![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
◾Naomba Kila Mtu asome ujumbe huu maana nimeona watu wengi sana wakivuka kutoka hali zao za Sasa hasa wansopitia magumu fulani kwenye Maisha yao.
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.
Karibu Tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
◼️Kuna watu mara Saba yao ndio italeta ushindi wao.
◼️Kuna watu mara Saba yao ndio italeta matokeo ya kiroho wanayoyahitaji.
◼️Kuna mara Saba ndio huthibitisha Muujiza.
◼️Hata Neno la MUNGU li hai halina upungufu wowote na hutenda kazi kubwa ya Kila namna kwa Sababu Neno la MUNGU ni kama dhahabu Iliyosafishwa mara Saba, Neno la MUNGU ni safi mno na limebeba majibu ya Kila Mtu katika KRISTO YESU Mwokozi.
Zaburi 12:6 "Maneno ya BWANA ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba."
➡️Ngoja nikupitishe kwenye mifano hai ndani ya Biblia ili unielewe nazungumzia Nini;
1. Ili Naamani apone ukoma takwa la ulimwengu wa roho lilikuwa lazima ajichovye mara katika maji ya Mto Yordani mara Saba.
2 Wafalme 5:10 "Naye Elisha akampelekea mjumbe, akisema, Enenda ukaoge katika Yordani mara saba, na nyama ya mwili wako itakurudia, nawe utakuwa safi."
➡️Kujichovya mara Saba Kwa Naaman kulikuwa Muhimu sana.
➡️Kujichovya mara Moja au mara tatu isingeondoa ukoma wake.
➡️Hata alipojichovya mara ya Nne na mara ya tano na mara ya sita haikutosha kuondoa ukoma wake.
◼️Lakini mara ya Saba yake iliamua hatima yake ya uponyaji.
2 Wafalme 5:14 "Ndipo akashuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa MUNGU; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi."
◼️Kujichovya mara Saba haikuwa matakwa ya Mtumishi Bali yalikuwa matakwa ya ulimwengu wa roho ndio maana Saba ikaja na majibu.
2. Ili Mtoto wa Mama Mshunemu afufuke ilibidi kwanza apige chafya mara Saba.
2 Wafalme 4:35 "Kisha akarudi, akatembea nyumbani, huko na huko mara moja; akapanda, akajinyosha juu yake; na yule mtoto akapiga chafya mara saba, na mtoto akafumbua macho yake.'
◼️Ili uponyaji wa Mtoto yule ukamilike ilikuwa lazima apige chafya mara Saba.
3. Ili Maombi ya kuleta mvua yalete mvua baada ya ukame wa Miaka mitatu na nusu ilibidi Maombi hayo yafanyike kwa uhakika mara Saba.
1 Wafalme 18:43-44 " Akamwambia mtumishi wake, Kwea sasa, utazame upande wa bahari. Akakwea, akatazama, na kusema, Hakuna kitu. Naye akanena, Enenda tena mara saba. Ikawa mara ya saba akasema, Tazama, wingu linatoka katika bahari, nalo ni dogo kama mkono wa mtu. Akanena, Enenda, umwambie Ahabu, Tandika, ushuke, mvua isikuzuie."
➡️Maombi ya mara Moja hayakutosha kuleta mvua ila mara Saba yalileta mvua.
◼️Mara Saba haikuwa matakwa ya Eliya ila ya ulimwengu wa roho ndio maana mara ya Saba ikaja na majibu ya Maombi.
Mimi Peter Mabula sijui kuhusu Wewe Ndugu katika kile unachoombea, Inawezekana Maombi yako ya siku ya kwanza yaliondoa mapepo lakini hayakuiondoa miungu inayokutesa, Kuna mambo kanuni ya ulimwengu wa roho inahitaji mara Saba.
➡️Inawezekana ukitoa Sadaka nzuri uliyoelekezwa na MUNGU baada ya hapo ukaanza kuwalaumu Watumishi wa MUNGU kwamba mbona hujatendewa na Sadaka ulitoa, Inawezekana Sadaka hiyo kazi yake kiroho ilikuwa kushughukika na Wewe ili ukae sawa kiroho na sio kuleta baraka, Kuna watu mara Saba yao ndio italeta majibu makubwa.
◼️Maombi ya mvua wakati wa Eliya yalihitaji mara Saba.
➡️Ndugu, Inawezekana umeomba mara 6 na kuacha na kumbe ungefunga mara ya Saba Maombi Yako hayo yangeleta majibu makubwa sana.
◼️Kuna mambo kwako yabasubiri mara saba Yako mbele za MUNGU ili yatokee.
➡️Inawezekana umekataliwa na wachumba 6 na unataka kujiua, Ndugu usijiue maana ukijiua unajipeleka jehanamu mwenyewe, subiri mara Saba Yako maana katika hiyo mara Saba utampata Mtu aliye Bora kuliko Wachumba 6 wote wote ukiwaunganisha pamoja, mara Saba huwa inazidi mambo ya siku ya kwanza hadi ya 6 yote ukiyaunganisha pamoja.
➡️Hannah alikuwa Tasa ila hitaji lake lilikuwa Uzao, aliomba miaka mingi sana lakini mara Saba yake ilipofika akazaa Mtoto Bora sana aitwaye Samweli.
Hadi Leo Kila Mtu anamjua Mtoto wa Hannah lakini Watoto wa Penina hakuna Mtu anawajua majina kwa sababu tu Hannah katika Saba yake alipata sio tu Bora Mtoto Bali alipata Mtoto Bora.
1 Samweli 1:19-20 " Wakaondoka asubuhi na mapema, wakasali mbele za BWANA, kisha wakarejea na kufika nyumbani kwao huko Rama; Elkana akamjua mkewe Hana; naye BWANA akamkumbuka. Ikawa, wakati ulipowadia, Hana akachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; akamwita jina lake Samweli, akisema, Kwa kuwa nimemwomba kwa BWANA."
4. Kuna mambo Kanuni yake ya kiroho imeamuriwa iwe mara 7 na sio 1 Wala 4 Wala 5.
Walawi 16:19 "Tena atanyunyiza baadhi ya damu juu ya madhabahu kwa kidole chake mara saba, na kuitakasa, ili machafu yote ya wana wa Israeli yaitoke."
➡️Ndugu najua Kuna mambo ukiomba mara Moja tu huwa unaona majibu ni sawa kabisa lakini yapo mengine kanuni yake ya kiroho ni mara 7 hivyo ukigundua jambo hilo mara Moja au mbili au tano haikuwezekana mwambie MUNGU unaomba mara Saba inayotimiza ije kwenye Maisha Yako na itakuja ikiwa na matokeo makubwa kuliko 1 hadi 6 za kwanza.
5. Hata Yeriko ilianguka baada ya kuizinguka mara Saba.
Yoshua 6:4 "Na makuhani saba watachukua tarumbeta saba za pembe za kondoo waume, mbele ya hilo sanduku; na siku ya saba mtauzunguka mji mara saba, nao makuhani watapiga tarumbeta zao."
➡️Kanuni ya kiroho ya kuangusha Yeriko ilikuwa siku Saba.
◼️Tena Yoshua akaambiwa na MUNGU kwamba kwa siku 6 watazunguka Yeriko kimya kimya, yaani alikuwa Maombi ya kimya kimya ya siku 6 lakini Maombi ya siku ya saba yalikuwa Maombi ya kelele na ushindi wa ajabu ukatokea kwao.
Yoshua 6:10 Yoshua akawaamuru watu, akasema Msipige kelele, wala sauti zenu zisisikiwe, wala neno lo lote lisitoke kinywani mwenu, hata siku ile nitakapowaamuru kupiga kelele, ndipo mtakapopiga kelele."
◼️Kanuni ya Kiroho ilihitaji siku 7 na sio chini ya hapo.
Yoshua 6:14 "Siku ya pili wakauzunguka mji mara moja, wakarejea kambini; ndivyo walivyofanya siku sita."
◼️Ilipofika siku ya 7 ukuta mkubwa sana ulianguka wenyewe.
Yoshua 6:20 "Basi watu wakapiga kelele, na makuhani wakazipiga tarumbeta; hata ikawa, hapo watu waliposikia sauti ya tarumbeta hao watu wakapiga kelele kwa sauti kuu sana, na ule ukuta wa mji ukaanguka nchi kabisa, hata watu wakapanda juu, wakaingia katika mji, kila mtu akiendelea kukabili mbele; wakautwaa huo mji."
➡️Inawezekana na Wewe Kuna ukuta mkubwa sana kati Yako na Kufunga Ndoa, kuzaa, kupata kazi, kupandishwa cheo, huduma Yako kukua, kupona ugonjwa mbaya n.k
Ndugu katika Jina la YESU KRISTO mara Saba Yako huo ukuta utaondoka wenyewe.
◼️Nakuomba endelea kuishi maisha matakatifu, endelea kuomba, endelea na Bwana YESU KRISTO utamuona MUNGU wa Miujiza.
➡️Kumbuka na hii Hata Mtu akikukosea msamehe tu hata mara Saba ili ubaki katika utulivu wako wa kiroho huku ukimsubiri Bwana YESU KRISTO katika mara Saba Yako.
Luka 17:4 "Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe."
◼️Katika Maombi Yako omba MUNGU akulipizie kisasi hata mara Saba Kwa mawakala wa shetani waliotesa Maisha Yako wanaotoka kuzimu.
Zaburi 79:12 "Uwalipe jirani zetu mara saba vifuani mwao Laumu zao walizokulaumu, Ee BWANA.''
Kuna watu ushindi wao unaamuliwa katika mara Saba yao mbele za MUNGU.
Asante kwa kujifunza Neno la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments