KWA NINI NILIAMUA KUACHANA NA UISLAMU NA KUWA MKRISTO?" SEHEMU YA 9

Na Abel Suleiman Shiriwa
Ushuhuda wa ajabu sana unaendelea, na kama kukusoma sehemu zilizotangulia basi Sehemu ya kwanza FUNGUA HAPA Na Sehemu ya pili FUNGUA HAPA Na kwa sehemu ya tatu FUNGUA HAPA.
Kwa sehemu ya 4 FUNGUA HAPA
Na kwa sehemu ya 5 FUNGUA HAPA na sehemu ya 7 ni FUNGUA HAPA
ILIPOISHIA:
Nikafungua mlango ili nijue naitiwa nini, nikatoka huku natetemeka, nikamkuta mama amesimama huku ananiangalia kwa hasira, akaniambia, "Heshima imeenda wapi siku hizi? umekuja ukiwa umechelewa, nakufungulia mlango, bila hata salamu unapitiliza kwenda chumbani ndo tabia gani hiyo?" Nikamwambia, "Samahani mama, nakubali nimekosea kwani kweli sijakusalimia" Nikamsalimia, akaitikia , Akaniuliza, "Mbona leo umechelewa kurudi na chakula huli?" Nikamjibu kuwa, "Mama hapa nilipo naumwa sana, kwani hunioni ninavyotetemeka? bila shaka itakuwa ni Malaria"
Ajanipa pole, akasema "Kachukue dawa umeze" Nikamwambia, " Usijali mama, انشا الله nitapona kwa uwezo wake mwenyezi Mungu, (Kumbe mwenzenu siumwi wala nini ni hofu tu) Akaniambia, "Sawa ila nilichokuuliza hujamijibu kwa nini leo umechelewa kurudi?" Nikamwambia, "Wale makafiri leo wameendesha mpaka usiku sana, nijaona kama nitaondoka mapema, watajihesabia ushindi, nikaiangusha DINI ya mnyazi mungu" Akasema, nilikasirika sana kuona umechelewa, umemiweka katika mashaka maana siyo kawaida yako kuchelewa, haya kalale kama utaendelea kuumwa, kesho tutaenda hosp" huyo akaenda chumbani, nikashusha pumzi, nikasema, Afadhali kumbe hajajua kama leo nimeachana na uislamu.
Nikaenda chumbani, usingizi ukawa umegoma kabisa, nikaanza kujihisi kama nipo ndotoni, siamini kile ambacho kimetokea, "Hivi kweli leo nimekuwa Mkristo? au naota?" ilinichukua muda mrefu kupata usingizi, asubuhi nilipoamka nikawa ni mwenye mawazo, Mama alipoamka tukasalimia, akaniuliza hali yangu vipi? Nikamwambia niko vizuri, Nikasubiri mida ya kunywa chai, nikanywa, nikasema, ngoja nipandishe kwa kina AHMAD nikamuone nijue kama nae ameshajua kama nimeritadi au vipi! kweli nilipoenda nilimkuta, nikamsalimia, nikakwambia, اخي كيف حالك?(Ndugu yangu vipi hali yako) Akanijibu, nzuri, nikamchombeza, "Vipi umeshasikia chochote uhusu ule muhadhara wa makafiri"? akasema, "Hapana sijasikia cho chote" moyoni nikwa nafuraha, Nikamwambia, "Leo wametangaza kuwa hawatakuwepo wanaenda sehemu nyingine (Ili Ahmad asije akaenda kule issue ikabumbulika) Akasema, "mimi mwenyewe nilikuwa na mpango wa kwenda huko leo, ahsante kwa kunijuza" Nikamwambia "Ndo hivyo bhana, mimi mwenyewe nilikuwa nataka niendelee nao lakini ndo.hivyo tena" Tukapiga stori muda swalq ukafika, Ahmad akaniambia" twende zetu kuswali" nikamwambia, "Unajua wakati nakuja huku mkojo ulinibana sana, kufika kwenye kile kichochoro cha kupanda huku kwenu, ikabidi nikojoe, nikakosa maji ya kustanji, hata jiwe nalo nikasahau kutafuta nina wasi wasi kaptura yangu ikawa na chembe chembe za mkojo, kwa hivyo ngoja niende home nikabadili kisha nitakuja kuswali, japo kuwa nitachelewa na kukosa daraja 27 kupitia
صلاة الجمع
Ahmad akasema, sawa, akaondoka kwenda masjid, me nikaenda zangu home, nilikwepa kwenda kusali, Jioni nikasema, nitaenda kwenye mkutano, ili nijue kinaendelea nini (Wakati huo nina hofu kubwa ya kufukuzwa nyumbani) kama watajua wakati huo bado sijawa na uwezo wa kujisimamia, nikasema, ni lazima nionyeshe matendo ya kiislamu waendelee kujua mimi ni mwenzao, mpaka pale nitakapo pata mpenyo wa kuondoka hapa home, (Waislamu hurudi kwenye uislamu kwa sababu hiyo) Nikataka niende saa 10 kwenye mkutano nikasema, ni mapema ni kheri niende saa 12:30 Jioni jioni ili nikute waislamu wametawanyika, maana nilijua tu ni lazima watakuja kwa wingi baada ya tukio la jana la mimi kuachana na uislamu, kabla sijaenda kule, nikaenda Kilimahewa kwenye maduka ya nguo, nikanunua sweta lenye kofia, na kapero kupitia hela ambayo nilipewa baada ya kutunzwa, nikanunua nikavaa nikaishusha kofia, huyo mguu wa mguu kuelekea Nyamaoro, nikapita njia ya JESHINI kuelekea IBUNGILO, kufika karibu na kanisa nikakuta umati mkubwa wa watu, Waislamu wamesimama wanaangalia na kusikiliza, nikazunguka mpaka nyuma ya nyumba ya mchungaji, nikakaa kule nyuma giza baada ya kuingia ndo nikaenda mezani kwa kina Ernest, basi nikaifunua kofia, nikawasalimia, wakafurahi sana, (Ile kapero nikaiwekaa kwenye mfuko) ERNEST akaniambia, "Abubakari Unajua Wakristo wamekusubiri sana" nikamwambia, "Ngoja niwasalimie ila sitokaa sana, nawahi home ila kesho nitawahi kuja" nikawasalimia Wakristo nikawaambia sasa hivi mimi ni mteule" wakashangilia sana, huku waislamu wakininyooshea vidole, baada ya salamu nikajiuliza nitaondokaje hapa?" Nikaingia kanisani, nikatokea mlango wa pili huyo nikatoka bila waislamu kuniona, mpaka nyumbani,
Kesho yake sikwenda kule kwenye mkutano, kwa hofu ya kugundulika kama nimeritadi, nikafukuzwa home mpaka ule mkutano unaisha sikwenda kabisa, hata kwenda msikitini nikawa nakwepa, pia kanisani nikawa siendi, ila moyoni mwangu, napenda sana kwenda kanisani, ila tu mazingira ya pale home hayakuwa yenye kuniruhusu, Basi mwezi wa ramadhani ukafika, nipo home, ikanilazimu nifunge ramadhani, na usiku tukawa tunapiga dufu, kuwaamsha watu wale daku, katikati ya mwezi huo wa Ramadhani, nikaenda tena kule kwenye kanisa la AICT NYAMORO, nikamkuta mchungaji Machibya, akanikaribisha ndani nikaingia, Akawaagizia wanae waniletee soda, nikamwambia hapana nimeshiba sana (Kumbe nimefunga) akaniambia mbona huonekani? nikamwambia "Nilikuwa safarini" wakati tunaongea nikawa napiga miayo ya njaa, baadae nikamuaga ili niwahi kwenda kufuturu,
Siku moja wakati tunapiga dufu, kuwaamsha watu wale duak, Kuna wimbo wa Qaswida nikawa nauimbisha, unasema hivi:
Yatakayokutokea zama zama kutokwa roho x2 kwanza vyote huagana viungo vya mwili, kila kiungo shahidi siku hiyo ikitimu
Kwanza atakutokea malaika wa mema, shetani ulimkana na mwenyezi kumtii hayo ndiyo mema yako uliyotenda mwenyewe
Pili atakutokea malaika wa mabaya x2 shetani hukumkana na mwenyezi kumtii hayo ndo mabaya yako uliyotendea mwenyewe,
Ile kufika sehemu ya tatu ambayo inasema:
Tatu atakutokea Malaika wa maji x2 Kama wewe mwema ladha yake utaonja, na kiu itakatika kwa kuyanywa mara moja.........
Kabla sijamaliza kuimbisha, ukafunguliwa mlango pembeni ya mlango ya mlango ule ambao tulikuwa tuwaamsha, akatoka mschana mmoja anaitwa Tatu, ni Mkristo, na anafahamu kuwa nimeshaachana na uislamu maana alikuwa ana hudhuriia sana mikutano ya kina Ernest, na ambao tulikuwa tunapiga dufu tulikuwa watu 7 Sita tuna dufu, mmoja sahani ya hela. akiwemo AHMAD na mzee,
Tulivyogonganisha macho yetu mimi na tatu, Nikajiuliza ametoka baada ya kusikia naimba, "Tatu atakutokea malaika wa mabaya, akajua ni tatu yeye?" nikaona hapa sasa limesha sanuka, tatu ataniumbua kwa wenzangu wajue kuwa nimeshakuwa Mkristo, halafu home kukasanuke; Nikitimuliwa nitaenda wapi? nikaacha kuimba nikageuka pembeni nisimtazame TATU, maana akili imeshavurugika, nikasema, hapa cha kufanya nikuitupa dufu (ngoma) kisha nitoke nduki kabla Tatu hajanisemesha.......... UTAENDELEA
Usikose sehemu 10 ujue kilitokea nini.

Comments