![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.
Karibu Tujifunze Neno la MUNGU ambalo ROHO MTAKATIFU amenipa Leo kwa ajili ya Kila Mtu Duniani.
➡️Kumkimbia YESU KRISTO ni kuukimbia Uzima Wa Milele.
◼️Ndugu naomba usiwe Wewe.
◼️Hata Leo YESU KRISTO anasema kwako Wewe usiye naye kwamba.
"Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.- Mathayo 11:28"
◼️Hata Sasa YESU anaendelea kusema juu ya wale waliompokea kama Mwokozi wao Kisha wanaishi Maisha Matakatifu katika yeye, anasema kwao kwamba '' Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu. -Yohana 10:28"
➡️ Ndugu kuhusu YESU KRISTO nakuomba usimsikilize Mtu yeyote Duniani anayekushauri kwamba hakuna umuhimu wa kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako.
◼️Kuhusu Kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi kama Mtu Kuna anayekuzuia usimsikilize kamwe Wala kufuata ushauri wake, hata kama ni Baba Yako au Mama Yako au Mke wako au Mume wako au Mtu yeyote wa Muhimu zaidi kwako, kuhusu jambo la kukukataza kumpokea YESU KRISTO usimsikilize Mtu huyo.
◼️YESU aliweka wazi kabisa kwamba Kuna watu watachukiwa baada ya kumpokea yeye kama Mwokozi wao, chuki hiyo itatokana na sababu nyingi ikiwemo sababu ya kukataa ushauri mbaya wa watu kuhusu YESU KRISTO lakini mwishoni mwa maandiko haya anasema Mtu mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili ya YESU KRISTO Mtu huyo ataiona nafsi yake.
Mathayo 10:34-39 " Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga. Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu;
na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake. Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili. Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili. Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona."
◼️Ndugu unamhitaji sana YESU KRISTO kama unahitaji uzima wa Milele.
◼️Narudia Tena kama unahitaji uzima wa Milele amua Kuokoka.
◼️Narudia Tena hakuna Uzima Wa Milele nje na YESU KRISTO hivyo amua kumpokea Leo awe Mwokozi wako.
◼️YESU unapompokea kama Mwokozi wako anakuandalia makazi Mbinguni maana yake ni uhakika utafika Mbinguni kama utamaliza safari Yako ya Duniani Ukiwa na YESU KRISTO kama Mwokozi wako.
Yohana 14:1-3 " Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo."
➡️Ndugu bado unahitaji Nini zaidi ya uchukue hatua za kuokoa roho Yako Leo?
◼️Amua kumpokea YESU KRISTO Leo.
Asante kwa kujifunza Neno la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments
Mume wangu alibadilika ghafla. Mwanaume ambaye hapo awali alinipenda na kunijali akawa baridi, asiyejali, na mwenye hasira bila sababu. Aliacha kuonyesha nia katika ndoa yetu, akaniepuka kabisa, na hatimaye akaniomba talaka. Nilivunjika moyo kwa sababu nilimpenda mume wangu kwa moyo wangu wote.
Mambo yalizidi kuwa mabaya aliponizuia kila mahali — WhatsApp, Facebook, Instagram — kana kwamba sijawahi kuwepo. Nililia kila usiku nikijiuliza nilifanya nini kibaya.
Siku moja, rafiki wa karibu alinitembelea na kunitambulisha kwa mtu wa kiroho anayeitwa Dkt. Dawn. Kwa kweli, mwanzoni nilikuwa na shaka, lakini niliamua kumweleza kila kitu kwa sababu sikuwa na chochote cha kupoteza.
Dkt. Dawn alinisomea mambo ya kiroho, na nilishtuka. Alifichua siri kuhusu ndoa yangu na maisha yangu binafsi ambayo hakuna mtu aliyejua. Kila kitu alichosema kilikuwa sahihi 100%. Kisha akafichua kwamba mwanamke mwingine alikuwa amemloga mume wangu. Mwanamke huyu alikuwa akimtembelea mara nyingi, na kwa upumbavu niliamini ilikuwa kuhusu kazi tu.
Dkt. Dawn alinisaidia kuvunja uchawi na akafanya ibada yenye nguvu ya kurejesha upendo kwa ndoa yangu.
Kwa mshangao wangu mkubwa, muda mfupi tu baadaye, mume wangu alinifungulia kizuizi mwenyewe na kuanza kunipigia simu na kunitumia ujumbe mwingi, akiniomba nimsamehe na nirudi nyumbani. Mwanzoni nilimpuuza kwa sababu ya maumivu aliyonisababishia, lakini hatimaye alirudi nyumbani akiwa na zawadi na machozi machoni mwake akiomba nafasi nyingine.
Leo, ndoa yetu ni imara zaidi, yenye furaha zaidi, na yenye amani zaidi kuliko hapo awali. Mapenzi kati yetu yanahisi upya kabisa.
Kana kwamba hiyo haitoshi, Dkt. Dawn baadaye alinisaidia na ibada ya ujauzito kwa sababu tulikuwa tumejitahidi kwa miaka mingi kupata watoto. Ndani ya wiki 8, nilipata mimba kiasili, na leo tumebarikiwa na wavulana wawili wazuri wenye afya njema.
Nitaendelea kushukuru milele.
Ukihitaji: Uchawi wa mapenzi wa kuungana tena na mpenzi wako wa zamani
. Usaidizi wa kurejesha ndoa
. Tamaduni za ujauzito za kupata mimba
. Usaidizi wa kiroho kwa kesi za mahakamani au kupona urithi
. Mwongozo na ulinzi wa kiroho
Ninapendekeza sana Dkt. Dawn. Ushuhuda wangu ni wa kweli, na furaha yangu leo ni uthibitisho. WhatsApp yake: +2349046229159. dawnacuna314@gmail.com