ULIMHITAJI RAHELI UKABADILISHIWA UKAPEWA LEAH.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki!

Karibu Tujifunze Neno la MUNGU.


◾kwanza naomba ieleweke kwanza kwamba  Sio kwamba Leah ni Jina baya na Wala sio kwamba akina Leah hawafai, hapana, Leah ni Jina zuri sana na wapo akina Leah watu mashuhuri sana na waliofanya mambo makubwa sana. 

Katika somo hili naomba Leah yeyote anayeishi Leo asijiweke kwenye Kundi la Mtu asiyefaa Wala Rachel wa Leo asijione yeye ndiye mwenye kustahili, Inawezekana kabisa Mtu mmoja anayeitwa Leo Rachel akawa katika uhalisia yeye ndio Leah wa kiroho yaani anachukua nafasi ya Mtu Mwingine hata bila yeye kujua.


◼️Lakini Yakobo kwa habari ya nani ataingia nae katika Ndoa alimhitaji Raheli na sio Leah, Yakobo alikuwa na sababu zake binafsi.


➡️Yakobo alimpenda Raheli ama kwa Jina lingine Recho au Rachel.


Mwanzo 29:18-20 " Yakobo akampenda Raheli akasema, Nitakutumikia miaka saba kwa kumpata Raheli, binti yako mdogo. Labani akasema, Afadhali nikupe wewe kuliko mtu mwingine; kaa kwangu. Yakobo akatumika miaka saba kwa kumpata Raheli. Ikawa machoni pake kama siku chache tu kwa vile alivyompenda."


➡️Ingawa Yakobo alimpenda Raheli na alikuwa tayari kulipa mahari ili kumpata siku ya kupewa Mke alibadilishiwa.

Siku ya kukabidhiwa Mke baada ya kumaliza mahari yake aliyoitumikia miaka 7, siku hiyo ya kukabidhiwa Mke muda ulikuwa ni usiku  kulikuwa giza hivyo hakumtambua Binti aliyepewa  hivyo Yakobo badala ya kupewa Rachel wake akapewa Leah.


Mwanzo 29:25-26 " Ikawa, kulipokuwa asubuhi, kumbe! Ni Lea. Akamwambia Labani, Nini hii uliyonitenda? Sikukutumikia kwa Raheli? Mbona umenidanganya? Labani akasema, Havitendeki hivi kwetu, kumtoa mdogo kabla ya mkubwa;"


➡️Katika maandiko hatuoni kama ni MUNGU ndiye aliyembadilishia Mke Yakobo Bali tunaona tamaduni ya kibinadamu ndiyo iliyoamua.


◼️Point kubwa hapa nataka uishike ni " Kubadilishiwa" Yakobo alibadilishiwa Mke.


➡️Hata Wewe unaweza ukabadilishiwa na wakati Mwingine anayekubadilishia akawa ni shetani na mawakala zake.


Ukisoma Mathayo 13:25 Biblia inasema "lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake."

Hii Ina maana kwamba shetani hupanda magugu katikati ya ngano.


◼️Ngano ni watu wema na Watakatifu na magugu ni watu wabaya wasiohusika na ufalme wa MUNGU.


◾Nini nataka niseme?


Ngoja niende kwa mifano.


➡️Ulikuwa kazini vizuri tu na una amani lakini shetani akawabadilishia bosi kazini akawaletea bosi aina ya magugu na ndio ikawa chanzo Cha Wewe kufukuzwa kazi, hiyo maana yake ukihitaji sana uendelee kuwa na Rachel wa Kiroho ila ukabadilishiwa ghafla na hali ikawa tofauti.


➡️Inawezekana una huduma kubwa ndani Yako lakini kukosea kuoa au kuolewa kunaweza kukasababisha usilitumikie kusudi la MUNGU Kwa usahihi, hapo ulimhitaji Raheli wa kiroho ila ukapewa Leah wa kiroho.


➡️Kuna Wachungaji 3 waliwahi kunishirikisha kitu Cha ajabu sana kwamba wake zao ndio kikwazo Cha huduma zao maana walikosea kuoa, kwa kauli zao walisema hivyo.


Mmoja kati yao aliniambia kwamba Mke wake ndio huondoa washirika Kanisani kwa kuwafukuza kabisa hadharani bila kosa.

Hii maana yake huduma Yake ilimhitaji Raheli wa kiroho ila akampata Leah wa Kiroho ili huduma isifike popote.


➡️Kwenye Kanisa baadhi ya Maeneo shetani hupanda Watumishi aina ya magugu, wako tayari hata kumkana YESU na wanafundisha kinyume na Wokovu, hao Mwanzo walikuwa vizuri tu lakini Baadae shetani aliwabadilishia akili zao, ni hatari sana.


◼️Ndugu zangu, shetani Yuko kazini na Kuna magugu anayapanda watu wa MUNGU huja kuyaona Baadae sana.


➡️Huyo Mtu aina ya magugu atajukikana Baadae, anaweza kuwa Mke au Mume au bosi au Mtumishi au Kiongozi au rafiki Yako n.k


Mathayo 13:26-28 " Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu.

 Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu? Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye?"


➡️Vipi kama una rafiki Yako na unamwamini sana lakini akili yake imeanza kubadilishwa na shetani ili aje baadae alete madhara kwako au kwenye Ndoa Yako?


◼️Nakuletea ujumbe huu mgumu  leo ukupe akili na uwe na tahadhari maana Wanadamu hubadilika, asiyebadilika ni Bwana YESU KRISTO pekee, kabla ya kuweka tumaini kwa Wanadamu weka tumaini kwa MUNGU katika KRISTO YESU ambaye atakuwa na Wewe daima.


Mathayo 28:20 "na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari."


◼️Ambatana na Bwana YESU KRISTO asiyebadilika ambaye atakuwa na Wewe hadi ukamilifu wa Dahari.


◼️Kumbuka yupo adui anayeweza kubadilisha, hadi  Kuna Watumishi wanasema hakuna mwisho wa Dunia, hao ni magugu.

Vipi kama Wewe ndio unawategemea hao?


◼️Shetani ni mwizi na huja kuiba anaweza hata kuiba fursa Yako, uchumi wako, uzao wako, kibali chako, hatima njema Yako n.k


Yohana 10:10 "Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele."


◼️Mpinge shetani ambaye ni mwizi, mfuate Bwana YESU KRISTO mwenye uzima wako wa milele.


◼️Leo mpinge shetani kwa Maombi katika jina la YESU KRISTO na Kataa kubadilishiwa iliyo haki Yako au baraka Yako kutoka kwa MUNGU.


➡️Je umebadilishiwa Nini kwenye Maisha Yako?


◼️Omba MUNGU akusaidie.


◼️Kama hujaingia katika Ndoa omba Ukikataa kubadilishiwa mwenzi na adui.


◼️Ombea Kanisa la MUNGU.


◼️Ombea kazi ya Injili.


 ◼️Ombea uzao wako.


◼️Omba MUNGU akubadilishie yeye kile ambacho shetani alikupa mwanzo.


➡️Kuna watu shetani aliwaambatanisha na Wachawi au wapelelezi wa kipepo, Omba ROHO MTAKATIFU akupe kutambua ili ujitenge na Hila za shetani.


◼️Ni Ndoa tu ndio huwezi kuibadilisha hivyo kama ulikubali shetani akakupa Mtu aina ya magugu jiombee kustahimili na muombee mwenzi wako aumbwe upya na MUNGU ndani yake ili asiwe magugu Tena Bali awe ngano.


➡️Kumbuka Hannah alikuwa Tasa lakini kwa dakika chache MUNGU alimbadilisha akawa Mama wa Watoto Wengi.


1 Samweli 1:19 "Wakaondoka asubuhi na mapema, wakasali mbele za BWANA, kisha wakarejea na kufika nyumbani kwao huko Rama; Elkana akamjua mkewe Hana; naye BWANA akamkumbuka."


◼️Hii Ina maana pia kwamba Kuna muda mchache au kwa usiku mmoja tu MUNGU anaweza akabadili chochote.


◾Nini ufanye katika Maombi?


1. Tubia dhambi zako na makosa yako yalimpa shetani uhalali wa kukubadilishia.


Ezra 9:13 "Na baada ya hayo yote yaliyotupata kwa sababu ya matendo yetu mabaya, na kwa sababu ya hatia yetu iliyo kuu, ikiwa wewe MUNGU wetu hukutuadhibu kama tulivyostahili kwa maovu yetu, tena umetupa mabaki;"


2. Omba ROHO MTAKATIFU akupe kutambua yote kukuhusu Wewe na watu watakaokuhusu au wanaokuhusu.


Yohana 16:13 "Lakini yeye atakapokuja, huyo ROHO wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake."


3. Jiombee macho ya rohoni yanayoona.


Waefeso 1:18 "macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;"


4. Maishanj Mwako Pinga Kila kazi za shetani kwa Maombi.


Yakobo 4:7 "Basi mtiini MUNGU. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia."


5. Ombea kazi ya Injili ili magugu yasipate nafasi.


Luka 10:2 "Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni BWANA wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake."


Asante kwa kujifunza Neno la  siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.

MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

By Mwl Peter Mabula 

Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)

Ubarikiwe.

Comments