Bwana YESU KRISTO
![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Mwokozi atukuzwe.
Karibu Tujifunze Neno la MUNGU Kisha tuombe Maombi ya ushindi.
Mithali 23:11 "Kwa sababu mkombozi wao ana nguvu; Atawatetea juu yako."
◼️Tunafahamu wakili kazi yake ni kumtetea Mtu na kusababisha ushindi kwa Mtu huyo.
◼️◼️Sasa katika kesi za kiroho unahitaji Mtetezi na huyo si mwingine ila ni YESU KRISTO na ROHO MTAKATIFU.
◼️Ukisoma Ayubu 19:25 unagundua kwamba MUNGU katika YESU KRISTO kwa njia ya ROHO MTAKATIFU anaweza kuwa mtetezi.
Biblia inasema Ayubu 19:25 "Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi."
◼️Na ukisoma Lukka 12:11-12 unaona ROHO MTAKATIFU kama mtetezi anaweza kukupa hata Neno la kusema kwenye mabalaza ya watesi.
Biblia inasema Luka 12:11-12" Na watakapowapeleka ninyi mbele ya masinagogi na maliwali na wenye mamlaka, msifadhaike kwa kuwaza maneno yenu jinsi mtakavyojibu au kusema; kwa kuwa ROHO MTAKATIFU atawafundisha saa ile ile yawapasayo kuyasema."
➡️Kuna Watu wapo kwenye kesi za kiroho zinazomuhitaji tu MUNGU kama mtetezi ndipo watashinda.
➡️Kunawatu kesi zao ni kuzuiliwa kipepo kuingia kwenye Ndoa au kuzaa .
➡️Kuna watu kesi zao ni za kibinadamu yaani kesi mahakamani au vikao vya ndugu dhidi yake.
➡️Kuna watu kesi zao ni magonjwa ili wafe ,migogoro ya ndtoa,kukosa kazi ,kuonewa kazini n.k
◼️Leo kwa Maombi muite YESU KRISTO kama mwanasheria wako naye atakutetea utashinda au kufanikiwa.
Chanzo cha ujumbe huu nilisikia ujumbe ukiniambia mimi Peter Mabula kwamba “OMBA BWANA YESU KRISTO AWE MTETEZI WAKO,WAKILI WAKO NA MWANASHERIA WAKO “ndugu fanyia kazi na utamwona MUNGU wa mbinguni.
Mithali 22:23 "Kwa sababu BWANA atawatetea; Naye atawateka uhai wao waliowateka."
◼️ MUNGU katika kukutetea anaweza hata kuteka uhai wa walio kuteka,mapepo, wachawi n.k.
◾ Neno mtetezi linamaana 2.
✔️✔️Mtetezi ni yule anayetetea wale wanaodhulumiwa, kile ulichodhulumiwa kiroho YESU anaweza kukutetea ukakipata.
✔️✔️Mtetezi ni yule anayetetea haki za wengine.
YESU KRISTO anaweza kutetea haki yako ,omba tu kwa MUNGU katika jina lake.
◼️MUNGU katika kukutetea anaweza hata kuwasumbua adui zako.
Yeremia 50:34 "Mkombozi wao ni hodari; BWANA wa majeshi ndilo jina lake; yeye atawatetea kwa bidii, apate kuistarehesha nchi, na kuwasumbua wakaao katika Babeli."
◾Ngoja nikueleze baadhi ya mambo ambayo MUNGU katika KRISTO YESU anaweza kuyatetea kwako.
1. YESU anaweza kukukomboa kwa kuukomboa uhai wako uliokuwa katika kuondoka.
Maombolezo 3:58 "Ee BWANA umenitetea mateto ya nafsi yangu; Umeukomboa uhai wangu."
2. YESU kama wakili wako anaweza kukupa kuishi hata kama kwenye mashtaka ya kiroho yaliandikwa ufe.
Zaburi 102:20 "Ili akusikie kuugua kwake aliyefungwa, Na kuwafungua walioandikiwa kufa."
NINI UFANYE KATIKA MAOMBI?
1. Tubia dhambi zako na kuziacha ili iwe rahisi yesu kukutetea
Ayubu 42:6 "Kwa sababu hiyo najichukia nafsi yangu, na kutubu Katika mavumbi na majivu."
2. Omba MUNGU akutetee(eleza akutetee kwenye nini)
Yeremia 50:34 "Mkombozi wao ni hodari; BWANA wa majeshi ndilo jina lake; yeye atawatetea kwa bidii, apate kuistarehesha nchi, na kuwasumbua wakaao katika Babeli."
3. Katika vikao vya kibinadamu vinavyoweza kukuweka hatiani omba ROHO MTAKATIFU awe na kinywa chako
Kutoka 4:12 "Basi sasa, enenda, nami nitakuwa pamoja na kinywa chako, na kukufundisha utakalolinena."
4. Omba MUNGU akutetee mahakamani.
Isaya 51:22 "BWANA, BWANA wako na MUNGU wako, awateteaye watu wake, asema hivi, Tazama, nimeondoa mkononi mwako kikombe cha kulevya-levya, hilo bakuli la kikombe cha hasira yangu; hutakinywea tena;"
5. Omba MUNGU akulipizie kisasi katika kukutetea
Yeremia 51:36 "Basi, Bwa5na asema hivi, Tazama, nitakutetea, nami nitatwaa kisasi kwa ajili yako; nami nitaikausha bahari yake, nitaifanya chemchemi yake kuwa pakavu."
6. Omba YESU KRISTO awe upande wako
Warumi 8:31 "Basi, tuseme nini juu ya hayo? MUNGU akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?"
7. Mfukuze adui kwa maombi.
Yoshua 23:10 "Mtu mmoja miongoni mwenu atafukuza watu elfu; maana BWANA, Mungu wenu, ndiye anayewapigania, kama alivyowaambia."
Asante kwa kujifunza Neno la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe.

Comments