![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.
Karibu Tujifunze Neno la MUNGU.
➡️Wako Watu waliwahi kupitia hatari mbaya sana, wengine inawezekana unawafahamu na wengine huwafahamu, wengine umesimuliwa wengine umesoma kuhusu wao kwenye Biblia ,hiyo inakufundisha kwamba nyakati mbaya kuna wakati huwa zipo, ingawa sio kwa watu wote
Mhubiri 9:12 "Maana mwanadamu naye hajui wakati wake; kama samaki wanaokamatwa katika nyavu mbaya, na mfano wa ndege wanaonaswa mtegoni, kadhalika wanadamu hunaswa katika wakati mbaya, unapowaangukia kwa ghafula."
➡️Biblia inasema Kuna wakati mbaya na unaweza kuja ghafla kwa baadhi ya watu
Changamoto mbaya kwa baadhi ya watu wanapojikuta katika wakati mbaya hufuata mashetani na kupelekea kuangamia au kupelekea kupata nguvu za giza na kuanza kuteswa na hizo nguvu za giza.
Mfano hai ni huyu Asa.
2 Mambo ya Nyakati 16:12-13 "Akashikwa Asa na ugonjwa wa miguu katika mwaka wa thelathini na kenda wa kumiliki kwake; ugonjwa wake ukazidi sana; lakini hakumtafuta BWANA katika ugonjwa wake, bali waganga. Asa akalala na babaze, akafa katika mwaka wa arobaini na mmoja wa kumiliki kwake."
➡️Huyu alipatwa na wakati mbaya wa kuumwa lakini ajabu yeye badala ya kumtafuta MUNGU yeye akawatafuta waganga wa kienyeji na hiyo kupelekea kifo chake.
◼️Ndugu leo nina habari njema za nyakati zote hivyo nisikilize.
Katika wakati mbaya mwite YESU KRISTO anayeweza kukulinda na hali mbaya zote.
Zaburi 121:7" BWANA atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako."
◼️Huyu YESU aliweza kuwatoa katika nyakati mbaya watu wengi sana hadi Biblia inasema isingetosha vitabu vya kuandika Miujiza hiyo.
Yohana 21:25 "Kuna na mambo mengi aliyoyafanya YESU; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa."
◼️Huyo Pekee anaweza kukulinda katika nyakati mbaya.
Mkumbuke Yakobo ambaye aliambiwa atalindwa Kila aendako na ilikuwa hivyo hivyo.
Mwanzo 28:15 "Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia."
◼️Ndugu, mwite YESU KRISTO kwenye Nyakati zote zikiwemo Nyakati mbaya.
Na uzuri zaidi ukiokoka na ukaishi katika kusudi lake ndio kabisa anaweza kukulinda na kukupa majukumu katika Wokovu wake.
Isaya 42:6 "Mimi, BWANA, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa;"
◼️Huyu MUNGU anaweza kuweka Malaika wakulinde, kama aliweka Malaika kulinda ardhi Mfano alipoilinfa ardhi ya Edeni, Wewe ni ni Zaidi.
Mwanzo 3:24 "Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima."
◼️Ndugu, mwite YESU KRISTO kwenye Nyakati zote zikiwemo Nyakati mbaya zinazoweza kujitokea katika Maisha Yako.
➡️Mkumbuke Batimayo ambaye alipona na Nyakati ngumu kwake ilafika mwisho.
Marko 10:51-52 " YESU akamjibu, akamwambia, Wataka nikufanyie nini? Yule kipofu akamwambia, Mwalimu wangu, nataka nipate kuona. YESU akamwambia, Enenda zako, imani yako imekuponya. Mara akapata kuona; akamfuata njiani."
✔️✔️ Hata wewe unaweza kupona kama ukimwamini YESU na kuhitaji akuponye
Kumbuka Wote waliomfuata YESU yeye aliwaponya wote.
Mathayo 12:15 "Naye YESU hali akiyafahamu hayo akaondoka huko; na watu wengi wakamfuata; akawaponya wote,"
◼️Nini ufanye
1. Mpokee YESU KRISTO kama Mwokozi wako binafsi.
Yohana 1:12-13 " Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU."
2. Omba MUNGU kwa jina lake YESU KRISTO utapona.
Yohana 14:13 "Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili BABA atukuzwe ndani ya MWANA."
3. Nenda Kanisani ukaombewe kwa jina lake YESU KRISTO.
Yakobo 5:15 "Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na BWANA atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa."
Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe.

Comments