![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe.
Karibu Tujifunze Neno la MUNGU.
Warumi 6:12 "Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake;"
◼️Dhambi ikikutawala tamaa ya kutimiza dhambi hiyo huwa ni kubwa sana.
◼️Dhambi hubeba kitu kinaitwa tamaa.
◼️Mtu aliyetawaliwa na dhambi ndani yake hutawaliwa Zaidi na tamaa ya kufanya dhambi hiyo.
➡️Ukijiona unatamani sana kufanya jambo fulani baya mbele za MUNGU tambua ndani yako dhambi imekujaa
➡️Dhambi na tamaa mbaya ni mt una mtoto wake.
➡️Ukiishinda dhambi ndani yako na tamaa itaondoka haraka sana ndani yako.
Mwanzo 4:7 "Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde."
Asante kwa kujifunza Neno la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe.

Comments