JE UNATAKA KUPONA UGONJWA.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.

Karibu Tujifunze Neno la MUNGU.


➡️Kuna watu wanaumwa na wanatamani kupona, Jifunze Neno la MUNGU hili la Leo.


➡️ Kwenye ulimwengu wa roho magonjwa yote yanaweza kusikia maana ni roho kamili iwe ni ugonjwa wa kimwili au wa kiroho ni roho kamili.


◼️Mfano wa ugonjwa ni huu


Mathayo 8:6-7 " akamsihi, akisema, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana. YESU akamwambia, Nitakuja, nimponye."


➡️Kuna watu hawaumwi ila Kuna Ndugu zao au rafiki zao wanaumwa, Jifunze ujumbe huu na fanyia kazi.


Luka 8:50 "Lakini YESU aliposikia hayo, alimjibu, Usiwe na hofu, amini tu, naye ataponywa.''


◼️Katika ujumbe huu sijataja ugonjwa gani ila MUNGU wa Mbinguni anaweza kuponya magonjwa yote.

Kama aliweza kufufua watu ambao walikuwa wameoza tayari kama Lazaro atashindwa Nini kuponya ugonjwa wowote.


Yohana 11:39-40 " YESU akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne. YESU akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa MUNGU?"


➡️Changamoto ya watu wengi ni Imani ndogo na kutokufanyia kazi Neno la MUNGU la Ufunuo wa ROHO MTAKATIFU.


◼️Hebu Leo Ndugu ongeza Imani Yako na fanyia kazi maelekezo yote ya MUNGU kwenye ujumbe huu.


Mambo 7 ya kufanya Ukitaka kupona ugonjwa wowote.


1. Kwa Maombi ya Imani mwambie YESU KRISTO akuponye utapona.


◼️Neno lake linathibitisha anaponya magonjwa yote.


Mathayo 4:23 "Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna katika watu."


2. Dai Baraka ya Uponyaji kwa Maombi ya Imani maana kifo cha YESU kilileta Baraka ya Uponyaji.


Isaya 53:5 "Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona."


3. Tambua YESU KRISTO anaponya hivyo mfuate aliko akuponye.


Mathayo 9:35 "Naye YESU alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina."


◼️Mfuate YESU Kanisani, kwenye semina za Neno la MUNGU, kwenye mikutano ya Injili na kule waliko Watumishi waaminifu wa Bwana YESU KRISTO utapona.


◼️ YESU KRISTO yuko Kanisani.


◼️ YESU KRISTO yuko kwenye semina za Neno la MUNGU.


◼️YESU KRISTO yuko mahali Watumishi wake Wanahubiri Injili yake.


◼️ YESU KRISTO yuko kwenye Maombi.


4. Kwa Maombi mwambiye MUNGU ahamishe ugonjwa kutoka ndani yako.


Kumbu 7:15 "Na BWANA atakuondolea ugonjwa wote; wala hatatia juu yako maradhi yo yote mabaya uyajuayo ya Misri, lakini atayaweka juu ya wote wakuchukiao."


◼️Ni Ahadi yake ataondoa ugonjwa au atahamisha magonjwa kutoka ndani ya Wateule wake, utaje huo ugonjwa ukimwambia MUNGU Kwa Imani auhamishe utoke ndani Yako, kwenye damu Yako, kwenye Moyo wako n.k


5. Kwa Maombi ukiwa mtu wa haki dai Uponyaji.


Ayubu 33:26 "Yeye humwomba MUNGU, naye akamtakabalia; Hata auone uso wake kwa furaha; Naye humrejezea mtu haki yake."


◼️Kuna Uponyaji huwafuata watu wa haki tu.

➡️Mfano hai Hezekiah alipona kwa sababu alitaja Maisha yake ya haki.


Isaya 38:2-5 " Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba BWANA, akasema, Ee BWANA, kumbuka haya, nakusihi, kwamba nimekwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana. Ikawa, neno la BWANA likamjia Isaya, kusema, Enenda ukamwambie Hezekia, BWANA, Mungu wa Daudi, baba yako, asema hivi, Mimi nimeyasikia maombi yako, nimeyaona machozi yako; tazama, nitaziongeza siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano."


➡️Mfano Mwingine Nuhu alipona na kifo Cha gharika kwa sababu alikuwa mwenye haki.


Mwanzo 6:9 "Hivi ndivyo vizazi vya Nuhu. Nuhu alikuwa mtu wa haki, mkamilifu katika vizazi vyake; Nuhu alikwenda pamoja na MUNGU."


◼️Uwe Mtu wa haki ili ukidai Uponyaji utapona kwa sababu Wewe ni Mtu wa haki.


◼️Haki ya Mtu inaanza na kuokoka Kisha kuishi maisha ya Haki yaani bila kuonea Mtu, nyanyasa Mtu au kumwibia Mtu.


6. Mwambie Mtumishi wa MUNGU katika KRISTO YESU akuombee utapona.


Yakobo 5:16 "Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii."


◼️Mweleze Mtumishi wa kweli wa Bwana YESU KRISTO atakuombea nawe utapona.

Kama ni Ndugu Yako ndio anaumwa mshauri aende Kanisani kwenye Maombi atapona.


➡️Kumbuka Kuna magonjwa ni ya kiroho na sio kimwili hivyo hata uponyaji wake ni wa kiroho na sio wa hospitalini, Mfano magonjwa ya kurogwa, mizimu, mapepo n.k


7. Kwa Maombi omba au ombewa kuondoa nguvu za giza ndani yako.


Luka 6:18 "na wale waliosumbuliwa na pepo wachafu; waliponywa."


◼️Nguvu za giza ndio chanzo kimojawapo Cha magonjwa yanayotesa wengi, hivyo pambana na nguvu za giza kwenye Maombi na magonjwa yataondoka ndani Yako.


➡️najua Kuna magonjwa ya kimwili na magonjwa ya Kiroho, ugonjwa wa kimwili hospitalini ukienda unapona lakini yapo magonjwa chanzo chake ni ulimwengu wa roho hivyo yanatakiwa kushughulikiwa kiroho ili kupona, Mfano ni kurogwa n.k


➡️Lakini pia yapo magonjwa ya kimwili tu lakini chanzo chake ni ulimwengu wa roho wa giza, ndio maana katika magonjwa yote unamhitaji MUNGU Kwa uponyaji.


◼️Nenda hata kwenye Maombezi Watumishi wa MUNGU katika KRISTO YESU watakuombea utapona.


Luka 8:2 "na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba,"

 Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU la  siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.

MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

By Mwl Peter Mabula 

Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)

Ubarikiwe.

Comments