![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU Mwenyezi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.
Karibu Tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
◼️Kila Mtu Duniani anamhitaji YESU KRISTO.
Mimi namhitaji YESU KRISTO na Wewe unayesoma ujumbe huu unamhitaji YESU KRISTO.
◼️Ukisoma Mwanzo 49:10 Biblia inamzungumzia YESU KRISTO kwamba mataifa yote wataimtii, Biblia inasema "Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja YEYE, MWENYE MILKI, AMBAYE MATAIFA WATAIMTII."
◼️Hivyo Mtu yeyote asipomtii YESU KRISTO Leo, akakataa kumpokea kama Mwokozi wake ipo siku Mtu huyo atatimiza andiko hili la kumtii YESU KRISTO ila wakati huo atajaribu kumtii akiwa jehanamu maana alimkataa Mwokozi wa watu wote.
◼️Kwa kusema hivyo ninaomba Kila unayesoma ujumbe huu mpokee YESU KRISTO kama Mwokozi wako kama hujampokea hapo utakuwa umemtii sawasawa na kusudi la MUNGU, Ndugu usingoje kumtii YESU KRISTO wakati ukienda jehanamu.
Mathayo 25:41 "Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;"
◼️Amua kumtii YESU KRISTO kuanzia Leo kwa kumpokea kama Mwokozi wako ili usiende jehanamu.
◾Kwanini tunamhitaji Bwana YESU KRISTO?
1. Tunamhitaji YESU KRISTO Kwa ajili ya uzima wa milele maana nje na Yeye hakuna Uzima wa Milele.
Yohana 3:16-18 " Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU."
◼️Ndugu mhitaji YESU KRISTO Kwa kumpokea kama Mwokozi wako Kisha fanya juhudi kuwaambia watu wote wanaokuhusu kwamba wampokee YESU KRISTO kama Mwokozi wao.
2. Tunamhitaji YESU KRISTO Kwa ajili ya uponyaji wa mwili.
◼️Ukisoma Mathayo 9:35 unaona Biblia ikisema kwamba YESU KRISTO anaponya magonjwa yote na madhaifu yote, Biblia inathibitisha ikisema "Naye YESU alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina."
➡️Ndugu baada ya kumhitaji YESU KRISTO Kwa ajili ya Uzima wa Milele unaruhusiwa kumhitaji YESU KRISTO Kwa ajili ya uponyaji.
Katika Biblia ukisoma Yohana 21:25 Biblia inasema Bwana YESU KRISTO alifanya miujiza mingi kiasi hakuna Kitabu Cha kutosha kuiandika yote, na katika Miujiza hiyo mingi sana ni ya kuponya watu, na katika kusoma kwangu Biblia sijawahi kuona mtu ndani ya Biblia ambaye alimwendea YESU kwa uponyaji harafu hakumponya, YESU KRISTO ni mponyaji, na Wewe mhitaji kwa uponyaji utapona.
Hiyo Yohana 21:25 inasema "Kuna na mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa."
➡️Hivyo hata ugonjwa unaokusumbua au unaowasumbua Ndugu zako YESU KRISTO anaweza kukuponya, mhitaji tu kwa ajili ya uponyaji.
3. Tunamhitaji YESU KRISTO Kwa ajili ya ulinzi.
2 Wathesalonike 3:3 "Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda na yule mwovu."
◼️Ukiomba ulinzi katika Jina lake YESU KRISTO ujue atakulinda sawa na Neno lake alilosema lolote tutakaloomba katika mapenzi ya MUNGU atalifanya.
Yohana 14:14 "Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya."
4. Tunamhitaji YESU KRISTO Kwa majibu ya Maombi yetu mbalimbali.
Yohana 14:13 "Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana."
◼️Ndugu omba kwa MUNGU katika jina la YESU KRISTO utapokea majibu Yako.
◼️ Ndugu mhitaji Bwana YESU KRISTO Kwa ajili ya majibu ya Maombi Yako.
5. Tunamhitaji YESU KRISTO Kwa ushindi dhidi ya Nguvu za giza.
Luka 10:19 "Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru."
◼️Kupitia Mamlaka iliyo katika Jina lake tunashinda Nguvu za giza zote.
◼️Leo mhitaji Bwana YESU KRISTO Kwa ajili ya ushindi dhidi ya Nguvu za giza zote.
◼️Hakika Tunamhitaji YESU KRISTO katika Maisha yetu yote.
◼️Kila mtu anamhitaji YESU KRISTO katika Maisha Yake yote.
◼️Tunamhitaji YESU KRISTO ili tupone, tupate uzima wa milele na ili tushinde nguvu za giza zote.
Waebrania 13:8 "YESU KRISTO ni yeye yule, jana na leo na hata milele."
Naamini umejifunza jambo zuri na utafanyia kazi.
Asante kwa kujifunza Neno la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe.

Comments