![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.
Karibu Tujifunze Neno la MUNGU katika ujumbe huu mfupi.
Mithali 1:7 "Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu."
➡️Huwezi kumcha MUNGU Kama una mizigo mingine.
➡️Huwezi kuwa na mizigo ya dhambi harafu unasema unamcha MUNGU.
2 Timotheo 2:19 "Lakini msingi wa MUNGU ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake. Na tena, Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu."
➡️Huwezi kuwa na majini harafu unasema unamcha MUNGU.
➡️Huwezi kuwa mganga wa kienyeji au mchawi harafu useme unamcha MUNGU.
◼️Njia kuu ya kumcha MUNGU ni kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako Kisha ukachagua kujitenga mbali na maovu.
Yohana 3:16-18 " Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU."
◼️Kumcha MUNGU ni chanzo Cha maarifa sahihi yanayohotajika kwa Mwanadamu.
1 Samweli 12:24 "Mcheni BWANA tu, mkamtumikie kwa kweli kwa mioyo yenu yote; maana, kumbukeni jinsi alivyowatendea mambo makuu."
◼️ Ndugu Mche MUNGU Kwa kutii maagizo yake na kuisikia Sauti yake katika ROHO MTAKATIFU.
Kumbu 13:4" Tembeeni kwa kumfuata BWANA, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye."
Asante kwa kujifunza Neno la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments