![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.
Karibu Tujifunze kwa ufupi umuhimu wa Macho ya rohoni.
◼️Ni Muhimu Sana Kila Mkristo Kuwa Na Macho Ya Rohoni.
➡️Mfano hai ni kwamba Hajiri na Ishmaeli walitaka kufa jangwani baada ya kupotea na Kisha kwa sababu walipotea muda mrefu jangwani wakakosa maji ya Kunywa, lakini kumbe katika eneo hilo hilo walilokuwepo kulikuwa na kisima kikiwa na maji safi, Kilichowasaidia ni Maombi kwa MUNGU yaliyomleta Malaika ili kumfumbua macho Hajiri ili naone kisima.
Mwanzo 21:14-19 " Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akimtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-sheba. Yale maji yakaisha katika kiriba, akamlaza kijana chini ya kijiti kimoja. Akaenda akakaa akimkabili, mbali naye kadiri ya mtupo wa mshale; maana alisema, Nisimwone kijana akifa; naye akakaa akimkabili, akapaza sauti yake, akalia. MUNGU akasikia sauti ya kijana. Malaika wa MUNGU akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana MUNGU amesikia sauti ya kijana huko aliko. Ondoka, ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa. MUNGU akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana."
➡️Hapo Sasa unajua umuhimu wa Macho ya rohoni.
◼️Usipokuwa na macho ya rohoni Kuna ushindi unaweza usiupate kwa wakati hadi Uone tatizo kiroho Kisha uliondoe kwa Maombi, au MUNGU tu akupe Neema ya kushinda hata bila kuona.
◼️ Ukiwa Na Macho Ya Mwili Utakuwa Unaoni Mambo Ya Mwili Lakini Ukiwa Na Macho Ya Rohoni Utakuwa Unaona Mambo Ya Rohoni.
◼️Ukiwa na macho ya rohoni utatambua mambo mengi kiroho hivyo utaweza hata kuyazuia katika ulimwengu wa Mwili kabla hayajatokea.
Macho ya rohoni yanaweza hata kuona mipango ya Siri, yanaweza kuona hata mawazo ya Mtu juu Yako.
Mfano hai ni huu ambapo Bwana YESU KRISTO alijua hadi mawazo wanayowaza watu kabla hawajatamka katika mwili.
Marko 2:8 "Mara YESU akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao, akawaambia, Mbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu?''
➡️Kumbuka Kila Jambo Kabla Halijatendeka Katika Hali Ya Mwili Huwa Limeanzia Rohoni.
◼️Unatakiwa uwe na ROHO MTAKATIFU ili uweze kujua mambo ya rohoni maana hayo hutambulikana kwa jinsi ya rohoni.
1 Wakorintho 2:14 "Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya ROHO wa MUNGU; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni."
◼️Hata baraka zote chanzo chake ni katika ulimwengu wa roho hivyo fanyia kazi unayoyaona kutokea ulimwengu wa roho.
Waefeso 1:3 "Atukuzwe MUNGU, Baba wa Bwana wetu YESU KRISTO, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake KRISTO;"
◼️Ukimdhibiti Adui Yako Rohoni Hatakuja Kukuonea Kamwe Katika Mwili.
◼️Adui Yako Akikushinda Rohoni Na Katika Mwili Atakushinda Tu usipopambana naye kwa Maombi katika Jina la YESU KRISTO Mwokozi.
◼️Ndio Maana Unatakiwa Uwe Muombaji Na Utakatifu Sana Ili Kushinda Rohoni Na Pia Uombaji Mara Kwa Mara Utakuwa Unanoa Hali Yako Ya Rohoni Hata Uone Vizuri Rohoni.
Wakolosai 1:9-12 " Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni; mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana (YESU), mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya MUNGU; mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha; mkimshukuru BABA, aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru.
◼️Ukiwa Mwenye Macho Ya Rohoni Unatakiwa Uwe Mtii Sana Na Mnyenyekevu Sana Kwa MUNGU Maana Kwa Kufanya Hivyo Utamfanya MUNGU Alitimize Kusudi Lake Kwako.
Asante kwa kujifunza Neno la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments
Mume wangu alibadilika ghafla. Mwanaume ambaye hapo awali alinipenda na kunijali akawa baridi, asiyejali, na mwenye hasira bila sababu. Aliacha kuonyesha nia katika ndoa yetu, akaniepuka kabisa, na hatimaye akaniomba talaka. Nilivunjika moyo kwa sababu nilimpenda mume wangu kwa moyo wangu wote.
Mambo yalizidi kuwa mabaya aliponizuia kila mahali — WhatsApp, Facebook, Instagram — kana kwamba sijawahi kuwepo. Nililia kila usiku nikijiuliza nilifanya nini kibaya.
Siku moja, rafiki wa karibu alinitembelea na kunitambulisha kwa mtu wa kiroho anayeitwa Dkt. Dawn. Kwa kweli, mwanzoni nilikuwa na shaka, lakini niliamua kumweleza kila kitu kwa sababu sikuwa na chochote cha kupoteza.
Dkt. Dawn alinisomea mambo ya kiroho, na nilishtuka. Alifichua siri kuhusu ndoa yangu na maisha yangu binafsi ambayo hakuna mtu aliyejua. Kila kitu alichosema kilikuwa sahihi 100%. Kisha akafichua kwamba mwanamke mwingine alikuwa amemloga mume wangu. Mwanamke huyu alikuwa akimtembelea mara nyingi, na kwa upumbavu niliamini ilikuwa kuhusu kazi tu.
Dkt. Dawn alinisaidia kuvunja uchawi na akafanya ibada yenye nguvu ya kurejesha upendo kwa ndoa yangu.
Kwa mshangao wangu mkubwa, muda mfupi tu baadaye, mume wangu alinifungulia kizuizi mwenyewe na kuanza kunipigia simu na kunitumia ujumbe mwingi, akiniomba nimsamehe na nirudi nyumbani. Mwanzoni nilimpuuza kwa sababu ya maumivu aliyonisababishia, lakini hatimaye alirudi nyumbani akiwa na zawadi na machozi machoni mwake akiomba nafasi nyingine.
Leo, ndoa yetu ni imara zaidi, yenye furaha zaidi, na yenye amani zaidi kuliko hapo awali. Mapenzi kati yetu yanahisi upya kabisa.
Kana kwamba hiyo haitoshi, Dkt. Dawn baadaye alinisaidia na ibada ya ujauzito kwa sababu tulikuwa tumejitahidi kwa miaka mingi kupata watoto. Ndani ya wiki 8, nilipata mimba kiasili, na leo tumebarikiwa na wavulana wawili wazuri wenye afya njema.
Nitaendelea kushukuru milele.
Ukihitaji: Uchawi wa mapenzi wa kuungana tena na mpenzi wako wa zamani
. Usaidizi wa kurejesha ndoa
. Tamaduni za ujauzito za kupata mimba
. Usaidizi wa kiroho kwa kesi za mahakamani au kupona urithi
. Mwongozo na ulinzi wa kiroho
Ninapendekeza sana Dkt. Dawn. Ushuhuda wangu ni wa kweli, na furaha yangu leo ni uthibitisho. WhatsApp yake: +2349046229159. dawnacuna314@gmail.com