TOFAUTI YA MTU MWENYE ROHO MTAKATIFU NA AMBAYE HANA ROHO MTAKATIFU.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.

Karibu Tujifunze Neno la MUNGU.


◼️Kuna watu Wana ROHO MTAKATIFU na Kuna watu hawana ROHO MTAKATIFU, watu hawa wawili ni tofauti, hawawezi kuwa sawa hata kidogo.


1 Yohana 4:2-3. " Katika hili mwamjua ROHO wa MUNGU; kila roho ikiriyo kwamba YESU KRISTO amekuja katika mwili yatokana na MUNGU. Na kila roho isiyomkiri YESU haitokani na MUNGU. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani."


Tofauti ni hizi baina na Mtu mwenye ROHO MTAKATIFU na Mtu asiyekuwa na ROHO MTAKATIFU.


1. Sifa ya kwanza ya Mtu mwenye ROHO MTAKATIFU ni kumkiri YESU KRISTO kuwa Mwokozi wake, anamkiri daima baada ya Kuokoka na katika Maisha yake ya Kila siku.


➡️Kinyume chake ni kwamba Mtu asiye na ROHO MTAKATIFU ni vigumu sana kumkiri YESU KRISTO kama Mwokozi wake.


2. Mtu mwenye ROHO MTAKATIFU humpenda YESU KRISTO kama Mwokozi wake, na sifa ya kumpenda YESU ni kumshuhudia kwa kinywa mbele ya watu, na hiyo ni kazi ya ROHO MTAKATIFU maana yeye kazi yake Moja ni kumshuhudia YESU KRISTO kama Mwokozi wetu.


Yohana 15:26 "Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa BABA, huyo ROHO wa kweli atokaye kwa BABA, yeye atanishuhudia."


➡️Kinyume chake ni kwamba mtu asiye na ROHO MTAKATIFU anamkataa YESU KRISTO kuwa Mwokozi wake.


➡️Ukiona watu wa dini yeyote wanaomkataa YESU au wanamchukia YESU KRISTO ni kwa sababu watu hao hawana ROHO MTAKATIFU.


3. Mwenye ROHO MTAKATIFU  Maisha yake yamejaa matunda ya ROHO MTAKATIFU.


Wagalatia 5:22-23 " Lakini tunda la ROHO ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria."


➡️ Kinyume chake ni kwamba Mtu asiye na ROHO MTAKATIFU hana matunda ya ROHO MTAKATIFU yaani hana upendo wa kweli, hana uvumilivu, amejaa hasira nyingi na hana kiasi, jambo dogo tu kwake linageuka vita kubwa.

Lakini pia watu wengine wasio na ROHO MTAKATIFU wamejaa matendo haya.


Wagalatia 5:19-21 " Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,

 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa MUNGU."


4. Mwenye ROHO MTAKATIFU ni mwenye kutubu hata inapotokea amekosewa, hii ni kazi ya Matunda 9 ya ROHO MTAKATIFU kama kutafuta amani, furaha, uvumilivu n.k


Waefeso 4:32 "tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na MUNGU katika KRISTO alivyowasamehe ninyi."


➡️Kinyume chake ni kwamba asiye na ROHO MTAKATIFU ana chuki, ni mgomvi na daima  anataka yeye ndio aombwe msamaha hata kama yeye ndio mkosaji.


5. Mwenye ROHO MTAKATIFU hupewa na ROHO MTAKATIFU kujua mambo ya baadae  yaani hufunuliwa mambo ya baadae.


Yohana 16:13 "Lakini yeye atakapokuja, huyo ROHO wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, NA MAMBO YAJAYO ATAWAPASHA HABARI YAKE."


◼️Mwenye ROHO MTAKATIFU hufunuliwa mambo mengi na ROHO MTAKATIFU.


1 Wakorintho 2:10 "Lakini MUNGU ametufunulia sisi kwa ROHO. Maana ROHO huchunguza yote, hata mafumbo ya MUNGU."


◼️Mwenye ROHO MTAKATIFU hupewa maelekezo na ROHO MTAKATIFU.


➡️Kinyume chake ni kwamba mtu asiye na ROHO MTAKATIFU hajui chochote.


➡️Mtu asiye na ROHO MTAKATIFU hujiendea tu hajui chochote na hupata madhara.


6. Mwenye ROHO MTAKATIFU karama za MUNGU hufanya kazi ndani yake.


1 Wakorintho 12:8-11 " Maana mtu mmoja kwa ROHO apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo ROHO yeye yule; mwingine imani katika ROHO yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika ROHO yule mmoja;

 na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha; LAKINI KAZI HIZI ZOTE huzitenda ROHO huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye."


➡️Kinyume chake ni kwamba Mtu asiye na ROHO MTAKATIFU karama za ROHO MTAKATIFU hazifanyi kazi kwake.

Mfano hawezi kuondoa mapepo kwa Maombi katika jina la YESU KRISTO, hawezi kumtumikia MUNGU n.k


7. Mwenye ROHO MTAKATIFU huenenda kwa ROHO MTAKATIFU.


Wagalatia 5:16 "Basi nasema, Enendeni kwa ROHO, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili."


➡️Kinyume chake ni kwamba Mtu asiyenaye anaenda kimwili yaani kwamba kuiba ni sawa, kwenda kwa waganga ni sawa, kutoa mimba ni sawa, kuzini ni sawa na kufanya Kila Uovu kwake ni sawa Kwa sababu hana ROHO MTAKATIFU.


8. Mwenye ROHO MTAKATIFU amejaa nguvu za MUNGU.


Warumi 15:13 "Basi MUNGU wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za ROHO MTAKATIFU."


◼️Mfano hai w Mtu aliyejaa Nguvu za ROHO MTAKATIFU alikuwa stephano.


Matendo  6:8 "Na Stefano, akijaa neema na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu."


✔️✔️Katika ROHO MTAKATIFU alifunuliwa hadi mambo ya Mbinguni.


Matendo  7:55-56 " Lakini yeye akijaa ROHO MTAKATIFU, akakaza macho yake, akitazama mbinguni, akauona utukufu wa MUNGU, na YESU akisimama upande wa mkono wa kuume wa MUNGU. Akasema, Tazama! Naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa kuume wa MUNGU."


◼️Mfano hai wa Mtu aliyejaa ROHO MTAKATIFU alikuwa ni Petro.


Matendo  4:8 "Ndipo Petro, akijaa ROHO MTAKATIFU, akawaambia, Enyi wakubwa wa watu na wazee wa Israeli,"


◼️Mfano hai wa Mtu aliyejaa ROHO MTAKATIFU alikuwa ni Paulo.


Matendo  13:9-11 " Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa ROHO MTAKATIFU, akamkazia macho, akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za BWANA zilizonyoka? Basi, angalia, mkono wa BWANA u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza."


➡️Kinyume chake ni kwamba Mtu asiye na ROHO MTAKATIFU amejaa nguvu za giza.


◼️Ndugu, mhitaji sana sana ROHO MTAKATIFU katika Maisha Yako.

Na ROHO MTAKATIFU utampata kwanza kwa kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na ishi katika yeye.

Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU la  siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.

MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

By Mwl Peter Mabula 

Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)

Ubarikiwe.

Comments