ABE SULEIMAN:KWA NINI NILIAMUA KUACHANA NA UISLAMU NA KUWA MKRISTO? (5),

Na Abel Suleiman Shiriwa.
 Ushuhuda wa ajabu sana unaendelea, na kama kukusoma sehemu zilizotangulia basi Sehemu ya kwanza FUNGUA HAPA Na Sehemu ya pili FUNGUA HAPA Na kwa sehemu ya tatu FUNGUA HAPA.
Kwa sehemu ya 4 FUNGUA HAPA
Ilipoishia:
Wislamu tukaona hapa kumeshachafuka, Hapa Mtume (S.a.w) anaenda kutukanwa, Kabla JAMAL, hajasema chochote Waislamu tukavamia Ile Meza ya Maswali, tukamshika Jamal ili tumuinue katika meza maana amemtukanisha Mtume (S.a.w) yeye badala ya kuingia kwenye mada ambayo ilikuwepo ya Issa siyo Yesu, yeye akaenda kwenye hoja ya wachungaji mbwa, ambayo ilipelekea mpaka Mwenyezi Mungu, na mtumewe, waitwe Mbwa, Wakati tunataka kumtoa, Wahadhriri wengine, wakasema mwacheni, huu ni mjadala, kwa hivyo kama mtamuondoa, mtawapa nguvu hawa makufari, niliposikia hivyo, nikaona hapa hapafai tena kukaa, nikaamua kuondoka zangu kwenda HOME, Ahmad yeye alibaki pale, me kufika home, nikaanza kutafakari, hivi yale maandiko ambayo yamesomwa pale, ni ya kweli? Allah na Muhammad ni wachungaji Mbwa? Wakati huo sikuwa na Quran iliyotafsiriwa kwa kiswahili, na wakati huo Niko pale Thaqaafa, hatuwa tukifundishwa Tafsiri ya Quran, kwa hivyo kuna baadhi ya aya ambazo nilikuwa nazijua maana yake, kupitia maustadh mbali mbali, Nikaazimia kuitafuta Quran, lakini sikuwa na hela ya Kununua, nikasema, nitafanya mpango niipate, Mida ya kuswali ilipofika, nikaenda msikitini, Nilipotoka hapo, nikaenda kwa kina Ahmad, li nimuulize kuhuhusu kilichoendelea pale, sikumkuta, nikasema basi nitarejea baada ya Swala ya Isha, na kweli baada ya mida hiyo nikamkuta, nikamuuliza, “Leo Swala ya Magharibi umeiswalia wapi?” akasema, “Msikiti wa Kirumba, baada ya Muhadhara wa makafiri wale, Masheikh walituambia twende msikitini wanataka kuongea nasi” Nikamuuliza, “Wamesemaje sasa?” akasema.

Wamesema kuwa, inabidi twende kushitaki, kwa Muhammad kuitwa Mbwa, Wengine wakasema, Pale zimetolewa hoja za kimaandiko, kushitaki kwa kesi hiyo itakuwa ni vigumu, maana ushahidi wanao, hapa cha kufanya twende tukaseme, wamesema Mtume Muhammad (S.a.w) Ni Malaya, na alikufa kwa Ukimwi” wengi walikubaliana na shauri hilo, Nikamuuliza, ‘Kwani maneno hayo yalisemwa Nilipoondoka?” Ahamad akasema, “Hapana, hawakusema, ilani njia ya kuwazuia wale wasiendelee kuusema Uislamu” Nikasema poa, Akanisindikiza mpaka home, nikaingia ndani yeye akarudi zake home, Kichwani mwangu nikawa bado natafakari, kuna niNI NYUMA YA PAZIA?” kwa nini mashitaka yasiwe yale ambayo yamesemwa na watu wakasikia, Je ni kweli sifa zale za Uchungaji Mbwa, zinamuendea Muhammad?” Nikajipa moyo kuwa huenda ni maneno ya kubuniwa tu na Makafiri, Ule Muhadhara haukuchukua siku nyingi, ukazuiwa, Kina SIMBA ULANGA, wakahamia pale katika Kanisa la AICT makongoro, (Ambamo Mzee aliingia wakati wa kuwakimbia Polisi) siku hiyo nilipojua wako pale, nikasema, basi ngoja nami, niende nikaulize maswali, nione kama wataniburuza kama walivyomburuza IDDY na Jamal, kufika pale nikakuta wamo ndani ya FENSI, nikasita nikasema, Hawa Mkafiri wasije wakaninyongea mle ndani, nikaondoka zangu, nikaacha kufuatilia Muhadhara ule, siku moja natoka Madrasa, Thaqaafa, mida ya saa 11 Jioni, nikiwa kwenye Gari, nilikuwa Dirishani mkono wa kushoto, ukiwa unaelekea GHANA, nikasikia kwa mbali sauti ya Mazinge, kufika pale msikitini, nikaona umati wa Waislamu wamesimama, na wengine wamekaa, nikasema, Yes, hapa lazima patakuwa na Muhadhara, Kufika miSSION Nikashuka zangu, kisha nikaanza kurejea nyuma, kurudi kwenye Msikiti wa Makongoro, na kweli nikwakuta Wahadhri akiwemo Mazinge, kulikuwa na Mkristo mmoja walikuwa wanahojiana nae, wakawa wanambana, lakini nilivyomchunguza nikajua huyu huyu hayumo miongoni mwa wale wahubiri wa Kikrsto, maana hata maandiko mengi hakuwa anayajua, Nikajiuliza, “Kwa nini Wahadhiri hawa wasiende kule Kwa Wakristo wakajadiliane, ili sisi tupate kujua nani zaidi?”
Nikakaa pale mpaka Muhadhara ukaisha, nikatoka mdogo mdogo kwa miguu mpaka home, nikachukua Biblia yangu ya AGANO la Kale, nikawa najisomea maandiko ambao nimeyaandika kutoka kwa Wahadhiri wa Kiislamu, nilikuwa nasoma vipande tu vile ambavyo nilikuwa naviandika, kesho yake siku ya Ijumaa, hatukuwa tukienda Madarasa, kwa ajili ya maandalizi ya Swala ya Ijumaa, Nilipomaliza kuswali, nikasema, hapa ngoja nikae nitengeneze maswali, kwa ajili ya kwenda kuwauliza Wakristo, nikasema potelea Mbali, hata kama wamo kwenye Fensi, nitaingia hivo hivyo, liwalo na liwe, kweli mida ya saa 10 Jioni, nikaingia zangu pale, nikawa nje pale, nikawakuta ndo wanaanza kupeleka somo, Nakumbuka lilikuwa somo la “Majini ni ndugu za Waislam” kwa mara ya kwanza nikasikia, ikisomwa HADITHI hii.
Kasema Mtume (s.a.w) “Anamwijia mmoja wenu shetani katika sala, basi anapuliza (anampuliza) katika matako yake, basi yule mtu inamwijia fikiria ya kuwa umemtoka upepo (kajamba) nae haukumtoka, basi akiona hali hiyo asiondoke kwenye sala mpaka asikie sauti ya kumtoka huo upepo au anuse harufu yake”. (KITABU CHA MKWELI MWAMIU, JUZUU YA 1 -2 HADITHI NA. 74, UK 42)
Nikastuka sana pozi la kwenda kuuliza maswali, Likainiisha, kusikia kumbe Waislamu tunaposali, shetani, hutupuliza katika matako yetu, na kikavuta picha, ni mara nyingi Waislamu huwa kuna hali ya mtu kuondoka katika swalakwa kusikia kijambo, na kwennda kutawadha tena, hata kama ni Imamu, nikajua kumbe, huwa siyo Vijambo, bali shetani ndiye mwenye kutupuliza matakoni, Nikaondoka, fasta, kwenda Kwenye Muhadhara wa Waislamu, ili nikawaulize kama wana hicho kitabu, ili nikisome, nihakukishe kweli kuwa, “Matako yetu sisi Waislamu, ni sehemu ya shetani kufanyia michezo yake ya Kupuliza?” Kufika pale, nikasogea katika meza ya Wahadhiri nikawakuta wana Biblia NA Quran tu, nikashangaa nikajiuliza, mbona wale Wakristo, wana lundo la vitabu vya Kiislamu kwenye meza yao, lakini huku kwetu kuna Bibila na Quran tu? Nikasubrir muhadhara uuishe, Nikamfuata Sheikh Abdulrahman, nikamwambia, “Sheikh nimesikia pale kwenye Mhadhara wa Wakristo, kumesomwa kitabu cha Hadithi, kimesemwa sisi Waislamu tunapulizwa katika matako yetu na shetani wakati wa kusali, Kitabu Kinaitwa MKWELI MWAMNINIFU, JUZUU YA 1-2 HADITHI NA. 74 Uk. 42, kuna ukweli gani hapo” Sheikh akaniambia, “Hao Mkafiri siku hizi wanaandika vitabu vyao kwa ajili ya kudhalilisha Uislamu, hicho kitabu kimechukua jina moja wapo la Mtume, lakini, Si cha Kiislamu”
Nikamsikiliza, haikuniingia akilini, nikarudi home, sikwenda kusali siku hio Swala ya Magharibi, wala Swala ya Isha, Kesho yake, nikaenda kwenye Maduka ya vitabu vya Kiislamu, nikauliza kama kitabu hicho wanacho, wakasema, kipo KITABU cha MKWELI MWAMINIFU JUZUU YA 3-4 Hicho ambacho unakitaka wewe vilikuwepo vitatu na vyote vimechukuliwa, Nikaondoka, nikawa nimepata Jibu kuwa, kumbe Masheikh huwa wanatuficha mengi, maana kama SHEIKH ABDULRAHMAN, AMENIAMBA KUWA NI KITABU CHA MAKAFIRI SASA NI VIPI kiuzwe katika maduka ya vitabu vya Kiislamu? Wakati natembea huku naondoka, nikasema, ngoja nirudi kwenye vitabu, ili nikisome kwa juu nione kimeandikwa na nani? KWELI nikarudi, Nikamomba anipe hicho kitabu cha Mkweli Mwaminifu Juzuun ya 3-4 Nikiangalie kilivyo, akanipa, nikaona MWANDISHI wake, Ni SHEIKH MOHAMED ALLY KINDY, wasambaji ni Uongofu TANGA, NI FUKA LA Vitabu vya Kiislamu, lipo TANGA, Nikakirudisha nikaondoka zangu, nikasema, Kuna haja kubwa sasa kuhudhuria kwenye Mikutano ya Wakristo, ili nijifunze mengi kuhusu Uislmu, Nikawa kila siku naenda pae, baadae Kina SIMBAULANGA wakaondoka wakamwacha ERNST, akawa ndiye Mwalimu wa Kikrsto, wakati uo anaachwa pale, hakuwa mwalimu mzuri sana kama walivyokuwa Kina SIMBA ULANGA kwa wakati ule, nilikaa kwa muda bila kuona Mihadhara, baadae, nikaja kusikia kuna Muhadhara, pale KONA YA BWIRU, katika Kanisa la Baptist, nikaenda pale, nikamkuta Ernest, nikasema, Yes, nami nimepata mnyonge wangu wa kujiburuzia, maana nilishamshuhudia akiluliza maswali kwenye Mihadhara ya Kiislamu, akawa anabanwa, na wakati mwingineanajenga hoja nzito, kwa hivyo nikawa namuliza maswali, wakati mwingine anashindwa kujibu, basi me naondoka kwa Takbiira, huku waislamu wakinisindikiza.
Nikapata Kjulikana sana kupitia Ernest, wakati mwingine naenda pae, nabnwaa vibaya, kwa aibu, naishia tu kutukana, kadiri siku zilivyozidi kusonga mbele ndivyo Ernest alivyokuwa anazidi kuwa Mwalimu mzuri, Mimi nikawa nachemka, kwake, Kina Omary Mussa ambao nao walikuwa tegemeo nao pia wakawa wanachemka,BAADAE AKAJA TENA Daniel Mwankwemwa, akawa anafundisha pamoja na Ernest, KunA SIKU NILIENDA pale, nikiwa najiamini kabisa hapa ni lazima nitashinda, lakini mambo yakwa tofauti, piaKuna siku moja nilikuwa natoka Kitangiri, Naeleka kwenye Muhadhara, pale Kona ya Bwiru, nikakuta kuna vurugu, Nikawakuta Wakristo wanawarushia mawe Polisi, nikasema, ‘Kumbe Makafiri nao wanaweza kuanzisha zali” Sikujua tatizo ni nini, ikabidi nimafute mtu pale nikauliza, kulikoni, akasema, ‘Mwankemwa alikuja kukamwatwa, ndo kukatokea vurugu hii, maana Waislamun wao wakifanya Mihadhara yao hawakamawti, ili Wakristo ndo tunakamwatwa” Nikakumbuka yale aloniambia Amad, kuwa mashitaka kwa Wakristo yawe, wamesema Muhammad ni Malaya, Ila niliumia kuona Muhadhara unafungwa, maana ilikuwa ni sehemu yangu ya kuulizia maswali, Ila ule Muhadhara, uliruhusiwa na ukandelea, Mimi na Ahmad kama kawaida kwenye kuuliza maswali, kuna siku naelekea hapo, nikasikia Kuna mtu anaongozwa sala ya toba, nikakimbia ili niwahi kufika pale, nikamkuta dogo mmoja anaitwa Hassan, alikuwa anaishi na Issa Kalenga, ndo anaokoa pale, nilikasirika, nikasema, huyu lazima nimtafute nimchome kisu, maana Murtad hukumu yake ni kifo tu, lakini Mungu alimficha, sikuwahi kuonana nae, mpaka pale nilipoachana na uislamu ndo nikaja kuonana nae, nilivyoendelea kuuliza maswali, zile ambazo nilikuwa nazichukua kutoka kwa kina Mazinge, nikawa nabwana nazo, mpaka nikwa nahisi kama hawa Wakrsto ni wachawi…. Nikaamua sasa ngoja niakae nianze kusoma vema, nikamfuata SHEIKH JABIRI KATURA, nikamuomba aninunile quran ya Kiswahili, kweli akaninulia,
Nikaanza kuichambua quran na Biblia, Nikasema, ngoja niangalie yupi mwenye hadhi ya juu kati ya Yesu na Mtume wangu, maana masomo ambayo walikuwa wanayatoa Wakristo, nilikuwa nayachukulia kama uongo, ila niliponunua quran ya tafsiri nikagundua kuwa hawakuwa waongo, BIBLIA nikaanza kuisoma kuanzia Mathayo, nikasema mpaka nifike Ufunuo, nikawa naisoma, Nilichokuja kugundua ni kuwa, Waislamu tunaamnishwa kuwa Yesu,yupo chini ki ubora kuliko Muhammad, Ila ukisoma maandiko, utagundua si kweli, mfano mzuri tu ni huu hapa.
Qur’an 46;9 (Surat Al-Ahqaf) Sema; mimi si kiroja (mpya) katika mitume wala sijui nitakavyofanywa, wala mtakavyofanywa ninyi, sifuati yaliyofunuliwa kwangu, sikuwa mie lolote, ila ni muonyaji tu ninayedhihirisha.
Hapa nilikuwa tukisoma kwa kiarabu lakini sikuwa najua maana yake, lakini baada ya kufutilia kwenye quran ya Kiswahili, nikasema, kumbe Muhammad, hajui hatima yake siku ya Mwisho, hajui atafanya nini yeye wala sisi tunaomfuata, Lakini Yesu yeye alisema haya kwa watu wake,
Yohana 10;27-28 27 Kondoo wangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata. 28 Nami nawapa uzima wa milele, wala hawatapotea kamwe, wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.
Ikiwa Yesu yeye Kondoo wake anawajua, tena amesema anawapa Uzima wa Milele, sasa inakuwaje hapo kwa Muhammad? Nikaanza kupata mashaka makubwa sana na Uislamu, mfano mzuri kwa mtu ambae anasoma hapa, hata kama ni muislamu, hebu tafakari hili.
Waislamu, tulifundishwa kuwa, Muhammad, yeye ndiye Kipenzi cha Mwenyezi Mungu, na ndiye Mbira wa Mitume na Manabii wote, yaani Yesu, Mussa, Ibrahimu, Na wengineo, Wapo chini kwa ubora, dhidi ya Muhammad, na Kwa mujibu wa Quan, tunafundishwa kuwa Issa hajafa, Isipokuwa Mungu alimnyanyua kwake, yaani mpaka leo Yesu yupo Mbinguni, Ila Muhammad ambae tunaaminishwa kuwa ni mbora yeye alikufa, tena kwa ugonjwa wa homa, yumo kaburini amekwisha kuoza, sasa hapa nani Mbora kati yake na Yesu?, Je Yesu aliye hai tena yupo mbinguni, atakuwa chini ya ubora dhidi ya marehemu aliye kaburini ambae hajui cho chote ambacho kinaendelea duniani?
Hivi Waziri mkuu ambae yeye ofisi yake ipo Ikulu, na yupo karibu na Raisi, anaweza kuwa chini ya Mkuu wa WILAYA, AMBAYE ofisi yake haipo Ikulu? Muhammad angekuwa mbora Mwenyezi Mungu asingemnyanyua kwake, halafu Yesu akwaa kaburi mpaka leo? Ni maswali ambayo yaliniumiza kichwa,
Siku moja wakati nasoma Biblia, nikakutana na andiko hili
1 Yohana 2: 1 Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,
2 naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.

Niliposoma andiko hili nikakumbuka kuwa sis I huwa tunamswalia, mtume, na wakati wa Sala, kwenye ATAHIYATU, HUWA TUNASEMA,
‘Mola wetu mrehemu Muhammad, na jamaa zake Muhammad, kama ulivyomrehemu Ibrahimu, na jamaa zake Ibrahimu, kama ulivyo mrehemu Ibrahimu na jamaa zake Ibrahimu, Umbariki Muhammad, na jamaa zake Muhammad, kama ulivyo mbariki Ibrahimu na Jamaa zake Ibrahimu……”
Nikajiuliza, kama kweli Muhammad ni mbora kuliko Ibrahimu, ni kwa nini tumuombee Rehema Muhammad kama za Ibrahimu? Ni kwa nini tusimuombee Ibrahimu rehema kama za Muhammad? Ina maana hapa Muhammad rehema hana, pia kama Ikiwa Ibrahimu yupo chini ya Muhammad, ni vipi tumtakie Baaraka kama Ibrahimu? Hivi kweli inawezekana Wanachama cha Mapinduzi kwenda kumuombea Muheshimiwa Pinda kwa Raisi Kikwete, ampe Pinda Mamlaka kama ya Mkuu wa Wilaya? Pinda na Mkuu wa Wilaya nani mwenye mamalaka zaidi? Na kwa nini Sisi tumuombee Kipenzi cha Mwenyezi Mungu, tena mbora wa mitume, badala ya yeye kutuombea sisi kwa Mungui? Hivi ni mtume gani au nabii gani ambae aliwahi kuombewa rehema na wafuasi wake kwa Mungu zaidi ya Mtume Muhammad? Nikasema, bila shaka hapa, tunauziwa mbuzi kwenye gunia, kila siku tumswalie mtume, sisi atatuswalia nani?
Nikazidi kuwa na mashaka na Mtume Muhammad, nikasema moyoni, ikisemwa, tumswalie (Tumtakie Rehema) Mtume, mimi nitakuwa nauchuna, nikafikiri Mtu keshakufa, ni kwa nini tuendelee kumuombea Rehema? Ikiwa huyu ni kipenzi cha Mungu, ni kwa nini Mungu alishindwa kumrehemu mpaka tupewe kazi hiyo ya kumtakia rehema, Mbona Yesu yeye ndiye muombezi kwa watu wake, kwa nini Kipenzi cha Mungu na mbora wa mitume asiwe muombezi badala yake awe muombewaji? Nikainuka, Nikasema, ngoja niende kwa Sheikh RAMADHANI pale Taqwa, ili nimuulize swali Hili, Nafika pale, nikakutana na Imamu, ABDALLAH PANYA, nikasema, Yes, naanza na huyu….. UTAENDELEA,
SEHEMU YA 6, UJUE KILIJIRI NINI BAADA YA KUKUTANA NA IMAMU

Comments