![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.
Karibu Tujifunze Neno la MUNGU.
◾Kauli mbiu ni Nini?
➡️Neno "kauli mbiu" Lina maana Ni maneno mafupi, ya kuvutia, na yenye ujumbe maalum yanayotumiwa kuhamasisha, kueleza malengo, au kufikisha ujumbe unaokumbukwa kwa urahisi na wanaosikia au wanaousoma.
◼️Hata katika kazi ya Injili sio jambo baya kuwa na kauli mbiu.
➡️Mfano Wahubiri wengi zamani nikiwa Kijana Mdogo, nilipokuwa nawasikia maneno mawili hayakukosekana kwenye Vinywa vyao nikajua hiyo ndio kauli mbiu ya Wahubiri wote Duniani.
◼️◼️Maneno hayo yalikuwa "YESU KRISTO anaokoa" Neno hilo au sentensi hiyo lilisemwa Mwanzoni wa Mahubiri au katikati ya Mahubiri.
◼️◼️Neno la pili lilikuwa Kila mwisho wa Mahubiri yao walisema "Mtu yeyote anayetaka kumpokea YESU KRISTO au anayetaka Kuokoka apite mbele"
➡️Nakumbuka siku Moja nikiwa mwanafunzi wa shule ya msingi katika Kijiji chetu alikuwa Mchungaji mmoja mzee sana akakusanya watu akaanza kuhubiri maneno hayo aliyasema, baadae nikiwa sekondari kule Biharamulo nilijiunga na Ukwata ingawa kwa wakati huo nilikuwa sijaokoka na Kila jumapili tulitembelea Kanisa mojawapo Karibu na shule yetu, huko kote Wachungaji walipokuwa wanaohubiri hawakuacha hata siku Moja kutaja maneno hayo mawili nikiyoyasema, yaani zaidi ya madhehebu 5 tofauti tofauti hakuna Mchungaji ambaye hakusema kwamba "Bwana YESU KRISTO anaokoa hivyo Hakikisha unampokea kama Mwokozi wako" na Neno lingine Kila mwisho wa Mahubiri yao walisema "Nakupa mwaliko wa kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi, yeyote anayetaka kumpokea YESU KRISTO aje mbele"
➡️Sijui kama kauli mbiu hiyo inaendelea Leo Kila mahari ihubiriwapo Injili ya KRISTO.
◼️Ila ni Muhimu sana hawa Wateule wa KRISTO tukawa na kauli mbiu njema.
◼️Mfano Kauli mbiu hii ifanye kuwa yako kwa kuishi na kuikiri kwa watu wote, kauli mbiu hii inatoka 1 timotheo 1:15 inayoweza
“KRISTO alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi ambao wa kwanza wao ni Mimi”
◼️“YESU KRISTO alikuja ulimwenguni kuokoa Wanadamu wa kwanza wao ni Mimi”
◼️Kila mtu akijua kuwa YESU KRISTO alikuja ulimwenguni Kuokoa Wanadamu wa kwanza wao ni yeye atahakikisha anaokoka maana anajua yeye ni wa kwanza katika waliookolewa na YESU KRISTO hivyo hatamwachia mwingine nafasi yake ya kwanza katika waliookoka.
➡️Mtume Paulo anayazungumza katika hii 1 timotheo 1:15 yeye katika historia hakuwa wa kwanza aliwakuta akina Petro na Yohana na maelfu wengine wameshampokea YESU KRISTO na Kuokoka lakini hapa anasema “wa kwanza wao ni mimi” hapa ina maana anajihesabia wa kwanza kama ambavyo Wakristo wote kila mmoja ajihesabu wa kwanza ili asiache nafasi hiyo ya Wokovu ipite.
Waebrania 12:23-26 " mkutano mkuu na KANISA LA WAZALIWA WA KWANZA walioandikwa mbinguni, na MUNGU mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika, na YESU mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili. Angalieni msimkatae yeye anenaye. Maana ikiwa hawakuokoka wale waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya nchi, zaidi sana hatutaokoka sisi tukijiepusha na yeye atuonyaye kutoka mbinguni; ambaye sauti yake iliitetemesha nchi wakati ule; lakini sasa ameahidi akisema, Mara moja tena nitatetemesha si nchi tu, bali na mbingu pia."
◼️Kumbuka YESU KRISTO alikuja kuwatafuta Wanadamu maana walikuwa wamepotea.
Luka 19:10 "Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea."
◼️Hivyo kila anyeokoka ajihesabu wa kwanza wao Kuokoka.
Mimi Nilikuwa muovu sana ila YESU KRISTO akaniokoa hivyo Wokovu ni wangu binafsi hivyo najihesabu ni "wa kwanza wao” katika walioamua Kuokoka, kauli hii ni ya kishujaa sana na ya kushindania Imani.
Yuda 1:3 "Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu."
◼️Ndugu jihesabu wewe ni wa kwanza hivyo hutakiwi kamwe kuipoteza hiyo nafasi ya kwanza.
Kumbuka YESU KRISTO alikuja Kuokoa Wanadamu waliokuwa na dhambi wa kwanza wao ni mimi Peter mabula, na wewe unaweza kutaja jina lako.
Ndugu, achana na kauli mbiu ambazo hazimwinui YESU KRISTO Wala MUNGU.
Leo Kuna madhehebu Wana Kauli mbiu kweli na Kila mshirika anaitaja Kauli mbiu hiyo lakini Kauli mbiu hiyo inainua dhehebu na sio YESU KRISTO mwenye Kanisa, ni vibaya sana.
Wengine Kauli mbiu zao zinainua Wachungaji na sio MUNGU wa Mbinguni, hayo ni makosa makubwa.
Ndugu zangu ni safi mno kuwa na kauli mbiu lakini Hakikisheni zinamwinua YESU KRISTO Mwokozi.
Asante kwa kujifunza Neno la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe.

Comments