![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.
◼️MUNGU wa Mbinguni atakutetea hata kama Wanadamu wanasema hutafanikiwa au wanajua ndio mwisho wako.
◼️Bwana YESU KRISTO atakupa ushindi hata kipindi ambacho Wanadamu wanasema huwezi kushinda.
◼️Hata kipindi watu wote wamekukatia tamaa kuhusu jambo Fulani YESU KRISTO anaweza kukupa ushindi.
Zaburi 113:7-9 " Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Na kumpandisha maskini kutoka jaani. Amketishe pamoja na wakuu, Pamoja na wakuu wa watu wake. Huweka nyumbani mwanamke aliye tasa, Awe mama ya watoto mwenye furaha."
◼️Hata kama unaumwa na watu wote wanasema ni mwisho wako, YESU KRISTO anaweza kukuponya na kukupa kuishi.
Zaburi 102:19-20 " Maana ametazama toka patakatifu pake pa juu, Toka mbinguni BWANA ameiangalia nchi, Ili akusikie kuugua kwake aliyefungwa, Na kuwafungua walioandikiwa kufa."
◼️Ndugu, amua tu Kuokoka na kuishi maisha matakatifu ya Wokovu wa KRISTO YESU.
Mpokee YESU KRISTO utakuwa salama hata sehemu ambayo wote wanasema hutakuwa salama.
YESU KRISTO hakuanza Leo kuponya Kila udhaifu Bali tangu zamani hakuna ugonjwa Wala udhaifu wa Mtu yeyote unaoweza kumshinda Bwana YESU KRISTO.
Mathayo 4:23 "Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna katika watu."
◼️Ndugu Hakikisha umempokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na ishi Maisha Matakatifu katika Wokovu wake.
◼️Mwamini Bwana YESU KRISTO maana anaweza kufanya yale ambayo wengine wote wameshindwa.
Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe.

Comments