limitations wa kipepo wa wa Maisha Yako.
Zaburi 71:13 "Waaibishwe, watoweshwe, adui za nafsi yangu. Wavikwe laumu na aibu wanaonitakia mabaya."
7. Omba ROHO MTAKATIFU akusaidie Kuvuka limitations zote za kipepo na za watu.
Zaburi 32:8 "Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama."
Asante kwa kujifunza Neno la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments