FARAJA YA KWELI.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 

Bwana YESU KRISTO atukuzwe.

Karibu Tujifunze kitu kupitia ujumbe huu wa Leo.


➡️Ni kweli Kabisa unapokuwa na tatizo unahitaji kufarijiwa.


➡️Unapokuwa kwenye magumu unahitaji faraja.


Zaburi 86:17 "Unifanyie ishara ya wema, Wanichukiao waione na kuaibishwa. Kwa kuwa Wewe, BWANA, Umenisaidia na kunifariji."


◼️Napenda kukuambia kwamba;


1. Neno la MUNGU ni mfariji mkubwa.


Warumi 15:4 "Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini."


◼️Uwe unaisoma Biblia Takatifu maana Ina faraja Yako ya kweli.


Zaburi 23:4 "Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji."


◼️Uwe unahudhuria Ibada za Mafundisho ya Neno la MUNGU maana Neno la MUNGU limebeba faraja nyingi.


2. ROHO MTAKATIFU ni Mfariji Mkuu.


Matendo  9:31 "Basi kanisa likapata raha katika Uyahudi wote na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na kuongezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya ROHO MTAKATIFU."


◼️Amua kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako ili kumruhusu ROHO MTAKATIFU aje Maishani Mwako.


◼️Amua kuwa Mtu wa Kumsikiliza ROHO MTAKATIFU.


◼️Amua kuwa unaomba katika ROHO MTAKATIFU maana Maombi katika ROHO MTAKATIFU ni faraja ya ajabu sana kwako.


  ◼️ROHO MTAKATIFU ni Mfariji wetu Mkuu, Hakikisha uko naye katika nyakati zote.


◼️◼️Kumbuka akikufariji ROHO MTAKATIFU ujue amekufariji MUNGU Mwenyezi na amekufariji Bwana YESU KRISTO Mwokozi.


2 Wathesalonike 2:16-17 " Na Bwana wetu YESU KRISTO mwenyewe, na MUNGU Baba yetu, aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema, awafariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika kila neno na tendo jema."


3. Watu wa MUNGU wenye kitu cha ki MUNGU kwa ajili yako, hao ni faraja kubwa kwako.


◼️Mfano hai ni Timotheo aliyetumwa kuwafariji Kanisa la mahali fulani.


1 Wathesalonike 3:2 "Tukamtuma Timotheo ndugu yetu, mtumishi wa Mungu katika Injili ya Kristo, ili kuwafanya ninyi imara na kuwafariji kwa habari ya imani yenu;"


◼️Mfano hai ni Rebecca aliyefanyika faraja ya Isaka baada ya kuondokewa na Mama yake Mzazi.


Mwanzo 24:67 "Isaka akamwingiza Rebeka katika hema ya mama yake, Sara, akamtwaa Rebeka, akawa mkewe, akampenda; Isaka akafarijika kwa ajili ya kufa kwa mamake."


Watumishi wa MUNGU waaminifu katika KRISTO YESU siku zote MUNGU huwapa faraja kwa ajili ya Watakatifu wanapopitia magumu yeyote.


1 Wathesalonike 5:11 "Basi, farijianeni na kujengana kila mtu na mwenzake, vile vile kama mnavyofanya."


◼️Lakini pia hakuna gumu lolote la kudumu hivyo omba MUNGU muda wa magumu nao upite kwenye Maisha Yako ili uje wakati wa furaha ya kudumu.


1 Wakorintho 10:13 "Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili."


4. MUNGU anaweza kumtuma Malaika ili kumfariji Mtumishi wake mwaminifu katika KRISTO YESU.


Zekaria 1:13 "Naye BWANA akamjibu yule malaika aliyesema nami kwa maneno mazuri, maneno yenye faraja."


◼️Mche MUNGU katika KRISTO YESU, Mtumikie Bwana YESU na kaa katika kusudi la MUNGU ili upate kibali Cha MUNGU Cha kuwatuma Malaika kwa ajili Yako.


➡️Lakini ni muhimu kujua kwamba unahitaji faraja katika tatizo ambalo sio dhambi na wala sio tatizo ambalo chanzo chake ni maovu yako.


Mfano Mtu umeiba ukavunjwa mguu useme unahitaji faraja, hapana hapo ni kutubu na kumrudia Bwana YESU na Kwa Wokovu.


◼️Hakuna faraja ya MUNGU katika mambo ya dhambi yaliyoleta tatizo.


Mfano Mtu azini apate magonjwa ya zinaa, usianze Kutafuta faraja, hapo Dawa ni kutubu, kurudi kwa Bwana YESU kwa ukamilifu Kisha omba akuponye utapona.


➡️Ukiwa kwenye matatizo uliyoyasababisha mwenyewe kwa dhambi zako unahitaji tu kutubu na kuacha uovu na sio kufarijiwa,  huhitaji kufarijiwa katika dhambi.


➡️Lakini yapo matatizo ambayo ni magumu anayoyapata Mtu wa MUNGU bila dhambi yeyote, kwa hayo wakati mwingine anahitaji kufarijiwa.

Mfano kuondokewa na Mzazi, mwenzi, Ndugu, Mtu wa Karibu n.k


Mfano umesingiziwa n.k

Unahitaji faraja na Mimi nimekupa njia za faraja ya kweli.


Asante kwa kujifunza Neno la  siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.

MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

By Mwl Peter Mabula 

Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)

Ubarikiwe

Comments