Ni kwa nini MUNGU aliichagua Israeli kuwa taifa lake teule?


BWANA YESU asifiwe ndugu.
Karibu katika tafakari hii.

  • Ni kwa nini MUNGU aliichagua Israeli kuwa watu lake wateule?


    Yawezekana umewahi kujiuliza juu ya jambo hilo.
    Yawezekana hujapata majibu kibinadamu , lakini mimi leo nataka tuangalie Biblia inazungumzia nini juu ya jambo hili.

    Kumbumbuku La Torati 7:7-9  inasema “BWANA hakuwapenda ninyi, wala hakuwachagua ninyi, kwa sababu mlikuwa wengi kuliko mataifa yote, maana mlikuwa wachache kuliko watu wote; bali kwa sababu BWANA anawapenda, na kwa sababu alitaka kuutimiza uapo wake aliowaapia baba zenu, ndiyo sababu BWANA akawaatoa kwa mkono wa nguvu, akawakomboa katika nyumba ya utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri. Basi jueni ya kuwa BWANA, MUNGU wenu, ndiye MUNGU; MUNGU mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kusika amri zake, hata vizazi elfu.”

    MUNGU alilichagua taifa la Israeli kuwa watu ambao kupitia kwao YESU KRISTO atazaliwa- mwokozi kutoka kwa dhambi na kifo (Yohana 3:16).

    MUNGU kwanza aliahidi kuja kwa masihi  baada ya Adamu na Hawa kuanguka katika dhambi ( Mwanzo mlango wa 3).

    MUNGU baadaye alithibitisha kuwa Masihi  atakuja kutoka kwa uzao wa Abrahamu, Isaka, na Yakobo (Mwanzo 12:1-3).

    Kwa hiyo YESU KRISTO ndiye sababu kuu ya MUNGU kuichagua Israeli kuwa watu wake malaamu.

    MUNGU hakustahili kuwa na watu wateule, lakini aliamua kufanya namna hiyo. YESU alistahili kuja kutoka kwa taifa la watu fulani na MUNGU  akachagua Israeli kupitia kumchagua Ibrahimu.

    Ingawa, sababu ya MUNGU kuichagua taifa la Israeli halikuwa  lengo  pekee la kumtoa YESU KRISTO. Nia ya MUNGU kwa Israeli ilikuwa kwamba wataenda na kuwafunza wengine kumhusu yeye.

     Israeli ilikuwa iwe taifa la makuahani, manabii na wamisionari kwa ulimwengu. Nia ya MUNGU ilikuwa, Israeli iwe watu wa kipekee, taifa ambalo lingeelekeza wengine kwa MUNGU aliye hai na ahadi zake, kutolewa kwa mkombozi, Masihi na mwokozi.

    Kwa sehemu nyingi Israeli ilikosea katika jukumu hili. Hata hivyo lengo lake kabisa kwa Israeli- lile la kuleta MKOMBOZI katika ulimwengu- lilitimizwa kikamilifu katika KRISTO YESU. na ambapo ''Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12 

    "Magen David" au nyota ya Daudi ni ishara ya Uyahudi

    Ukitaka KUJUA SIRI YA ISRAEL FUNGUA HAPAMUNGU wa Israeli awabariki sana na kama hujaokoka ndugu fanya hivyo leo maana hakuna uzima wa milele kwingine nje na BWANA YESU (Yohana 14:6-YESU akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa BABA, ila kwa njia ya mimi. , PIA Matendo 4:12-Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. ), BWANA YESU anakuhitaji ndugu ambae hujampokea maana alikufa mara moja ili wewe uwe hai milele katika yeye. Mpe maisha yako leo.


                                        MUNGU akubariki sana


                       Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula


                                Maisha ya ushindi Ministry.


                                               0714252292


                 HAKUNA ALIYE KAMA MUNGU WA ISRAELI.


                                            Amen.

Comments