![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.
Karibu Tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
◼️Huyu anayezungumzwa katika ujumbe huu kwamba anayaweza mambo yote ni Kila Mkristo aliyeokoka, anaishi Maisha Matakatifu, na anaomba Maombi kwa Imani kubwa katika Jina la YESU KRISTO Mwokozi, hivyo Mtu huyo anaweza kuwa ni Wewe hivyo ingia ndani ya ujumbe huu Ukiwa ni Wewe binafsi.
Wafilipi 4:13 "Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu."
◼️Naweza kuwashinda mawakala wa shetani wote kwa kutumia Jina la YESU KRISTO nikiwa ndani yake.
1 Wakorintho 15:57 "Lakini MUNGU na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu YESU KRISTO."
◾Kwanini nayaweza mambo yote na kwanini naweza kushinda dhidi ya hila za shetani?
1. Ni kwa sababu YESU KRISTO amenipa mimi kinywa cha kuwashinda mawakala wa shetani katika ulimwengu wa roho.
Luka 21:15 "kwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga."
2. Ni kwasababu Neno la MUNGU lina nguvu ya kushinda majini wote na wachawi wote na hilo Neno ndilo liko ndani yangu na ninalitumia kwenye Maisha yangu na kwenye Maombi.
Matendo 19:20 "Hivyo ndivyo neno la BWANA lilivyozidi na kushinda kwa nguvu."
➡️Anayeniendea kwa waganga wa kienyeji anajisumbua tu na kujitaabisha maana MUNGU wa Mbinguni ameshanipa tayari kumshinda hata mganga kabla hata hajamwendea.
➡️Ndugu Mteule wa KRISTO ni kweli wachawi na watu wabaya wanaofanya vita na wewe lakini tangazo la Mbinguni kwako ni kwamba utashinda kwa Jina la YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai Milele.
Yeremia 1:19 "Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, asema BWANA, ili nikuokoe."
◼️Tunaposema mambo yote yanawezekana katika Jina la YESU KRISTO tuna uhakika maana MUNGU wa Daudi ndiye MUNGU wetu.
Kwa hali ya kibinadamu ya Kawaida ilikuwa haiwezekani Daudi Kijana Mdogo asiye na mafunzo ya kivita kumshinda komando Maarufu wa Wafilisti, lakini Daudi alishinda kwa sababu kwa Wateule wa MUNGU Kuna kuyaweza Mambo yote katika MUNGU atutiaye Nguvu, Goliathi hii Siri ya Wateule wa MUNGU alikuwa haijui ndio maana alipokuja kichwa kichwa aliishia kufa kwa pigo Moja tu dogo la kiroho.
1 Samweli 17:45-50 " Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la BWANA wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana. Siku hii ya leo BWANA atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko MUNGU katika Israeli. Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba BWANA haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya BWANA, naye atawatia ninyi mikononi mwetu. Ikawa, hapo Mfilisti alipojiinua, akaenda akamkaribia Daudi, ndipo Daudi naye akapiga mbio, akalikimbilia jeshi ili akutane na yule Mfilisti. Daudi akatia mkono wake mfukoni, akatwaa humo jiwe moja, akalitupa kwa kombeo lake, akampiga Mfilisti katika kipaji cha uso; jiwe hilo likamwingilia kipajini, akaanguka chini kifudifudi. Hivyo Daudi akamshinda yule Mfilisti kwa kombeo na jiwe, akampiga Mfilisti, akamwua; walakini Daudi hakuwa na upanga mkononi mwake."
◼️Hii sio kwangu tu Mimi Peter Mabula au kwa Daudi tu, hii na kwako pia uliyeokolewa na Bwana YESU KRISTO, utayaweza mambo yote maana MUNGU atakutia Nguvu.
◼️Ndugu endelea na YESU KRISTO utashinda na Zaidi ya kushinda.
Warumi 8:37 Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.
➡️Hata Farao hakuijua Siri hii iliyo na Wateule wa MUNGU tu kwamba "Watayaweza mambo yote katika MUNGU " Farao alipojaribu kupigana na watu wa MUNGU aliishia kufa na jeshi lake likaishia kufa baharini.
Kutoka 14:21-28 " Musa; akanyosha mkono wake juu ya bahari; BWANA akaifanya bahari irudi nyuma kwa upepo wa nguvu utokao mashariki, usiku kucha, akaifanya bahari kuwa nchi kavu, maji yakagawanyika. Wana wa Israeli wakaenda ndani kati ya bahari katika nchi kavu; nayo maji yalikuwa ukuta kwao mkono wa kuume, na mkono wa kushoto. Na wale Wamisri wakawafuatia, wakaingia ndani kati ya bahari, farasi zote za Farao, na magari yake, na wapanda farasi wake. Ikawa katika zamu ya alfajiri, BWANA akalichungulia jeshi la Wamisri katika ile nguzo ya moto na ya wingu, akalifadhaisha jeshi la Wamisri. Akayaondoa magurudumu ya magari yao, hata yakaenda kwa uzito; na Wamisri wakasema, Na tukimbie mbele ya Israeli; kwa kuwa BWANA anawapigania, kinyume cha Wamisri. BWANA akamwambia Musa, Nyosha mkono wako juu ya bahari, ili maji yarudi tena juu ya Wamisri, juu ya magari yao, na juu ya farasi zao. Musa akaunyosha mkono wake juu ya bahari, na kulipopambazuka, bahari ikarudi kwa nguvu zake; Wamisri wakakimbia mbele yake; na BWANA akawakukutia mbali hao Wamisri kati ya bahari. Yale maji yakarudi yakafunikiza magari na wapanda farasi, hata jeshi lote la Farao lililoingia katika bahari nyuma yao; HAKUSALIA HATA MTU MMOJA."
◼️Bahari ilikuwa upande wa Wateule wa MUNGU ndio maana ikagawanyika ili wapite na Neno la kuyaweza Mambo yote katika MUNGU liwezekane, na ikawa hivyo.
➡️Wakati wa Yoshua hata jua na mwezi vililazimika kuwa upande wa Wateule wa MUNGU ili washinde vita, na hapo utaratibu wa watu wa MUNGU kuyaweza Mambo yote katika MUNGU utaratibu huo ufanyike, na ikawa hivyo kweli.
Yoshua 10:12-13 " Ndipo Yoshua akanena na BWANA katika siku hiyo ambayo BWANA aliwatoa Waamori mbele ya wana wa Israeli; akasema mbele ya macho ya Israeli, Wewe Jua, simama kimya juu ya Gibeoni; Na wewe Mwezi, simama katika bonde la Aiyaloni. Ndipo jua likasimama, na mwezi ukatulia, Hata hilo taifa lilipokuwa limekwisha jipatiliza juu ya adui zao."
◼️Ndugu endelea na Wokovu ishi Maisha matakatifu,omba katika ROHO MTAKATIFU na tangaza ushindi kwa kinywa chako katika Jina la YESU KRISTO.
Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe.

Comments