SISI TUNAKWENDA KWA JINA LA YESU MILELE NA MILELE.

 

Peter na Jemimah Mabula 
Watenda kazi katika Shamba la MUNGU Mwenyezi 

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.

Karibu Tujifunze  Neno la MUNGU wa Mbinguni.


Mika 4:5 "Kwa maana mataifa yote watakwenda, kila moja kwa jina la mungu wake, na sisi tutakwenda kwa jina la BWANA, Mungu wetu, milele na milele."


◼️Sisi tutakwenda kwa Jina la MUNGU wetu Milele na Milele.

Hiyo ndio sifa ya watu wa kweli wa MUNGU katika KRISTO YESU inavyotakiwa kuwa.


➡️Leo Wapo watu wa kidunia huenda kwa majina ya miungu yao waliodanganywa kwenye dini zao za kishetani.


➡️Wengine wanatumikia miungu yao ambayo ni mizimu au maroho wa kuzimu lakini sisi Kanisa hai la YESU KRISTO tunamtumikia MUNGU wa Mbinguni ambaye ametupa Jina la YESU KRISTO. 


Matendo  4:12 "Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo."


➡️ Hivyo Ndugu Kama yupo mganga au mchawi anaenda kwa jina la miungu yake, Wewe nenda kwa jina la YESU KRISTO utamshinda.


➡️Mfano ni kwamba Zamani kulikuwa na Wafilisti ambao waliabudu miungu yao na kudhani hiyo miungu Ina Nguvu na itawaokoa mbele ya MUNGU wetu aliye hai, miungu ya Wafilisti ilianguka mbele  tu ya  Sanduku la Agano la MUNGU wetu wa Mbinguni.


1 Samweli 5:2-4 " Wafilisti wakalichukua sanduku la MUNGU, wakalitia katika nyumba ya Dagoni, wakaliweka karibu na Dagoni.

 Na watu wa Ashdodi, walipoamka alfajiri siku ya pili, kumbe! Dagoni imeanguka chini kifudifudi, mbele ya sanduku la BWANA. Wakaitwaa Dagoni, wakaisimamisha mahali pake tena. Hata walipoamka kesho yake asubuhi, kumbe! Dagoni ilikuwa imeanguka chini kifudifudi, mbele ya sanduku la BWANA; na kichwa chake Dagoni na vitanga vya mikono yake vyote viwili vimekatika, vipo vimelala kizingitini; Dagoni ikasalia kiwiliwili chake tu."


➡️Hata leo Wafilisti wapo, Wafilisti wa Leo wanaenda kwa jina la miungu yao ,sisi tunaenda kwa jina la MUNGU wetu wa mbinguni.


◼️Uzuri mmoja ni kwamba MUNGU wetu sisi tulio na KRISTO ndio MUNGU Pekee wa kweli na nje na Yeye hakuna MUNGU wa kweli.


Isaya 44:6 "BWANA, Mfalme wa Israeli, Mkombozi wako, BWANA wa majeshi, asema hivi; Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu."


➡️Mfano mmoja ni Goliath ambaye  alikuwa na miungu yake lakini Daudi alimshinda kwa sababu Daudi alikuwa amebeba jina la YAHWEH Mungu wetu .


1 Samweli 17:45-50 " Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la BWANA wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana. Siku hii ya leo BWANA atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko MUNGU katika Israeli. Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba BWANA haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya BWANA, naye atawatia ninyi mikononi mwetu. Ikawa, hapo Mfilisti alipojiinua, akaenda akamkaribia Daudi, ndipo Daudi naye akapiga mbio, akalikimbilia jeshi ili akutane na yule Mfilisti. Daudi akatia mkono wake mfukoni, akatwaa humo jiwe moja, akalitupa kwa kombeo lake, akampiga Mfilisti katika kipaji cha uso; jiwe hilo likamwingilia kipajini, akaanguka chini kifudifudi. Hivyo Daudi akamshinda yule Mfilisti kwa kombeo na jiwe, akampiga Mfilisti, akamwua; walakini Daudi hakuwa na upanga mkononi mwake."


◼️Sisi tuliookoka tutakwenda kwa Jina la YESU KRISTO Milele.

Tukiwa na Jina la YESU KRISTO tutashinda daima.


◼️Uzuri mmoja ni kwamba hakuna Jina lenye Nguvu kuzidi Jina la YESU KRISTO.


Wafilipi 2:10-11 " ili kwa jina la YESU kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa MUNGU BABA.


◼️Kwenye Jina la YESU KRISTO vitu vyote vya Mbinguni hutii, vitu vyote vya Duniani hutii na vitu vyote vya kuzimu hutii.

Kama vitu vyote vya Mbinguni hutii kwenye Jina la YESU KRISTO Ndugu unahitaji Jina gani lingine nje na Jina la YESU KRISTO?

Watu wenye akili wanalikimbilia Jina la YESU KRISTO Maisha yao yote.


Marko 10:28-30 " Petro akaanza kumwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe. YESU akasema, Amin, nawaambieni, Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili, ila atapewa mara mia sasa wakati huu, nyumba, na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele."


◼️ Ndugu, nenda kwa Jina la YESU KRISTO Milele na Milele.


➡️Hata kama Ndugu zako hawataki Wewe nenda kwa Jina la YESU KRISTO Milele na Milele.


➡️Hata kama Mke wako au Mume wako hataki Wewe nenda kwa Jina la YESU KRISTO Milele na Milele.


➡️Hata kama Wazazi wako hawataki, Wewe nenda kwa Jina la YESU KRISTO Milele na Milele.


➡️Hata kama Bosi wako na kazini kwako hawataki Wewe timiza majukumu Yako kwa usahihi huku ukienda kwa Jina la YESU KRISTO Mwokozi Milele na Milele.


◼️Amua kuishi ndani ya KRISTO bila kuangalia watu wanasemaje.


Matendo  17:28 "Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake."


◼️Ndugu, maamuzi ya kwenda uzima wa Milele ni Yako binafsi, hayana ubia na Baba au Mama au Mtu Mwingine yeyote hivyo mpokee YESU KRISTO kama Mwokozi wako ili uwe na sifa za kwenda na Jina la YESU KRISTO Milele na Milele.


Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU la  siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.

MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

By Mwl Peter Mabula 

Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)

Ubarikiwe.

Comments