![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.
Karibu Tujifunze Neno la MUNGU kuhusu majaribu ambayo kama Mkristo unaweza ukayapitia.
◾Tuanze na maana ya jaribu.
◾Majaribu ni nini?
◼️Majaribu ni mambo magumu ambayo yanampata mtu bila kuyataka.
✔️Majaribu huwa ni ya muda tu.
2 Petro 2:9 "basi, BWANA ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu;"
✔️✔️Biblia Iko wazi sana ikisema MUNGU anajua kuwaokoa Watakatifu wake dhidi ya Majaribu.
➡️Kumbe Kuna muda wa Majaribu lakini pia Kuna muda wa MUNGU kukutoa katika Majaribu hayo.
➡️Unapofikiria unavyoteseka kwenye jaribu ulilopo naomba kukuambia kwamba fikiria pia na kwamba ipo saa ya MUNGU kukutoa katika Majaribu hayo kwa ushindi na ushuhuda.
Mimi Peter Mabula nawiwa sana rohoni mwangu muda huu kukuambia Wewe Mteule wa KRISTO unayepitia katika Majaribu wakati huu kwamba utavuka salama kwa Jina la YESU KRISTO.
✔️✔️Ni kweli umekuwa kwenye Majaribu lakini Kwa jina la YESU KRISTO utavuka Salama.
◼️ Katika maana za Majaribu pia Kuna majaribu ambayo maana yake ni mambo ya kumshawishi Mtu kutenda makosa.
Mfano hai ni pale Bwana wetu YESU KRISTO alipokuwa kwenye Majaribu, tunaona shetani akimwambia amsujudie, hiyo ikufundishe kwamba Majaribu ya shetani Lengo ni ili utende dhambi.
Lakini kwa kielelezo kwetu tunaona Bwana wetu YESU KRISTO akishinda Majaribu hayo ingawa yalikuwa mengi.
Luka 4:13 "Basi alipomaliza kila jaribu, Ibilisi akamwacha akaenda zake kwa muda."
◼️Maana nyingine ya Majaribu ni mambo mabaya yanayompata Mtu bila kupanga wala kukusudia wala kutegemea.
◼️ Majaribu mengine ni ya MUNGU Mwenyewe anakujaribu ingawa Majaribu ya MUNGU ni kwa wakomavu kiroho tu na huwajaribu watu wachache sana.
Mfano katika Biblia nzima MUNGU aliwajaribu watu wachache sana.
Mmoja wapo Ibrahimu.
Mwanzo 22:1 "Ikawa baada ya mambo hayo MUNGU alimjaribu Ibrahimu, akamwambia, Ee Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa."
➡️ Biblia iko wazi sana kwamba majaribu yapo na ni ya aina mbali mbali.
1 Petro 1:6 "Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali;"
◼️Hii maana yake ni kwamba kuna saa unafurahi lakini kabla ya furaha ulipata majaribu.
◼️Andiko linatufundisha kwamba jaribu lina mwisho ndio maana baada ya jaribu furaha.
◼️ Ndugu jaribu unalopitia ni la muda tuu utavuka salama kuna jina la YESU KRISTO.
➡️Inawezekana jaribu lako ni ugonjwa au kunyanyaswa au kukosa Mtoto au kukosa mwenzi wa ndoa ndugu jaribu hilo ni la muda tuu endelea kuwa mwaminifu kwa MUNGU maana muda wa jaribu utaisha na furaha yako itakuja.
1 Wakorintho 10:13 "Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili."
➡️je umefukuzwa kazi ,biashara imeibiwa,unanyanyaswa,
Ndugu katika KRISTO utavuka salama, jaribu hilo ni la muda tuu, vumilia huku ukiomba na kuishi Maisha matakatifu ya Wokovu.
FAIDA ZA KUSHINDA MAJARIBU.
1. Ukiwa katika KRISTO ukashinda majaribu ya duniani utapokea taji ya uzima
Yakobo 1:12 "Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, BWANA aliyowaahidia wampendao."
2. Baada ya jaribu utakuwa kama dhahabu.
Ayubu 23:10 "Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu."
➡️Dhahabu ni kitu cha thamani kila mtu anatamani aione,awe karibu nayo, aimiliki n.k
3. MUNGU atakubariki mambo mengi.
◼️Mfano hai ni Ayubu baada ya kushinda Majaribu alibarikiwa sana na MUNGU.
Ayubu 42:10 "Kisha BWANA akaugeuza uteka wa Ayubu, hapo alipowaombea rafiki zake; BWANA naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza."
◼️Mfano hai ni Ibrahimu ambaye baada ya kushinda jaribu mambo yake yalikuwa mazuri daima.
Mwanzo 22:16-18 " akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema BWANA, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee, katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu."
Asante kwa kujifunza Neno la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe.

Comments