NI KWA NINI NILIAMUA KUACHANA NA UISLAMU NA KUWA MKRISTO?” SEHEMU YA 7


Na Mtumishi wa MUNGU, Abel Suleiman Shiriwa.

Ushuhuda wa ajabu sana unaendelea, na kama kukusoma sehemu zilizotangulia basi Sehemu ya kwanza FUNGUA HAPA Na Sehemu ya pili FUNGUA HAPA Na kwa sehemu ya tatu FUNGUA HAPA.
Kwa sehemu ya 4 FUNGUA HAPA
Na kwa sehemu ya 5 FUNGUA HAPA na sehemu ya saba ni FUNGUA HAPA

Kwa sauti ya Hasira, nikakwambia Mzee, “Kwani ni lazima uende na mimi Kuswali” Akaniambia, “Ni kwa nii unanijibu kwa ukali hivyo? Kwani kunisubiri tukaenda wote msikitini kuna tatzo gani?” Sikumjibu, Nikona nisipoenda kuswali, na wakati nimewaaga naenda huko itakuwa tatizo, nikaamua, niende Kuswali swala ya Magharibi kwanza, kisha baada ya kuswali, nikamwambia, Mzee, “Me naenda zangu kwa kwa Ahmad” Akasema, “Pouwa, me naenda kufundisha wanafunzi wangu Quran, Halafu kwa nini Abubakari siku hizi Umeacha kufundisha Madrasa kama ulivyokuwa mwanzo?” Nikamwambia, “Nimeamua niendelee kusoma zaidi halafu ndo nitaendelea kufundisha?” (Hakujua kama mimi niko busy kusoma Quran na Biblia, Ili kuutafuta Ukweli) Akaenda zake, nami nikatembea mpaka GREEN VIEW nikapanda gari mpaka Nyamanoro, Nikashuka, nikapanda kwenda Ibungilo Kanisa la AICT walipokuwa wanafanyia mkutano kina Ernest, Kufika kule sikuwakuta, Nikamuuliza mama moja aliyekuwa anauza Dukani, ni Muislamu anaitwa, Mariamu, “Hawa Jamaa leo mbona wamemaliza mapema?” Akasema, “Wametangaza kuwa leo ndo siku ya mwisho, kesho watakuwa wanaelekea Sehemu nyingine” Nikamuuliza, “Sehemu gani?” akasema, “MISUNGWI” Nikamuaga nikaondoka zangu.
Nikafika home, nikaenda kuoga, nikakaa sebuleni kusubiri nile, Kisha niingie chumbani nijisomee, na kweli ikawa hivyo, Moyoni mwangu, bado nikawa na shauku ya kutaka kukijua hicho kitabu cha uzima kikoje, nikachukua Daftari ambalo Nilikuwa naandika maandiko ambayo nilikuwa nayasikia kutoka kwa Kina Mazinge, Ili niyasome, kwa makini, maana maandiko yao mengi ambayo niliyachukua kwako, nilipokuwa naenda nayo kwenye Mihadhara ya Kikristo nilikuwa nabawa nayo, Pitia pitia yangu, nikakutana na andiko hili.
1 Korintho 15:18 Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea.
19 Kama katika maisha haya tu tumemtumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote.

Nikastuka, nikawa najiuliza, Hili andiko Wahadhiri wengi wa Kiislamu walilitumia kuwasilimishia Wakisto wengi, Nikasema, Kumbe Wakristo, wamepotea tena ni masikini kuliko watu wote Nikaona moyo wa kupenda kuwa Mkristo umeanza kuuondoka, nikabaki njia panda, Uislamu nimeshaanza kuustukia, Huku nako tena ni hivi, nikaendelea kujisomea BIBLIA zaidi huku moyo wangu hauna furaha, Nikawa nasoma Kitabu cha Yohana, nikakutana na hili andiko.
Yohana 6:37 Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.
38 Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka.
39 Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika wote alionipa nisimpoteze hata mmoja, bali nimfufue siku ya mwisho.
40 Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.

Nikaanza kutafakari, mbona kule tumeambiwa, waliolala Katika Kristo Yesu wamepotea, Huku Yesu anasema, aendae kwake, hatopotea, na tena yeye ndiye atakae mfufua siku ya Mwisho, sasa hapa kukoje? Lipi andiko sahihi? Sikupata Jibu, nikajisikia kuchoka, nikaamua kulala zangu, Asubuhi kama kawaida School, Nikiwa Darasani, Mawazo yangu yapo tu kwenye yale maandiko, Wakati naendelea kufikiria, Maneno ya Ernest yakaanza kunijia, yale aliyotoa andiko la 1 P etro 3:15-18 Kuwa, kuwa, Katika Nyaraka za Mtume Paulo, yapo mambo ambayo ni vigumu kuelewa, nayo, na katika mambo hayo watu wasio na Elimu, huyapotoa, kama wapotoavyo maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe….. Nikajisemea Moyoni, “Kama ikiwa maandiko mengine waliyokuwa wanayasoma Kina Mazinge, niliyokuwa nayaandika, baada ya Kufundishwa na Wahubiri wa Kikrito, nikagundua kuwa walikuwa wanayapotosha, Kuna uwezekano mkubwa, kabisa hata lile la 1 Kor 15:18-19 Likawa linapotoshwa, akili yangu ikawa inanilazimisha nirudi home, nikachukue tena BIBLIA nisome, Ili nijue hakika yake, maana kama nilikuwa nimeshaanza kutamani kuwa Mkristo, Kwa nini andiko hilo liwe Kikwazo? Nikajisemea, kama Kina Ernest wangekuwepo ningeenda kuwauliza, lakini hawapo nitamuuuliza nani? Nikatoka nikaenda kwa Mwalimu nikamuomba Ruhusa niende nyumbani, maana sijisikii vizuri, kweli nilikubaliwa, huyo nikaenda zangu home, Kufika Home, nikasalimia kama kawaida, halafu nikaingia zangu chumbani, nikachukua Biblia na kulifungua lile andiko, Nikasema ngoja nianze 1 Kor 15:12 mpaka mwisho Kufikia aya ya 15 Nikaduwaa tena, inasema.
1 Korintho 15:15 Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi.
Nikasema, Kumbe ni kweli Nabii Isa hakufa, Nikaifunga Biblia, nikajilaza, baadae nikachukua tena, na kufungua, nikawa nimefungua Ufunuo Nikaanza kusoma kuanzia mstari wa kwanza, nikwa naendelea nayo, Kufika mstari wa 17 Nikapata kitu hapo, Ngoja niinukuu.
 Abel Suleiman Shiriwa.
Ufunuo 1: 17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.

Hapo nikakapaguvu ya kuendelea kuisoma Biblia, nikajiuliza, Kule nimesoma kuwa, Waliosema Kristo amefufuka ni mashahidi wa uongo, Mbona hapa naona hapa Yesu amesema, alikufa na akafufuka, sasa ni vipi? Ngoja nirudi kusoma kule kwa Wakorintho, niliporejea kusoma, ki ukweli naweza kusema Mungu, alikuwa na makusudi nami, kwani niliweza kuelewa kusudio la andiko lile, nilianza kuisoma kuanzia aya 1 Mpaka 20, Kuanzia 12 Nikaanza kutafakari aya kwa aya, nikaelewa, tena nilielewa bila hata kufundishwa na Mkristo ye yote, ngoja ninukuuu uone nilivyoweza kuelewa.
1 Korintho 15: 12 Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu, mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu?
Hapa Paulo, alikuwa anawaambia baadhi ya watu ambao walikuwa wameamini kuwa Yesu alikuwa amefufuka, wakatokea baadhi ya wengine wakisema, hakuna kiyama ya wafu, yaani wafu hawatofufuliwa, akawa anawauliza kwa nini baadhi yao wana hubiri kinyume?
13 Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo naye hakufufuka;
14 tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure.

Hapo Paulo, anawakumbusha kuwa, kama kiyama haitokuwepo, basi Kristo nae, hakufufuka, na kama ikiwa Kristo hakufuka, basi mahubiri yote ambayo aliyahubiri yeye pamoja na Mitume wengine kuwa Kristo amefufuka, basi ni mahubiri yasiyo na faida, maana kile ambacho wamekihubiri ni Bure, kwa sababu kama wafu hawafufuliwi, Kristo atafufukaje?, sasa basi wao waliohubiri hivyo wameonekana kuwa ni mashuhuda wa Uongo wa MUNGU, kama anavyosema hapa.
15 Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi.
16 Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo naye hakufufuka.

Tena hapo akaeleza vizuri kuwa, Ushahidi wao huo utathibitika kuwa ni wa uongo, iwapo tu kama Kristo hakufuka, maana kama wafu hawana ufufuo, Kristo nae hakufuka, Ina maana Kama Ikiwa Kiyama ya wafu Kipo, na ya kuwa Kristo amefufuka, Je watakuwa mashahidi wa uongo tena? Jibu ni ‘Hapana’ Akazidi kuwasisitizia kuwa, Kama hao watayashika hayo mafundisho ya watu wengine kuwa Kiyama ya Wafu, haipo, na kwamba Kristo hakufuka, basi, Imani yao ya Ufufuo na tumaini lao kwa Yesu litakuwa Bure ndo maana akasema,
17 Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu.
Sasa Kama Kristo Hakufuka, imani yao ya kazi gani? Kama kuna watu wamelala (Wamekufa) Katika Kristo wakiwa na Imani kuwa Yesu alipokufa alichukua mizigo yao, walisamehewa dhambi zao na kuoshwa kwa damu ya Yesu Msalabani, basi watakuwa bado wamo katika dhambi zao, maana Yesu huyo ambaye wao wana amini kuwa, amekufa na kufufuka, wakati sivyo hivyo, basi bado wamo katika dhambi zao, maana mwenye kuwafsisha kwa damu hajafa,tumaini lao li wapi? Kwa hivyo wamekufa, wangali na dhambi zao, mtu ukifa katika dhambi, ni lazima uwe mpotevu, ndipo akasema tena Paulo,
18 Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea.
19 Kama katika maisha haya tu tumemtumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote.

Kwa hivyo, Paulo akazidi kuwasisitiza kuwa, Hao ambao wameshalala, wakiamini kuwa Yesu amekufa, hali ya kuwa baadhi yenu mmeshaanza kusema hakufa, na kama ikiwa kweli, basi hao wenzenu, wamepotea, na sisi ambao tupo hai tunaamini kuwa Yesu kafa na kufuka, na wakati hakufa wala kufuka, basi tu Masikini kuliko watu wote, (Masikini katika imani) Kwa sababu wengine imani zao zina amini kuwa Baada ya kufa, kuna kufufuka, halafu sisi tulio ndani ya Kristo, tunaamini hakufa wala hatofufuka, sasa tutapata wapi Tumaini? Tutakuwa wageni wa nani siku ikitokea wafu wakafufuliwa, halafu sisi Kristo wetu akaendelea kuwa kaburini, hamuoni kwamba hatutakuwa na kitu? Wenzentu watapata faraja kuwaona viongozi wao wakiwa na uhai tena baaada ya kufufuliwa, Mwisho Paulo, akawatoa wasiwasi kuwa, Wasikubali mafundisho hayo Potofu, maana msingi wa kweli ni huu.
20 Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala.
Nilipomaliza kuisoma aya hiyo ya 20 Kuwa Kristo amefufuka, Nikasema, Kumbe, Wahadhiri wengi wa Kiislamu hufanya upotoshaji mkubwa wa maandiko, Wanasoma maandko kwa kuyakata, Ili watu wajue kuwa wana elimu, na nikagundua kuwa, Wakristo wengi wanao silimishwa kwa kupitia maandiko ya Biblia, huwa hawayasomi kwa kuyaelewa, na pengine Biblia hawaisomi kabisa, Kama ikiwa mimi tu ni muislamu, nimeweza kuisoma kwa kutaka kuelewa, kuna baadhi ya mambo nimeweza kuyaelewa, Je wao ambao wako nayo Biblia, itakuwaje si zaidi yangu?
Basi tokea hapo Hata Thaqaafa, nikawa naenda kwa kusua sua, Maustadhi ninapokutana nao wananiuliza mbona Aboubakari siku hizi huji Mara kwa mara Madrasa?, nikawa nawajibu kuwa, Nitaanza kuja kama zamani, Ilipita miezi kadhaa, Nikiendelea kuisoma Biblia kwa makini ili nijue undani wa Yesu, niujue uwezo alio nao, Kitabu cha Yohana, nilikuwa nakipenda sana, Siku moja nilisoma andiko hili
Yohana 3:35 Baba ampenda Mwana, naye amempa vyote mkononi mwake.
36 Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.

Andiko hili ki ukweli nakiri mbele zenu, na mbele za Mungu, lillifungua zaidi na kunifanya nijue ni kiasi gani mpango wa Allah na Muhammad, kuwapeleka watu motoni, nikagundua ni kwa nini Muhammad aliwaita Wakrisro makafiri kwa kusema Yesu Yesu ni Mwana wa Mungu, maana Quran inakataza kusema Yesu ni Mwana wa Mungu,
Quran 18:4. Na kiwaonye wanao nena: Mwenyezi Mungu ana mwana.
Nikajua kumbe ujio wa Quran ni kuja kuwaonya watu wasiseme kuwa Mungu ana mwana, na isitoshe Quran imekuja baada ya Yesu Kuondoka, Kama Quran ingetangulia kuja Kabla ya Yesu, na ikasema kuwa, Mungu hana Mwana Mwana, basi ningemuona Yesu Muongo, lakini Yesu ndo katangulia, Muhamamad akafuata,nani, Nikaonana, Hapa kuna fedha moja ni halali, na moja bandia, Sasa katin ya fedha bandia, na Fedha halali, Ipi iliyotangulia? (Akili kumkichwa) Nikasema, Kumbe lengo la kuja Quran ni kuwafanya watu wasipate Uzima wa milele bali moto wa Milele, na pia kuwafanya watu wakaliwe na ghadhabu ya Mungu, maana Yesu amesema kuwa,
Yohana 3:35 Baba ampenda Mwana, naye amempa vyote mkononi mwake.
36 Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.

Inamaana kitendo cha mtu kutokuamini kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, tayari hana uzima, ila mtu ambae atawamini Mwana Huyo ndiye mwenye Uzima, asiye mwamini Mwana Ghadhabu ya Mungu inamkalia, Nikasema, Kumbe hapa nilipo katika Uislamu Ghadhabu ya Mungu inanikalia kwa sababu sijawamini Mwana, NikiFUNGA mwezi wa Ramadhani, nikitumaini kupokea thawabu kwa Mungu, kumbe hakuna kitu bali ghadhabu ya Mungu iko juu yangu, Kumbe Muhammad kaja kutupotosha tuseme kuwa, Yesu siyo Mwana, ili Ghadhabu ya Mungu iwe juu yetu,, tena kwa kufuata kauli ya majini ambayo ndo yalianza kutangaza kuwa Mungu hana Mwana.
Quran 72:1. Sema: Imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini lilisikiliza, na likasema: Hakika sisi tumeisikia Qur'ani ya ajabu!
2. Inaongoza kwenye uwongofu, kwa hivyo tumeiamini, wala hatutamshirikisha yeyote na Mola wetu Mlezi.
3. Na kwa hakika utukufu wa Mola wetu Mlezi umetukuka kabisa; hana mke wala mwana
Nikasema, kumbe tunaminishwa kuwa kusema Yesu ni Mwana wa Mungu, ni Ukafiri ili tusitamani kwenda kwa Kristo kwenye Imani ya Uana, Kumbe lengo lao Sisi Waislamj tuzidi kukaliwa na ghadhabu ya Mungu, maana Muhammad alijua kuwa mtu akimkiri Yesu atakuwa na uzima, Ili kuwazuia watu wasitoke kwenye Wasitoke kwenye Uislamu, akasema.
MWENYE KUACHA UISLAMU AUAWE
Ibn Umar (r.a) amesimulia kuwa:Mtume (s.a.w) amesema,"Mwenye Kulitadi (atakayetoka kwenye Uislamu) basi muueni."
(Bulugh Al Maram,hadith no.1031,uk.461)

Nikasema hapa nlipo nimepotea, Nikaanza kukumbuka ahadi za Muhammad kupitia Quran zinapingana na Ahadi za Yesu aliyetangulia, mfano mzuri huu hapa.
Yesu amesema, Mbinguni hakuna kuoa wala kuolewa..
Luka 20: 34 Yesu akawaambia, Wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa;
35 lakini, wale wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na kule kufufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi;
36 wala hawawezi kufa tena; kwa sababu huwa sawasawa na malaika, nao ni wana wa Mungu, kwa vile walivyo wana wa ufufuo.

Muhammad yeye anasema kuna kuoa na kuolewa.
Quran 52:20. Wakiegemea juu ya viti vya fahari
vilivyopangwa safu, na tutawaoza wanawake
weupe wenye macho mazuri.

Nikajisemea, kama huyu angekuwa wa Mungu kweli, basi angeneda sawa sawa na alivosema Yesu, maana hakuna mwingine mwenye kuweza kuyatengua maneno ya Yesu hata ifikapo siku ya Mwisho.
Mathayo 24: 34 Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia.
35 Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

Na kwa kuwa Maandiko mengi nilishayasoma, nikakumbuka hili andiko,
Yohana 5: 25 Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai.
26 Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake.
27 Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni Mwana wa Adamu.
28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.
29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.

Nikaona ni wazi kuwa, Kwenye Uislamu siyo sehemu salama kabisa, maana Watu hawatafufuka bila kuiskia sauti ya Mwana wa Mungu (YESU), na ikiwa ambae hamwamini Mwana Siku ya Ufufuo ataenda kwenye ufufuo wa hukumu, Muhammad na sisi Waislamu ambao tunakataa kuwa Yesu siyo Mwana wa Mungu, tutakuwa wageni wa nani siku hiyo? Nikabaini wazi kuwa, Yesu ndiye mwenye kuwafufua watu siku ya mwisho, kama ataamua amuache Muhammad kaburini, (Asimfufue) me nikiwa muislamu nitaenda kwa nani wakati Kiongozi wangu bado yumo kaburini? Nikawaona Wakristo wane kiongozi mzuri, ambaye atasimama nao siku hiyo, baada ya kutafakari hayo, nikasema, Kina Ernest nitawapa wapi? Baada kupita siku 4 Wakati nipo home, Ahmad akaja akaniambia, “Wale Makafiri wamerudi tena Kule Nyamaonoro AICT jana nilienda kuwauliza maswali, Moyo wangu Ukalipuka kwa furaha, Nikamwambia, Leo lazima niende, Ahmad hakujua kuwa Taarifa anayo nipa ni neeema kwangu, Ilipofika mida ya sa 9:30 A lasiri, huyo nikapanda zangu kwenda Ibungilo Nyamanoro kwenye Mkutano wa Kina Ernest na Mjuni, Kufika pale nikawakuta ndo wanatoa Spika zao Nje, waanze kufunga Vyombo Waanze Mkutano, Nikazunguka Nyuma ya Kanisa kumwangalia Ernest……. UTAENDELEA,
USIKOSE SEHEMU YA  YA USHUHUDA HUU,

Comments