Kanisa la P A G kigamboni vijibweni mambo safi, wafanya ubatizo, BWANA YESU akiwainua kutoka utukufu hadi utukufu kihuduma.

Kanisa la Pentecostal Asemblies of GOD (PAG)  Vijibweni soweto chini ya mpakwa mafuta wa BWANA Mchungaji Eliza Kihwili  linaendelea kupanuka na na wengi kuokolewa, pamoja na hoyo  mwisho wa wiki iliyopita walibatizwa vijana 9 kanisani hapo.

Mchungaji Eliza ambaye historia ya maisha yake ni ya ajabu sana  maana pamoja na kuishi bila figo moja lakini MUNGU ameendelea kumtumia na kumbariki  na sasa kanisa hilo linakuwa kwani kwa mujibu wa mcungjai Elizabeth sasa kuna waumini zaidi ya 35 katika ibada moja na MUNGU amekuwa akiwaleta watu wengi. Huduma hiyo ambayo hata miaka miwili haijamaliza inaendelea kwa kasi kubwa huku BWANA akiwa amewabariki  kiwanja kikubwa sana pamoja na vyombo vya kisasa kabisa vya mziki .

Pamoja na mafanikio hayo furaha nyingine ni kwamba miezi michache iliyopita wamefanikiwa kuanzisha kwaya ya kanisa pamoja na kuchagua viongozi wa vijana  na lengu kubwa la Mchungaji huyo ni zaidi ya waumini 400 waabudu pamoja kanisani hapo.

Licha ya BWANA kumwita katika huduma wakati ambapo yuko kwenye majaribu ya ugonjwa lakini MUNGU ni mwaminifu sana na kazi aliyoianzisha ndani ya huduma hiyo , yeye BWANA ataitimiza.

Hizi hapa ni baadhi ya picha za ubatizo wa kihitoria katika kanisa hilo . Ubatizo ambao ulifanya na Mchungaji kiongozi wa Kawe Pentecostal Church, Mchungaji Elly Boto. kama kawaida Maisha ya ushindi tulikuwepo na sasa tunakuletea matukio katika picha kwenye ibada hiyo ya ubatizo.


Safari yetu ilianzia hapa kigamboni stend.
Wana wa MUNGU safarini kuelekea baharini kwenye ubatizo.



Hapa ndio tunafika baharini tayari kwa ibada ya ubatizo.

Niko ndano ya YESU nakula raha, niko ndani ya YESU naburudika.

Mchungaji Elizabeth Kihwili akiwatizama vijana wa kanisani kwake wakibatizwa.

Neno la MUNGU ndio kweli inayodumu milele. Hapa Mchungaji Boto akisoma neno la utangulizi kabla ya ubatizo.

Tunamhitaji MUNGU na nguvu zake.

Mchungaji Elly Boto akimsihi MUNGU juu ya wateule wa YESU ambao dakika chache zilizofuata walibatizwa.

Tuko tayari kumtumikia BWANA YESU

Tuko tayari kuitimiza haki ya MUNGU kwa kubatizwa.



Nakubatiza kwa jina la MUNGU BABA, MUNGU MWANA NA MUNGU ROHO MTAKATIFU.

Niko tayari kwa kumtumikia BWANA YESU.


YESU akikuweka huru , hakika unakuwa huru kweli kweli.

Ni furaha sana kubatizwa ubatizo wa maji mengi kama walivyobatizwa watu wa MUNGU wa zamani.


Niko tayari kwa kubatizwa.

Askari wa BWANA YESU baada ya kuitimiza haki ya MUNGU kwa kubatizwa.

Blogger kutoka maisha ya ushindi blog nilikuwepo katika zoezi hilo. Hapa nikiwa na Pastor Elly Boto(Katikati) pamoja na viongozi wengine wa kanisa.

Waliobatizwa katika picha ya pamoja baada ya kubatizwa

Waliobatizwa wakiwa katika picha ya pamoja na Mchungaji wao Elizabeth Kihwili pamoja na mchungaji kiongozi Elly Boto kutoka Kawe KPC
Maisha ya ushindi tunawapa hongera sana kwa kubatizwa ndugu hawa. Ubatizo ni jambo la kimungu na ubatizo ni muhimu kwa kila mtu aliyemkiri BWANA YESU kuwa BWANA na MWOKOZI wa maisha yake. na kama hukuwahi kusoma habari kumhusu Mchungaji Eliza FUNGUA HAPA

Comments