NGUVU YA NENO LA MUNGU NA MAOMBI.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.

Karibu Tujifunze mambo machache kuhusu Neno la MUNGU na Maombi.


◼️Neno la MUNGU lina kazi nyingi katika kumtengeneza Mtu hata Mtu huyo akampendeza MUNGU katika KRISTO YESU.


Zaburi 12:6 "Maneno ya BWANA ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba."


◼️Neno la MUNGU linaweza kumsaidia  Mtu katika maombi.


Isaya 40:8 "Majani yakauka, ua lanyauka; Bali neno la MUNGU wetu litasimama milele."


➡️Neno la MUNGU liko imara siku zote na hakuna wa kuliyumbisha.


◾Kwanini Neno la MUNGU liko imara?


◼️Ni kwa sababu Neno la MUNGU limehakikishwa na MUNGU mwenyewe.


Mithali 30:5 "Kila neno la MUNGU limehakikishwa; Yeye ni ngao yao wamwaminio."


◼️Hata katika utendaji kazi Neno la MUNGU linaweza kutenda kazi tofauti tofauti kwa wakati mmoja.


Baadhi ya utendaji kazi wa Neno la MUNGU ni huu.


1. Neno la MUNGU linaweza kufanya kazi kama upanga wa ROHO MTAKATIFU.


Waefeso 6:17" Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa ROHO ambao ni neno la MUNGU;"


◼️Neno la MUNGU kama upanga wa ROHO MTAKATIFU linaweza kukata na kuondoa mabaya yote yaliyoshikilia roho zetu mfano mawazo machafu n.k


◼️Neno la MUNGU kama upanga kwa njia ya Maombi linaweza kuwakata maroho wa kuzimu wanaokutesa kiasi kwamba ukawa huru.


◼️Inawezekana ni wewe unalihitaji Neno la MUNGU kama upanga ili likutengeneze hata umpendeze MUNGU.


2. Neno la MUNGU linaweza kufanya kazi kama nyundo.


Yeremia 23:29 "Je! Neno langu si kama moto? Asema BWANA; na kama nyundo ivunjayo mawe vipande vipande?"


◼️Kazi ya nyundo ni kugonga mahali pagumu ili pakawe sawa.


◼️Kazi ya nyungo ni kupasua mahali pagumu.


◼️Nyundo huponda na kusaga vyote vilivyoinuka.


◼️Inawezekana ni wewe unalihitaji Neno la MUNGU kama nyundo ili kupiga rohoni tabia yako ya uzinzi, madawa ya kulevya, tabia ya uchawi, kuvuta sigara, tabia ya pombe na kila tabia sugu zote ndani yako. 


◼️Neno la MUNGU linakufanya utubu na uache dhambi.


◼️Ndugu, inawezekana kabisa wewe unalihitaji Neno la MUNGU kama nyundo kubwa ili kukuponya.


Mathayo 8:16 "Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi,"


◼️Lipokee Neno la MUNGU kama nyundo ili kukufanya umpendeze MUNGU.


◼️Neno kama nyundo linaweza pia kuharibu nguvu za giza zinazokufuatilia kama wewe ni Mkristo muombaji na unajua kuomba katika Jina la YESU KRISTO huku ukitumia Neno la MUNGU.


3. Neno la MUNGU linaweza Kufanya kazi kama moto.


Yeremia 5:14 "Kwa sababu hiyo BWANA, Mungu wa majeshi, asema hivi, Kwa sababu mnasema neno hili, tazama, nitafanya maneno yangu katika kinywa chako kuwa moto, na watu hawa kuwa kuni, nao moto utawala."


◼️Kazi ya moto ni kuchoma na kuteketeza.


◼️Neno kama moto unaweza kulitumia katika maombi na kuzichoma nguvu za giza, kuziunguza na kuzitowesha.


Waebrania 4:12 "Maana Neno la MUNGU li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo."


◼️Kazi ya moto ni kuchoma.


◼️Inawezekana ni wewe unalihitaji Neno la MUNGU kama moto umerithishwa tamaduni za kimila za kipepo ambazo ziko kinyume na Neno la MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi.


◼️Inawezekana ni wewe ni mgumu kutubu na huoni kama unahitaji kutubu, moto ukiuruhusu uteketeze hizo taratibu za kiukoo za kimila hakika hizo taratibu zitaondoka kwa Jina la YESU KRISTO Mwokozi.


◼️Ndugu, unalihitaji Neno la MUNGU katika maeneo yote ya maisha yako.


◼️Litumie Neno la MUNGU katika maombi yako na kubali Neno la MUNGU likutengeneze,litii Neno la MUNGU daima.

Asante kwa kujifunza Neno la  siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.

MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

By Mwl Peter Mabula 

Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)

Ubarikiwe.

Comments