![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai milele |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe.
◼️Patikana kwenye uwepo wa Nguvu za MUNGU.
Matendo 4:31 "Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa ROHO MTAKATIFU, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri."
➡️Hawa walipatikana kwenye uwepo wa Nguvu za MUNGU wote wakajazwa ROHO MTAKATIFU, huo ni Muujiza wa Miujiza, Hakikisha na Wewe unapatikana kwenye Nguvu za MUNGU.
◼️Kupatikana maana yake kuwepo sehemu sahihi, kwa wakati sahihi na Kwa kusudi maalumu.
➡️Adamu alikuwa anapatikana katika uwepo wa MUNGU lakini siku Moja hakupatikana kwa sababu alitenda dhambi ndio maana MUNGU akaanza kumuuliza Yuko wapi.
Mwanzo 3:9 "BWANA Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?"
◼️Katika Maisha Yako zingatia sana kuwa mtii kwa Neno la MUNGU katika ROHO MTAKATIFU.
Neno la MUNGU linasema kwenye Kila eneo la Maisha Yako hivyo lipe nafasi Kila mara.
Zaburi 107:20 "Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao."
➡️MUNGU anapolituma Neno lake kwako ujue Kuna kazi hilo Neno litafanya kwa faida Yako, usilikwepe kama unahitaji kushinda.
➡️Vipi kama MUNGU amelituma Neno fulani la Injili kwako ili kifungulia baraka zako fulani na Wewe unalikwepa hilo Neno?
Zaburi 147:18 "Hulituma neno lake na kuviyeyusha, Huuvumisha upepo wake, maji yakatiririka."
➡️Uwe na uhakika ulilikwepa Neno la MUNGU la Ufunuo wa ROHO MTAKATIFU utakosa ulichokusudiwa ma MUNGU kupitia Neno hilo.
◼️Jifunze kumtanguliza MUNGU Kila Kila mahali unapokuwa.
Mithali 3:5-6 " Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako."
◼️Jifunze kujitoa kwa ajili ya wengine kwa ajili ya KRISTO YESU.
1 Wakorintho 15:58 "Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya BWANA sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika BWANA."
◼️Simama katika Imani ya Wokovu wa KRISTO Hakikisha hakuna kinachoweza kukutoa kwa YESU KRISTO.
Yuda 1:3 "Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu."
◼️Kataa kushindwa na zishinde changamoto zote zinazotokea huku ukimtegemea MUNGU katika KRISTO YESU.
Warumi 8:37 "Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda."
◼️Tafuta nafasi ya kumtumikia Bwana YESU KRISTO Kwa uaminifu.
Warumi 12:11 "kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia BWANA;"
➡️Kama huwezi kuhubiri Mtumikie Bwana YESU KRISTO Kwa kutoa pesa zako ili kuwapeleka Wahubiri.
Warumi 10:15 "Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!"
➡️Unaweza ukamtumikia Bwana YESU kwa kujenga Kanisa, kushuhudia mitaani Injili au hata kuaalika Ibadani watu 10 Kila wiki.
◼️Mtumikie MUNGU katika nafasi aliyokupa, jithamini na jiamini huku ukifanya kazi hiyo kwa bidii.
◼️Ishi Maisha ya Maombi.
Yuda 1:20 "Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika ROHO MTAKATIFU,"
◼️Mambo yote ya Duniani tuliyakuta hivyo tutayaacha hivyo Kumbuka sana kuishi maisha matakatifu ya Wokovu wa Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
1 Petro 1:14 -15 "Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;"

Comments