MAOMBI YA KUAMSHA BARAKA ZAKO.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 


Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.

Karibu Tujifunze Neno la MUNGU Kisha tuombe Maombi ya ushindi.


◼️Kuna vitu au baraka hadi uamshe kwa Maombi ndipo vinatokea.


◾Ngoja nianze na mifano 5.


1. MUNGU aliiamsha roho ya Zerubabeli na Joshua ili Wamtumikie.


Hagai 1:14-15 " BWANA akaiamsha roho ya Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, liwali wa Yuda, na roho ya Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, na roho zao mabaki ya watu; wakaenda, wakafanya kazi katika nyumba ya BWANA wa majeshi, MUNGU wao; katika siku ya ishirini na nne ya mwezi, katika mwezi wa sita, katika mwaka wa pili wa Dario mfalme."


➡️Hawa walikuwepo tu, Tena walikuwa Viongozi wa Kiroho ila mpaka roho zao zilipoamshwa kwa habari ya utumishi ndipo wakaanza kutumika.


➡️Kuna Mtu Inawezekana unasoma ujumbe huu hadi utakapoamshwa roho Yako na Bwana YESU ndipo utaanza kumtumikia, kwa Sasa roho Yako kama imefungwa ndio maana huoni ukubwa wa kuanza kumtumikia Bwana YESU KRISTO.

◼️Ndugu, ujumbe huu ukupe akili na utumie kwa Maombi ili uamke.


2. Waisraeli kwa miaka zaidi ya 1800 walikuwa wanaishi mataifa mbalimbali utumwani ingawa kwao wanapajua, lakini majira yalipofika  ya MUNGU kuamsha roho zao ndipo wakarudi Israeli ya Sasa.


Yoeli 3:6-7 " tena watoto wa Yuda na watoto wa Yerusalemu mmewauzia Wayunani, mpate kuwahamisha mbali na mipaka yao; tazameni, nitawaamsha wapatoke mahali mlipowauza, nami nitawarudishia malipo yenu juu ya vichwa vyenu wenyewe."


◼️Point ni kwamba mpaka walipoamshwa na MUNGU ndipo Kila Mtu akawa na msukumo wa kurudi kwako hivyo wakaanza kurudi na mwaka 1948 wakawa Taifa huru Tena wakiwa katika nchi yao.


➡️Hata vita ya Sasa kati ya Waisraeli na Waarabu ni kwa sababu Waisraeli waliamshwa na MUNGU kurudi katika nchi yao na walilorudi katika nchi yao waliwakuta Waarabu wamekaa hapo miaka zaidi ya elfu Moja.


➡️Pia Kumbuka Israeli anachukiwa na shetani aliye ndani ya wapinga KRISTO, Lengo la shetani ni kuwaondoa Israeli sehemu Wokovu wa KRISTO ulianzia kitu ambacho hakiwezekani Tena.


◼️Point ni kwamba Waisraeli hadi walipoamshwa na MUNGU ndipo walipakumbuka kwao na kuanza mipango ya kurudi.


➡️Kuna Mtu Leo hadi aamshwe kiroho kwa Maombi ndipo atapakumbuka Nyumbani kwao na kuwakumbuka Wazazi wake.


◼️ Ndugu omba katika Jina la YESU KRISTO utaona matokeo ya MUNGU kuamsha roho za watu ili wafanye iwapasavyo katika kusudi la MUNGU.


3. MUNGU aliiamsha roho za Viongozi wa kabila la Yuda na Benjamini ili kujenga hekalu Yerusalemu.


Ezra 1:5" Ndipo wakaondoka wakuu wa mbari za mababa, wa Yuda na Benyamini, na makuhani, na Walawi, naam, watu wote ambao MUNGU amewaamsha roho zao kukwea, ili kuijenga nyumba ya BWANA, iliyoko Yerusalemu."


➡️Inawezekana ninyi mna ujenzi wa Kanisa ila miaka Sasa hakuna kinachoendelea, nyumba zenu mnajenga ila nyumba ya MUNGU mmesinzia kuhusu kuijenga kiasi kwamba  hakuna anayeshtuka, Leo omba MUNGU ili aamshe roho za watu kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa la KRISTO.


4. Bwana YESU KRISTO alifanya Maombi ya kumwamsha na kumwinua  msichana aliyekuwa amekufa, akaamka na kupona.


Marko 5:41-42 " Akamshika mkono kijana, akamwambia, Talitha, kumi; tafsiri yake, Msichana, nakuambia, Inuka. Mara akasimama yule kijana, akaenda; maana alikuwa amepata umri wa miaka kumi na miwili. Mara wakashangaa mshangao mkuu."


➡️Maana Mojawapo ya hii ni kwamba tunaweza kuomba Maombi ya kuamsha na vikaamka tunavyotaka viamke.


5. MUNGU anaweza akaamsha roho za adui zako ili wapigane wao kwa wao kwa ushindi wako Wewe.


◾Mfano ni huu.


Isaya 19:2 "Nami nitawaamsha Wamisri juu ya Wamisri; nao watapigana, kila mtu na ndugu yake, na kila mtu na jirani yake, mji juu ya mji, na ufalme juu ya ufalme."


◼️Ndio maana Maombi ya kuamsha ni Muhimu sana, Leo omba katika Jina la YESU KRISTO utamuona MUNGU wa Mbinguni.


➡️Ni Wewe tu ndio unajua unatakiwa kuomba kuamsha Nini?


➡️Mwingine anaombea mwenzi wake wa Ndoa ili aamke kwa ajili ya ujenzi au kwa ajili ya kuikumbuka familia na kuithamini na kuijali.


➡️Mwingine anamuombea bosi wake ili aamke na kumpandisha cheo au kumuongezea Mshahara.


➡️Mwingine anaombea Watumishi wa KRISTO ili waamke na kuipeleka Injili wilayani kwao n.k


➡️Mimi sijui Wewe unataka kuombea Nini lakini yapo Maombi ya kuamsha, na   Maombi hayo ni Leo unaposoma somo hili ambalo Mimi Peter Mabula nimekuletea Leo kwa Ufunuo wa MUNGU Mwenyewe.


◼️Leo omba kuamsha baraka zako, ushindi wako, afya Yako, uzao wako, kibali chako n.k


➡️Inawezekana unanyanyasika kazini kwako kwa sababu wafanyakazi wenzako wanatumia rushwa kukuangusha, unaweza ukaamsha roho ya bosi kwa Maombi ili huyo bosi asione fedha ya rushwa wanayompa watu wabaya  ili kutoa maamuzi kuhusu Wewe.

Mfano ni huu


Isaya 13:17 "Tazama, nitawaamsha Wamedi juu yao, ambao hawaoni fedha kuwa kitu, wala hawafurahii dhahabu."


◼️MUNGU Kwa Maombi Yako katika Jina la YESU KRISTO anaweza akaamsha watu wakuu wasiopendelea hivyo ikiwa hivyo hutaonewa kamwe.


◼️Maombi ya Leo yanahitaji Imani kubwa katika Jina la YESU KRISTO na hicho unachokiamsha kwa Maombi kitaamka.


➡️Unaweza ukaamsha Watoto ndani Yako na ukazaa hata kama madaktari walisema huwezi kuzaa.


➡️Mkumbuke Petro aliyeomba Maombi ya kumwinua  kiwete na huyo kiwete akainuka.


Matendo  3:6-7 " Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la YESU KRISTO wa Nazareti, simama uende. Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu."


➡️Hata Wewe unaweza kuamsha chochote kwa Maombi katika kusudi la MUNGU.


➡️Petro pia aliomba Maombi ya kumwamsha Tabitha na akamka.


Matendo  9:40 "Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, ondoka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi."


➡️Hata wewe unaweza ukaomba Maombi ya kuasha na ikawezekana kwa Jina la YESU KRISTO Mwokozi.


➡️Kwa Maombi Wewe unaweza ukaomba Maombi ya kumwamsha Mchumba wako akaamka na kuanza mipango ya Ndoa ambayo imesimama muda mrefu.


➡️Unaweza ukaomba kuwaamsha Watoto wako na ukazaa kwa jina la YESU KRISTO.


◾Nini ufanye katika Maombi?


1. Leo amsha roho za watu kuwa upande wako dhidi ya adui zako.


Mfano ni huu


Isaya 19:2 "Nami nitawaamsha Wamisri juu ya Wamisri; nao watapigana, kila mtu na ndugu yake, na kila mtu na jirani yake, mji juu ya mji, na ufalme juu ya ufalme."


2. Leo kwa Maombi amsha roho za watu wa kukusaidia ili kutimiza kusudi la MUNGU aliokuitia.


Mfano ni huu


Ezra 1:5 "Ndipo wakaondoka wakuu wa mbari za mababa, wa Yuda na Benyamini, na makuhani, na Walawi, naam, watu wote ambao MUNGU amewaamsha roho zao kukwea, ili kuijenga nyumba ya BWANA, iliyoko Yerusalemu."


3. Leo kwa Maombi iamshe afya Yako njema, amsha Ndoa ili ufunge ndoa n.k


Mathayo 17:20 "YESU akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; WALA HALITAKUWAKO NENO LISILOWEZEKANA KWENU."


4. Leo amsha uchumi mzuri, amsha watu kuja kununua kwenye biashara Yako n.k


Yohana 15:16 "Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ILI KWAMBA LOLOTE MMWOMBALO BABA KWA JINA LANGU AWAPENI."


5. Leo amsha uponyaji kwenye mwili wako, omba katika Jina la YESU KRISTO.

Kumbuka Bwana YESU aliiamsha uponyaji ukatokea.


Luka 7:14-15 " Akakaribia, akaligusa jeneza; wale waliokuwa wakilichukua wakasimama. Akasema, Kijana, nakuambia, Inuka. Yule maiti akainuka, akaketi, akaanza kusema. Akampa mama yake."


6. Omba MUNGU aamshe roho za watu ili kile alichokuambia zamani kitimie.


2  Nyakati 36:22 "Ikawa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la BWANA alilolisema kwa kinywa cha Yeremia lipate kutimizwa, BWANA akamwamsha roho yake Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote, akaiandika pia, akisema,"


7. Omba MUNGU aamshe roho za wenye Nguvu watakaopigana na adui zako ili Wewe uwe Salama.


2Nyakati 21:16 "BWANA akawaamsha roho Wafilisti, na Waarabu waliowaelekea Wakushi juu ya Yehoramu,"


8. Omba MUNGU aamshe mjeledi kwa adui zako.


Isaya 10:26 "Na BWANA wa majeshi ataamsha mjeledi juu yake, kama vile alivyopiga Midiani karibu na jabali la Orebu; na fimbo yake itakuwa juu ya bahari, naye ataiinua kwa namna ya Kimisri."


9. Omba MUNGU afufue kazi yake ambapo ataasha roho za watu kwa ajili ya utumishi katika Injili ya KRISTO.


Habakuki 3:2 "Ee BWANA, nimesikia habari zako, nami naogopa; Ee BWANA, fufua kazi yako katikati ya miaka; Katikati ya miaka tangaza habari yake; Katika ghadhabu kumbuka rehema."

Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU la  siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.

MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

By Mwl Peter Mabula 

Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)

Ubarikiwe.

Comments