Posted by
Peter Mabula
- Get link
- X
- Other Apps
![]() |
Mtumishi Gasper Madumla |
SOMO : NAMNA PASAKA ILIVYO * Sehemu ya mwisho *
Haleluya….
Jina la Bwana Yesu lisifiwe…
Ninakukaribisha mpendwa tujifunze pamoja kwa habari ya PASAKA ili tunaposherekea sikukuu hii tujue ni nini tunasherekea.
PASAKA ni kufa na kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo ndani yetu,na sio
katikati yetu,wala pembeni yetu Bali ndani yetu.Ndani yetu ni katika
kilindi cha mioyo yetu,kwamba tuanze kukumbuka kifo chake na kufufuka
kwake kuanzia huko ndani,
Maana hakuna Yule aliyekufa kisha akafufuka siku ya tatu,
ISIPOKUWA NI MMOJA TU AMBAYE NI YESU KRISTO PEKEE.
PASAKA sio ile ya kutamkwa tu,
PASAKA ndio ukristo wenyewe.
Tunapozungumzia KIFO CHA BWANA YESU tunazungumzia MSAMAHA wa dhambi ulioachiliwa kwetu bure.
Sikia;
Yesu alikuwa sawa sawa na Baba ,pale ilipohitajika wa kumtuma Duniani
ili ifanyike upatanisho baina ya Mungu na wanadamu waliokuwa na dhambi,
Tunaona Bwana Yesu akajitoa,akaja Duniani na kuzaliwa chini ya sheria
kama mwanadamu wa kawaida ili atukomboe sisi tuliokuwa watu wa dhambi.
Ikiwa ndio hivyo basi ,tutakubaliana kuwa Ipo Neema na Rehema za Mungu
ndani ya kifo cha Bwana Yesu,kwa maana Yeye alijitoa kwa wengi
waliopotea,ili wapate UKOMBOZI.Tunasoma Luka 19 : 10 “ Kwa kuwa Mwana wa
Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea. “
Sikia;
Kilichopotea hapo ni USHIRIKA ( SPIRITUAL CONNECTION/BOND) baina ya
Mungu na watu wake baada ya anguko la dhambi ya wazazi wetu wa kwanza
Adamu na Hawa.
Na ndio maana baada ya dhambi Mungu anashindwa kumuona Adamu mahali anapotakiwa awe,
Tunasoma ;
Mwanzo 3 :9 :
“ Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? ”
Hapo haimaanishi kwamba Mungu alikuwa hamuoni kabisa,bali alikuwa
hamuoni katika Nafasi/position yake anayopaswa kuwa siku zote.
Okey ;
Leo inasikitisha sana kwa viongozi wa dini kuwasisitiza Waamini wao
kwamba kuingia katika mfungo na maombi kwa mwezi mmoja tu eti kwamba ni
mwezi wa TOBA,!
Je miezi mingine vipi ?
Sio miezi ya TOBA ?
Je inakuwaje basi mtu aishi kidunia miezi hiyo yote,kisha amgeukie Mungu kwa mwezi mmoja tu,?
Je kama akifa kabla ya mwezi huo ,inakuaje ?
.,Mbingu ataiona?
Labda ujiulize maswali hayo.
Hii ni makosa kwa kanisa,Kanisa lazima lifahamu kuwa Hakuna mwezi wa
toba bali miezi yote ni miezi ya TOBA,Na ndio maana tunatakiwa KUKUMBUKA
MSAMAHA WA DHAMBI ZETU KILA SIKU.
Wayahudi walikuwa na sikukuu
ambazo hazikuendelea katika agano jipya,lakini SIKUU YA PASAKA yenyewe
yaendelea maana waliambiwa waikumbuke siku ile walipotolewa Misri kwa
mkono wa Bwana,
Tunasoma Hesabu 9:2 ;
“ Tena, wana wa Israeli na washike sikukuu ya Pasaka kwa wakati wake ulioagizwa. ”
Pia Soma Kutoka 12: 14
.Katika agano jipya hatukumbuki utumwa wa Misri bali twakumbuka wokovu tuliopata kupitia BWANA YESU.( 1 Petro 1 : 18-19 )
Haleluya…
Ninampenda huyu Yesu wa Msalaba…
Jina la Bwana liinuliwe…
Wakristo wa leo wameichukua PASAKA kama sikukuu ya kula pilau na kufanya mambo yasiyokuwa hata na maana,
Bali mimi ninakuambia kuwa kwa habari ya PASAKA,kama ukiitafakari
vizuri waweza kulia machozi ukikumbuka namna ulivyokuwa
Mzinzi/Mwizi/Muabudu sanamu/Mtu wa mapokeo ya dini/Mlevi/Tapeli N.K.
Lakini sasa eti wewe ni mpendwa wa Bwana au wengine ni watumishi.Katika kiwango hicho tu yafaa umpe MUNGU Utukufu.
KUFA NA KUKUFUFUKA KWA BWANA YESU.
Wewe mpendwa ni lazima utambue kuwa BWANA MUNGU anakupenda sana kuliko
unavyompenda .Na ndio maana akakubali kufanywa laana pale msalabani kwa
ajili yangu na yako.
Tunasoma Galatia 3 : 13 :
“ Kristo
alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa ALIFANYWA LAANA KWA AJILI
YETU; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;”
Ili Yesu amwage damu yake alihitaji mwili,hivyo akauacha Uungu wake akawa sawa na mwanadamu ila hakutenda dhambi.
“ bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;
tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ”Wafilipi 2 :7-9
Biblia inasema tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, “alijinyenyekeza akawa mtii ”
Tazama hapo ndipo akakirimiwa jina la Yesu,kwa maana nyingine ni kwamba jina la Yesu latokana na UTII.
Hivyo ikiwa Bwana Yesu atafufuka ndani yako siku ya leo ,kitachofufuka ndani yako ni UTII,maana Yeye ni MTII.
Okey ;
Nilikuambia kuwa :
Waisraeli ,kilichowafanya wasipatwe na madhara ya kufiwa kwa wazaliwa
wao wa kwanza ilikuwa ni DAMU iliyopakwa kwenye nyumba zao,Hivyo DAMU
ilikuwa kielelezo cha utetezi wao kutopatwa na pigo lolote.Kwa maana
hiyo DAMU isingelikuwapo labda katika moja ya nyumba ya muisraeli,Basi
ni dhahili angelipata na pigo.
Tazama sasa katika PASAKA wetu
KRISTO,ameachilia DAMU yake iwe ULINZI wa kutopigwa na pigo lolote lile
kutoka kwa adui.Yeye aliyekuwa ndani ya Kristo hawezi kupatwa na pigo
lolote lile lijapokuja,
Tunasoma Hesabu 23 : 23:
“
Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli.
Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda
Mungu! ”
Hivyo PASAKA namna ilivyo sasa ni tofauti na jinsi
anavyotakiwa iwe,Mungu anatutizamia kwamba tukumbuke wema na fadhili
zake pamoja na upendo wake wa kututoa sehemu chafu ya dhambi na kutuleta
katika msamaha wa pendo lake
.Wakolosai 1 : 13-14 :
“ Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;
ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi; ”
Ili Bwana Yesu afufuke ndani yako ni lazima umkubari awe Bwana na
Mwokozi wako kwa kinywa chako mwenyewe.Sasa na ukiwa kama bado
hujampokea Bwana Yesu Kristo awe Bwana na mwokozi wa maisha yako ,basi
wakati ndio huu ili Bwana Yesu afufuke na wewe siku ya leo,waweza
kufuatisha sala hii;
Sema,
Bwana Yesu Kristo,mimi ni mwenye
dhambi ninakiri kwa kinywa changu ,ninaomba unisamehe makosa yangu
yote,ninayoyakumbuka na nisiyoyakumbuka,ninayoyajua na
nisiyoyajua,unifute jina langu katika kitabu cha hukumu,na uandike jina
langu katika kitabu cha uzima.
Ongera kwa kuokoka,na Bwana Yesu sasa atafufuka na wewe mpendwa.
MWISHO.
UBARIKIWE.
- Get link
- X
- Other Apps

Comments
Mwanzoni, nilikuwa na shaka, lakini kitu kuhusu maneno yake kilinipa amani. Aliniambia haswa kilichokuwa kibaya na kwamba mtu alikuwa ametupa uchawi mkali kututenganisha. Aliandaa kazi maalum ya kiroho na uchawi wa kuungana tena kwa ajili yangu - na ndani ya siku chache, mume wangu alinipigia simu ghafla, akilia na kuomba msamaha.
Tangu wakati huo, maisha yangu hayajawahi kuwa sawa. Ndoa yetu sasa ni tamu na yenye furaha zaidi duniani. Tunapendana zaidi kuliko hapo awali, na nyumba yetu imejaa vicheko na baraka.
Lakini sio hivyo tu - Dkt. Dawn pia alisaidia kuondoa bahati mbaya na nishati hasi iliyozunguka familia yetu. Tangu wakati huo, kila kitu kimekuwa laini: amani nyumbani kwetu, maendeleo ya kifedha, afya njema, na furaha safi.
Ninashukuru ulimwengu kila siku kwa kuniongoza kwa Dkt. Dawn. Kwa kweli ni mtu mwenye nguvu na mwanga wa kimungu. Ikiwa unapitia hali yoyote - huzuni, bahati mbaya, au kuchanganyikiwa - usikate tamaa. Mfikie na uache ulimwengu ufanye kazi kupitia yeye ili kubadilisha hadithi yako, kama vile alivyobadilisha yangu.
Wasiliana naye kwenye WhatsApp: +2349046229159 dawnacuna314@gmail.com
Niliwasiliana na Dkt. Dawn wakati uhusiano wangu ulipovunjika kabisa. Mpenzi wangu wa zamani alikuwa ameniacha na kunizuia kwenye mitandao yote ya kijamii. Nilivunjika moyo na kupoteza tumaini. Baada ya kushauriana na Dkt. Dawn, kila kitu kilibadilika. Mpenzi wangu wa zamani alirudi peke yake, akaomba msamaha kwa dhati, na akaomba msamaha. Leo, tunaishi pamoja kwa furaha, na hata tuna mtoto.
Maneno hayatoshi kuelezea jinsi ninavyoshukuru. Kutokana na uzoefu wangu, naweza kusema kwa ujasiri kwamba Dkt. Dawn ni halisi, anayetegemewa, na mwenye nguvu. Ikiwa unakabiliwa na hali yoyote ngumu maishani mwako hivi sasa, Dkt. Dawn anaweza kukusaidia.
ANAWEZA KUKUSAIDIA KWA MATATIZO YAFUATAYO:
Kurudisha ndoa na mahusiano yaliyovunjika
Kuvutia mafanikio na ukuaji katika biashara
Matatizo ya uanaume, utasa, na ukosefu wa watoto
Kurejesha mali zilizoibiwa au zilizopotea
Kurudisha kazi zilizopotea au fursa za kazi
Kinga dhidi ya uchawi na macho mabaya
Hirizi za mvuto
Kutatua migogoro ya ardhi na mali
Kuwafanya wapenzi kutimiza ahadi zao
Kushinda kesi mahakamani, na mengine mengi
Huu si ulaghai — ni ushuhuda kutoka kwa uzoefu.
Kwa maelezo zaidi, wasiliana naye moja kwa moja kwenye WhatsApp. +2349046229159. dawnacuna314@gmail.com