![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai milele |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki yangu uliye na YESU KRISTO.
◾Ninao ujumbe mfupi wa Neno la MUNGU la Ufunuo kwa ajili ya ushindi wako dhidi ya Nguvu za giza.
◼️Walinzi wa kipepo wanaokulinda wakutane na tetemeko la MUNGU, hayo ndio Maombi yangu Mimi Peter Mabula kwa ajili Yako rafiki yangu unayesoma masomo yangu Kila mara.
➡️Walinzi wote wa kipepo waliowekwa na mawakala wa shetani kwamba wakuzuie kuingia katika Ndoa au kuzaa au kufunguliwa au kupona , hao wapambe wa shetani katika Jina la YESU KRISTO wakutane na tetemeko la MUNGU.
◼️Yamkini bado hujaelewa kama Kuna tetemeko la MUNGU linaloweza kuwatesa maadui zako tu Wewe uliye na KRISTO YESU na unaishi Maisha Matakatifu, ngoja nikupitishe katika maandiko haya.
◼️◼️Watu wa Moabu wenye Nguvu sana waliokuwa wanasumbua watu wa MUNGU siku Moja walikutana na tetemeko la MUNGU likawatowesha na kuwayeyusha hata hawakuwasumbua Tena watu wa MUNGU.
Kutoka 15:15 "Ndipo majumbe wa Edomu wakashangaa, Watu wa Moabu wenye nguvu tetemeko limewapata, Watu wote wakaao Kanaani wameyeyuka."
✔️✔️Tetemeko la MUNGU liwapige Wachawi wote wanaokusumbua au kusumbua Ndoa Yako.
Katika Jina la YESU KRISTO imekuwa.
✔️✔️Tetemeko la MUNGU liwapate majini wote waliotumwa na mganga ili kutesa Maisha Yako.
✔️✔️Tetemeko la MUNGU liwapige watu wabaya wanaofanya mipango ufukuzwe kazi au usipate kazi.
◼️◼️Kuna tetemeko la MUNGU huwa linashughukika na maadui tu ndio maana tetemeko hilo lilipotokea Gerezani walimokuwemo akina Paulo lilishughulika na Walinzi tu huku akina Paulo wako salama.
Matendo 16:26 "Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa."
✔️✔️Leo katika Jina la YESU KRISTO tetemeko hilo hilo kwenye ulimwengu wa roho lishughulike na mizimu wote wanaokutesa, lishughulike na makuhani wa Madhabahu za giza wanaokutesa na lishughulike na mawakala wa shetani wote wanaotaabisha Maisha Yako.
◼️◼️Bwana YESU KRISTO anazo Nguvu nyingi mojawapo ni Nguvu ya tetemeko ndio maana Wakati anaukamilisha Wokovu wetu pale Msalabani Walinzi walikutana na nguvu ya tetemeko hilo ikabidi kwa usalama wao waanze tu kukiri YESU KRISTO ni Mwana wa MUNGU.
Mathayo 27:54 "Basi yule akida, na hao waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu, walipoliona tetemeko la nchi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakisema, Hakika huyu alikuwa Mwana wa MUNGU."
✔️✔️Walinzi hawa kabla walikuwa wamejaa viburi na dharau kwa YESU KRISTO hadi wakawa wanamdhihaki wakisema "Kama ni Mwana wa MUNGU jiponye" lakini Nguvu ya tetemeko la YESU KRISTO liliwafanya walinzi waanze wenyewe bila kuhubiriwa na Mtu, waaenze kusema YESU KRISTO ni Mwana wa MUNGU.
✔️✔️Leo wapo wapinga KRISTO ambayo Wana maneno ya dharau kwa YESU KRISTO, ni kwa sababu hawajakutana na nguvu ya tetemeko lake, siku walikutana na nguvu ya tetemeko lake watakiri wenyewe kwamba YESU KRISTO ni MUNGU na hakuna uzima wa milele nje na yeye.
➡️Rafiki yangu, kwa YESU KRISTO walinzi wenyewe walimkiri YESU baada ya kukutana na tetemeko lake.
➡️Kwa Paulo na Sila walinzi walikutana na tetemeko la MUNGU hadi mlinzi mkuu atakata kujiua akaokolewa na Paulo.
◼️Inawezekana unateswa na majini waliotumwa kwako, Leo katika Jina la YESU KRISTO omba hao majini wakutane na tetemeko la MUNGU wa Mbinguni.
◼️Inawezekana biashara Yako haiendelei kwa sababu ya uchawi na mizimu ya Ukoo, Leo katika Jina la YESU KRISTO omba hao mawakala wa shetani wakutane na tetemeko la MUNGU hawatarudi kwako Tena.
◼️Kila mlinzi aliyewekwa na mganga wa kienyeji ili kuendelea kukutesa, Leo katika Jina la YESU KRISTO omba MUNGU kwamba tetemeko lake liwapate wote bila kubakiza hata mmoja.
◼️Leo omba na mawakala wa shetani wote wanaokufuatilia watakatiliwa mbali kwa Jina la YESU KRISTO.
Asante kwa kujifunza Neno la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments