![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU Mwenyezi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.
Inawezekana hujaupenda ujumbe huu lakini Jifunze itakusaidia.
◼️ Kuingia katika Ndoa na Mtu wa dini nyingine ni vibaya zaidi ya kuingia katika Ndoa na mpagani.
◼️Usije kamwe ukaoana na mpagani, Wateule wa KRISTO wapo wengi funga Ndoa na mmoja wao, usioe mpagani Wala usiolewe na mpagani, ila Sasa ingawa mpagani hafai ila mwenye dini nje na KRISTO YESU ni mbaya zaidi kuliko mpagani, yaani mpagani ana heri kuliko mpinga KRISTO.
◼️Biblia Iko wazi sana juu ya hilo,
Kumbu 7:3-4 " binti yako usimpe mwanawe mume, wala usimtwalie mwanao mume binti yake. Kwa kuwa atamkengeusha mwanao mume asinifuate, ili wapate kuabudu miungu mingine; ndipo itakapowaka hasira ya BWANA juu yenu, naye atakuangamiza upesi."
◼️Biblia ipo wazi ya kwamba wale walio kinyume na MUNGU katika KRISTO YESU wako upande wa miungu.
Haijalishi zipo dini ngapi ila dini inayohusika na MUNGU wa Mbinguni aliyeumba Mbingu na Dunia ni dini mbili tu yaani Mkristo aliyeokoka pamoja na Myahudi ndio maana Wayahudi wanatumia Biblia vitabu vyote vya Agano la kale na Wakristo wanatumia Biblia Agano la kale na Agano jipya, nje na hapo ni watu kuabudu miungu.
Isaya 44:6-8 " BWANA, Mfalme wa Israeli, Mkombozi wako, BWANA wa majeshi, asema hivi; Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu.
Naye ni nani kama mimi atakayeita, na kuyahubiri haya, na kunitengenezea, tangu nilipowaweka watu wa kale? Na mambo yanayokuja na yatakayotokea, wayatangaze. Msiogope wala msifanye hofu; je! Sikukuhubiri haya zamani na kuyaonyesha? Na ninyi ni mashahidi wangu. Je! Yuko Mungu zaidi yangu mimi? Hakika hapana Mwamba; mimi sijui mwingine."
◼️Hivyo nje na MUNGU wa Mbinguni Kuna miungu tu haijalishi watu wengi wanaiabudu.
◼️Hivyo ukioana na Mtu asiye na Wokovu wa KRISTO ni zaidi ya kuoana na mpagani.
◾Kwanini nimesema maneno haya magumu sana Leo kwa baadhi ya watu?
Huu ndio ukweli wa Neno la MUNGU.
➡️Watu wa dini za mpinga KRISTO ni watu ambao hawaji katika Ndoa hivi hivi Bali huja kwa Missions zao za kidini.
◾Inawezekana hujanielewa, unamkumbuka Delilah aliyekuwa anaabudu miungu?
Waamuzi 16:23-24 " Kisha wakuu wa Wafilisti wakakusanyika ili kumtolea sadaka Dagoni mungu wao, na kufurahi; maana walisema, Mungu wetu amemtia Samsoni adui wetu mikononi mwetu. Na hao watu walipomwona wakamhimidi mungu wao, maana walisema, Mungu wetu amemtia mikononi mwetu huyu adui wetu, aliyeiharibu nchi yetu na kuwaua watu wengi miongoni mwetu."
➡️Delila alikuwa mfilisti na mungu wao alikuwa dagoni, harafu huyo mwabudu shetani ndio akaolewa na Mtumishi wa MUNGU Samson, Delila alikuja kwenye Ndoa kwa Mission Maalumu.
➡️Hata wewe Kijana Mkristo au Binti Mkristo ukioana na Mtu kutoka dini ya mpinga KRISTO ujue amekuja na mission ya kidini kwako, asipokupata Wewe atawapata Ndugu zako au Watoto mtakaozaa, hiyo itakuwa Haina faida kwako katika Ufalme wa MUNGU.
➡️Huyu Delilah alikuja kwenye Maisha ya Samson Mtu wa MUNGU ili kuondoa Nguvu za MUNGU ndani ya Samson, hivyo alikuja kwenye Ndoa na Samson kwa mission Maalumu.
◼️Hata wewe anaweza kutokea Mtu wa dini za mpinga KRISTO ili akuondolee Nguvu za ROHO MTAKATIFU kwenye Maisha Yako, ndio maana nikasema mpagani ana nafuu kidogo kuliko Mtu kutoka dini ya mpinga KRISTO.
◾Je unamkumbuka Jezebel?
Huyu ndio mwakilishi wa kiwango Cha juu zaidi wa wapinga KRISTO kuoana na watu wa MUNGU.
Huyu Yezebeli alipooana na Mtumishi wa MUNGU Ahabu alifanya mabaya mno.
➡️Kwanza alikuja kwenye Ndoa akiwa na miungu yake na dini yake ya mpinga KRISTO, hivyo alikuja kwenye Ndoa akiwa na mission kubwa sana na mbaya sana kwa watu wa MUNGU, kwanza akalazimisha nyumba ya Ibada ya kishetani ijengwe na ikajengwa.
1 Wafalme 16:32 "Akamjengea Baali madhabahu katika nyumba ya Baali, aliyoijenga huko Samaria."
➡️Baada ya hapo watu wenye Nguvu za MUNGU wa kweli alianza kuwaua ili Taifa Zima wabaki wapinga KRISTO, ni mission mbaya sana aliyokuwa nayo kupitia Ndoa tu.
1 Wafalme 18:4 "kwa kuwa ikawa, Yezebeli alipowaua manabii wa BWANA, Obadia akatwaa manabii mia, akawaficha hamsini hamsini katika pango, akawalisha chakula na kuwapa maji)."
◾Huyu alikuja kwenye Ndoa na mission yake ya kishetani.
➡️Ndivyo ilivyo kwa wapinga KRISTO wote huja kwenye Ndoa na Mkristo wakiwa na mission ya kidini ili kuwatoa Wakristo kwa MUNGU wa kweli ndio maana nikasema ni heri kuoana na mpagani kuliko Kuoana na Mtu wa dini ya mpinga KRISTO.
➡️Kumbuka mpagani hana dini hivyo ni rahisi kidogo kumfanya aokoke kuliko mwenye dini yake kumbadilisha.
➡️Sisemi kwamba uoe mpagani au uolewe na mpagani, Usifanye hivyo kamwe ila mpagani ana nafuu kuliko mwenye dini ila ni dini ya mpinga KRISTO.
◼️ Narudia Tena usije kamwe ukaoana na mpagani, Wateule wa KRISTO wapo wengine funga Ndoa na mmoja wao, usioe mpagani Wala usiolewe na mpagani ila Sasa ingawa mpagani hafai ila mwenye dini nje na KRISTO YESU ni mbaya kuliko mpagani.
◼️Kumbuka Wote wasio na YESU KRISTO wanaabudu miungu hivyo ni rahisi kukunasa Wewe na kukuhamishia kuabudu miungu yao.
➡️Andiko hapo juu Mwanzoni wa somo linasema "Watawakengeusha" yaani hao Wana Nguvu kubwa ya kukengeusha watu wa MUNGU ili wafuate miungu.
➡️Sasa kama mpagani hafai hata kidogo kuingia nae katika Ndoa huyo mpiga KRISTO ndio mbaya zaidi kuingia nae katika Ndoa, ndio maana nimesema kuolewa au kuoa Mtu wa dini nyingine ni vibaya kuliko kuoa au kuolewa na mpagani.
Biblia inakataza kufungwa nira Moja na watu wasiomwamini YESU KRISTO kama Mwokozi wao.
2 Wakorintho 6:14 "Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?"
➡️Nina marafiki zangu wawili Wanaume ambao walioa watu kutoka dini ya mpinga KRISTO na Leo Watoto wao wote wako dini ya mpinga KRISTO na hata wao ingawa Wana majina ya KRISTO ila hawaeleweki kama ni Wakristo au wapinga KRISTO, ni hatari sana.
Sasa Hawa ni Wanaume ila wamenaswa, kwa Mwanamke ni rahisi zaidi kunaswa maana Mke humilikiwa.
Wewe Mwanamke Mkristo ambaye hauko katika Ndoa Usikubali kamwe kuolewa na Mtu wa dini ya mpinga KRISTO.
➡️ Vijana na Binti wengi sana katika kizazi Cha Leo wanadangwa walidhani dini tofauti sio tatizo kumbe ni tatizo kubwa linaloweza kuathiri hadi Watoto Baadae, linaweza kuathiri hadi kizazi.
Wengine hudanganywa kwamba MUNGU ni mmoja kwa dini zote, huo ni uongo mbaya.
MUNGU wa Wakristo sio Mungu wa dini nyingine zote maana hizo ni dini za mpinga KRISTO.
1 Yohana 2:18 "Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho."
➡️Najua upendo una Nguvu sana ila upendo usisababishe ukose Uzima wa Milele, upendo usisababishe Watoto wako wamkose YESU hata wakose Uzima wa Milele, Ina maana gani uzae Watoto wa kwenda tu jehanamu?
➡️Wewe uliye Sasa kwenye Ndoa na mpinga KRISTO Hakikisha unabaki na YESU KRISTO na Hakikisha Watoto wako Wana YESU KRISTO, pia msaidie mwenzi wako aokoke, ndio maana Biblia inasema Mtu asiyemwamini YESU KRISTO hata akiondoka kwenye Ndoa Wewe hufungwi ukioana na Mtu Mwingine.
1 Wakorintho 7:15 "Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini MUNGU ametuita katika amani."
◼️Ushauri wangu usiachane na mwenzi mliyeoana ila asikuondoe kwa YESU KRISTO kamwe, kama itafika hatua ya ama umchague YESU KRISTO au umchague yeye ni heri muachane ili Wewe ubaki na YESU KRISTO Mwokozi.
◼️Nawajua pia watu wengi ambao walikuwa wapinga KRISTO ila wakampokea YESU KRISTO kama Mwokozi wao, hao wengi wao ni watu Bora sana na hao wanafaa sana kwa Ndoa Takatifu maana wengi wao wakimshika YESU hawamwachi kamwe, hivyo usiwaogope watu hao kwa ajili ya Ndoa Takatifu kama utapata Ufunuo wa MUNGU juu yao kwa ajili ya Ndoa.
◼️Ila Wewe ambao hauko kwenye Ndoa kamwe Usikubali kuingia katika Ndoa na mpinga KRISTO.
Narudia Tena hata kama anakuvutia kiasi gani na hata kama unampenda kiasi gani usioane na mpinga KRISTO, heri mwambie aokoke kwanza ni ujipe muda kujua kama kweli ameokoka.
Narudia Tena Usikubali kamwe kuoana na mpinga KRISTO.
Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe.

Comments